Uchaguzi DARUSO wana UDSM mjitafakari

amos eglan

JF-Expert Member
Sep 27, 2015
310
462
Wakati chuo kikuu cha udsm kikielekea kwenye uchaguzi wa serikali ya wanafunzi daruso ambayo kwa siku za karibuni imekosa msisimko tofauti na miaka ya nyuma ambapo ilkuwa daruso inatoa viongozi imara wanaoweza kulikemea taifa na kutetea maslahi ya wanafunzi si udsm pekee Bali Tanzania nzima..

Tofauti na sasa ambapo serikali na jamii imekuwa ikifanya uozo mwingi wamekaa kimya wanafunzi Tanzania wananyanyasika na TCU na bodi ya mikopo kwa kunyimwa haki zao na wanakatisha masomo wapo kimyaaa nambaya zaidi hii inatokana na kuingiza siasa zaidi kuliko maslahi ya wanachuo na taifa yaani wasomi wanajigawa kutokana na itikadi zao binafsi za kisiasa kutumika na wanasiasa

Pia watu ambao wengi wao lengo Lao ni kutaka kufanya uongozi huo Kama daraja La kujitengenezea CV ili watakapo maliza wajue kwamba CV zao zimenona maana waliongoza umma wa UDSM hawa ndio wengi na hawana dhamira ya dhati Bali kujitengenezea majina ya kisiasa tu..

Rai yangu chagueni viongozi watakaoweza kuwatetea Kama wanafunzi nchi nzima na si kuwa wabinafsi na achaneni na hao wanasiasa uchwara wanaotaka kujijenga ki siasa kwa kupiga porojo nyingi na mchague watu wasio na uoga wa aina yeyote wala wasioendeshwa na wanasiasa uchwara Daruso ni taasisi kubwa ambayo inazidi kupoteza mvuto wake
 
Nawatakia kila la kheri vijana makin wa chadema waliochukua fomu

Hakuna mgombea yeyote wa ccm atakaesimamia maslahi ya wanachuo

Vote for change
 
Nafikiri ipo haja kwa vijana hao kujiunga kwa pamoja na kusimama kwa lengo la kuweka maslahi ya Wanachuo kwa ujumla na si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom