Uchaguzi huru wafanywa Tunisia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi huru wafanywa Tunisia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanakili90, Oct 23, 2011.

 1. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wananchi wa Tunisia wanapiga kura leo
  kuchagua bunge litalotayarisha katiba mpya na
  kumteua rais wa muda. Tunisia ilikuwa ya mwanzo kuanza ghasia za
  mabadiliko katika nchi za Kiarabu baada ya
  kijana mmoja, Mohamed Bouazizi kujichoma
  moto, kupinga dhuluma za uongozi. Huu ndio uchaguzi wa mwanzo huru tangu
  Tunisia kupata uhuru kutoka kwa Ufaransa
  mwaka wa 1956, na uchaguzi wa mwanzo
  tangu maandamano ya mabadiliko kuanza katika
  nchi za Kiarabu. Watunisia wanafanya uchaguzi haraka, miezi 10
  tu baada ya dikteta Zine al-Abidine Ben Ali
  kuondoshwa. Vyama zaidi ya mia moja vinashiriki,
  kimojawapo ni cha Kiislamu, ambacho kilipigwa
  marufuku na Ben Ali, na ndicho kilichojitayarisha
  vema. Kinatarajiwa kupata kura nyingi kushinda chama
  chochote kile. Kampeni kwenye internet inakiponda chama
  hicho kuwa kina msimamo mkali, lakini viongozi
  wake wanasema wanapinga utawala wa
  Kiislamu na wanataka uwazi, uvumilivu, na nchi
  kutokuwa na chama kimoja kitachogubika
  vengine. Vyama visivokuwa vya Kiislamu piya
  vinatarajiwa kufanya uzuri. Kampeni zao zilihusu maswala ya kiuchumi,
  kijamii, biashara za kibinafsi, ajira na usawa. Watu ndani ya nchi na katika nchi za Kiarabu
  wanataraji mengi kutoka Tunisia, kwa sababu
  Tunisia ndio iliyoanzisha maandamano ya
  mabadiliko. Na wananchi wenyewe wana hamu kuwa nchi
  yao ifanikiwe.

  Source:BBC
   
 2. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,084
  Trophy Points: 280
  Inatia moyo kuona wananchi waliokuwa wamekandamizwa na utawala wa kiimla leo wanapata fursa muhimu ya kupiga kura kidemokrasia. Tawala zilizotumia ulaghai na mbinu mbalimbali zikiwepo za kidini kogofya raia hatimaye zimefikia mwisho.

  By the way, akina mama wanaruhusiwa kupiga kura? Kama ndivyo, basi utakuwa ni ukombozi mkuu kutoka makucha ya tawala (za mashariki ya kati) zina(zili)-zoamini mwanamke ni mwanadamu wa daraja la pili. Nasikia hata huko Saudia na Kuwait nao ama wameanza au wanafikiria kuruhusu wanawake kupiga kura.

  Mwenyezi Mungu awe upande wao, wavuke kwa salama.
   
 3. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hahaha umeona idadi ya vyama vya upinzani?hahaha tz havizid 20 je tunisia?
   
Loading...