Uchaguzi CCM: Siri zaanza kufichuka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi CCM: Siri zaanza kufichuka!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 27, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  *Yabainika mawaziri walivyotetea wapambe wao
  *Samuel Sitta asema Lembeli ni rafiki yake tu
  *Nape: Tutawaondoa wala rushwa mara moja

  Mtanzania | ALHAMISI, SEPTEMBA 27, 2012 | DEBORA SANJA, DODOMA NA BENJAMIN MASESE, DAR

  WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikimaliza vikao vyake vya juu mjini Dodoma, siri nzito zimeanza kufichuka, namna ambavyo baadhi ya wajumbe walivyokuwa wakihangaika kutaka wapambe wao wapitishwe kwa kila namna.

  Vikao hivyo ni pamoja na Kamati ya Maadili, Mkutano Mkuu na Halmashauri Kuu ya Taifa.

  Habari za kuaminika zilizopatikana jana, zinasema mvutano huo uliibuka baada ya wajumbe kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, kung'ang'ania kwa nguvu zote kuhakikisha wapambe wao wanapitishwa.

  "Ndugu yangu vita ilikuwa kubwa mno, kuna mmoja wa wajumbe ambaye ni waziri katika Serikali yetu (jina tunalo), alipambana mpaka jasho likamtoka, akitaka safu yake iingie kwa nguvu,…wapambe wake hawa ni wabunge ambao wanajiita wapambanaji wa ufisadi, unajua huwezi amini, lakini wameangukia pua, mwenyekiti wetu alitumia busara za hali ya juu, …pamoja na njama zote hizi, nakwambia chama kimetenda haki ya kuwachagua wagombea ambao wana sifa zote.

  "Mmoja wa wajumbe, waliokuwa mstari wa mbele kuongoza mashambulizi hayo, ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye alikuwa akitetea jina la Mbunge wa Kahama, James Lembeli ili lipitishwe.

  "Chama kimetenda haki, kimeniokoa mimi binafsi na wengine waliokuwa wamelengwa kuangamizwa, tunashukuru chama na busara zilizotumika kuvunja ngome za maangamizi zilizokuwa zimepangwa.

  "Mfano baadhi ya majina, yalipendekezwa mikoani, lakini muhtasari wa taarifa za majina hayo ulipofikishwa Dodoma, ulikuwa umechakachuliwa, …baadhi ya wajumbe walisimama kidete kutetea muhtasari huo uchukuliwe kama ulivyo.

  "Hali ilikuwa mbaya, kwani ilifikia hatua John Chiligati kuzomewa na wajumbe, baada ya kupinga jina la Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja ambaye alikuwa anapambana na Lembeli," alisema mjumbe huyo.

  Juzi Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alisema uteuzi wa wagombea ndani ya chama hicho, umelenga kuandaa timu ya ushindi wa chama na si ushindi wa mtu binafsi.

  Alisema, anatambua kuibuka kwa mijadala mikali dhidi ya mapendekezo ya wagombea walioenguliwa na Kamati ya Maadili na Kamati Kuu (CC), huku akisisitiza lengo ni kukipa chama uhai.

  Alisema, lengo la uchaguzi huo ni kutafuta viongozi shupavu, jasiri wanaojua kujieleza na watakaosaidia chama kupata ushindi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 na uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

  SAMUEL SITTA

  Alipoulizwa na MTANZANIA, Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta alisema, yeye hakuchangia jambo lolote, zaidi ya kunyoosha mkono na kushusha.

  "Sikuchangia jambo lolote, sikuwa na kundi lolote ndani ya kikao, sikuwa na kampeni, kama ni kampeni ningezifanya kwa mke wangu, lakini hakuwa na misukosuko yoyote kuanzia Tabora hadi Dodoma, …kitendo cha kusema nilikuwa na kundi, wanajua Lembeli ni rafiki yangu… hayo ni maneno ya kupanga baada ya kuona jina la Lembeli halikurudi, hata mimi nilishawahi kupata misukosuko kama hii, nawaomba watu watulie," alisema.

  MKONO ATOA YA MOYONI

  Naye Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM), amesema kamwe hana kinyongo baada ya jina lake kuondolewa kwenye kinyang'anyiro cha nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania.

  Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, ilisema Mkono ambaye amewahi kusema kama asipopitishwa kugombea nafasi hiyo, CCM kutachimbika, alisisitiza hana kinyongo na uwamuzi huo.

  "Nimepokea kwa mikono miwili uwamuzi huu, sina kinyongo hata kidogo, naunga mkono kwa asilimia mia moja uwamuzi wote wa vikao vya uteuzi wa wagombea,

  …kuachwa kwangu hakuna maana kwamba, kuna jambo limekosewa, bali ni taratibu za chama ambazo zimepitia hatua mbalimbali, zikiwemo zile za Mwenyekiti wangu, Rais Jakaya Kikwete.

  "Mimi ni CCM damu, nawaunga mkono wenzangu walioteuliwa, ninatoa ahadi ya kuwapa ushirikiano wa kutosha," alisema Mkono.

  NAPE ALIA NA RUSHWA

  Katika hatua nyingine, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema, NEC imetoa onyo kwa wagombea walioteuliwa, kujihusisha na vitendo vya rushwa.

  Nape aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuwa, chama kimewaonya wagombea kujihusisha na vitendo vya rushwa.

  "Tukimgundua mgombea yeyote anatoa rushwa ili achaguliwe, tutamuondoa kabla hata hajafikia katika huo uchaguzi, marufuku kwa wagombea kwenda kuwatembelea wapiga kura," alisema.

  Alisema, katika majina ya walioomba, walikuwa asilimia 40, huku vijana chini ya miaka 40 sawa na asilimia 50 walitoka vyuo vya elimu ya juu.

  Alisema zaidi ya nusu ya wabunge, walioomba kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hawakuteuliwa.

  Akitaja majina ya wagombea kwa upande wa ujumbe wa NEC viti 10 Bara, Nape alisema waliopitishwa ni, Otieno Baraka, Shy-Rose Bhanji, David Mathayo David, Twalhata Ally Kakurwa, Godwin Kunambi, William Lukuvi, January Makamba, William Malecela, Benard Membe, Salehe Mbwana Mhando, Wilson Mukama, Mwigulu Nchemba, Innocent Nsena, Richard Tambwe, Anna Magowa, Christopher Mullemwah na Mwanamanga Mwaduga.

  Wengine ni Ruth Msafiri, Stephen Wassira, Hadija Uledi Faraji, Dk. Hussain Abdulrehenan Hassan, Nicholaus Haule, Dk. Fenela Mukangara, Nussura Nzowa, Martin Shigela, Dk. Luteni Kanali, Kesi Athuman Tambo, Jackson Msome, Fadhili Nkurlu, Tumsifu Mwasamale, Assumpter Mshama na Rashid Kakozi.

   
 2. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  sita na kundi lake kwisheni.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kama kweli RAFIKI WA HAKI kwa maana ya Mwanasheria,

  Je Kijana mwenzetu Ridhiwani Kikwete, pindi atakaposikia maneno kma haya ATAJISIKIJE MTANZANIA MWENZAKE TENA MAMA MJANE anapozulumiwa kilicho chake eti kwa jina la urafiki na nyumba ya utawala katika nchi yetu?????????????

  Hili jambo lifuatiliwe zaidi ili kumfuta machozi mama huyu na watoto yatima aliyo na jukumu la kuwalea hapo nyumbani kwake.

   
 4. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Sitta ni fighter ukimya wake una kishindo. Ukiona kobe kainama basi ujue anatunga sheria.
  .
   
 5. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Stori za makundi. Kupoteza muda. Unafiki.
   
 6. b

  blueray JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  tunajua mizengwe, uchakachuaji na rushwa ni baadhi ya 'sera' za CCM! Hakuna jipya la maana...
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa CCM , ukoo, ushikaji, UFISADI na uchakachuaji yote ni jadi; iwe ni uchaguzi wa ndani au wa nje ya chama hicho.
   
 8. b

  blueray JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sita hana lolote ni mnafiki, kwa mafisadi anapataka, kwa wananchi anapataka, mwishowe atararuliwa na mafisadi Na akirudi kwa wananchi hawatampokea
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Wala sishangai!
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Huyo Nnawiye analalama kuhusu rushwa kwani amesahau hulka ya chama chake?
   
 11. l

  lupasulwisye Senior Member

  #11
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM wote lao ni moja kuifilisi nchi hii.Watanzania tumewachoka.Kwaheri zenu
   
 12. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Azipa 16:30 Yesterday
   
 13. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  William Malecela? Ana kigezo gani cha Uongozi wenye sifa? CCM kwishni
   
 14. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,634
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Sielewi baadhi ya watu wanaomtaja Sitta kama mpambanaji wa ufisadi.
   
 15. b

  blueray JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kigezo gani! Ina maana we hujui W. Malecela ni mtoto Wa J. Malecela Snr!
   
 16. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Thanx Mkuu! tunaomjua huyo jamaa ni opportunist. Miaka yote aliyoishi USA ameshindwa kupata hata Bachelor, dada zake ni Dr. Mpeni uongozi huyo jamaa kwa kigezo cha Ubaba
   
 17. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  • FILIKUNJOMBE ADAI YEYE, MKONO, LUGOLA WALIPONZWA NA PINDA,
  • NAPE ATAKA WASIORIDHIKA WAKATE RUFAA,
  • WASOMI WAPONGEZA.

  Waandishi Wetu | 27 September 2012 | Mwananchi

  SIKU moja baada ya Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), kutangaza majina ya wagombea, baadhi ya vigogo walioachwa kwenye uteuzi huo wameeleza ya moyoni, huku Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe akisema anaamini ametoswa kwa sababu alitia saini ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

  Katika Bunge la 10 lililoketi Aprili mwaka huu, baadhi ya Wabunge wa CCM akiwamo Filikunjombe, Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono na Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola, waliunga mkono hoja ya kutokuwa na imani na Pinda iliyokuwa imeanzishwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe wa Chadema.

  Wabunge hao wa chama tawala, waliungana na wenzao wa upinzani kutaka kupiga kura za kutokuwa na imani na Pinda kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ameshindwa kuisimamia Serikali kwa kuwawajibisha mawaziri wazembe.

  Hata hivyo, mpango huo haukufanikiwa baada ya Spika wa Bunge Anne Makinda kueleza kuwa haukufuata taratibu zinazotakiwa.

  Filikunjombe alipotakiwa jana kuzungumzia kuenguliwa kwake kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa ndani ya chama, alisema anaamini yeye na wenzake hao wa CCM, wametoswa kwa sababu ya kushiriki mpango wa kumng'oa Waziri Mkuu Pinda.

  Hata hivyo, alisema amelazimika kukubali hali hiyo na kupokea matokeo, kwa kuwa hatua yake ya kusaini kitabu hicho ilitokana na nia njema kutaka Waziri Mkuu ajiuzulu ili mambo fulani muhimu katika jamii yafanyike.

  Filikunjombe alibainisha kuwa alisaini kitabu hicho cha kutokuwa na imani na Pinda akiwa na akili timamu na alikuwa anajua kinachoweza kutokea kutokana na hatua yake hiyo.

  "Nimesaini kitabu kile kwa nia njema, nikiwa na akili timamu na sijutii uamuzi wangu huo, ila siwezi kuwasemea Kigwangalla (Khamis mbunge wa Nzega) na Bashe (Hussein). Lakini sisi watatu (yeye, Lugola, Mkono) tumeenguliwa kwa sababu hiyo (ya kutokuwa na imani na Pinda)."

  Aliendelea: "Nashangaa leo naonekana adui wa chama wakati nilikuwa nakinusuru na kusema kweli adui wa CCM ni Wabunge wa chama hicho ambao hawakusaini kitabu hicho cha kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, " alisema Filikunjombe.

  Mkono
  Mbunge wa Musomo Vijijini, Nimrod Mkono alisema kutoswa kwake ni uamuzi wa watu aliowaita wenye chama.

  "Walikata jina langu nikakata rufaa, likarudishwa Dodoma, lakini walipokutana wakaona sifai. Wakaamua kunifukuza sasa hapo mimi nifanye nini?" alihoji Mkono.

  Mkono alisema huu ni utaratibu wa chama chao cha CCM ambao umewapa baadhi ya watu haki ya kuwafukuza wengine bila kuwapa fursa ya kujitetea.

  "Kama ilivyotokea kwangu wamekaa na kuona Mkono hafai, fukuza basi wakafanya hivyo na hiyo haijalishi kama nilisaini kutokuwa na imani na Waziri Mkuu au la. Suala la msingi ni kuwa Mkono amefukuzwa na atarudi kama ilivyokuwa kwa mwana mpotevu." alisema bila kufafanua.

  Kigwangalla
  Mbunge wa Nzega, Dk Hamis Kigwangalla alisema anaheshimu uamuzi wa vikao vilivyokaa na kufikia uamuzi uliochukuliwa na kwamba, ataendelea kuwa mwanachama na kukitumikia chama pamoja na wananchi kwa nguvu zote bila kinyongo.

  "Nitaendelea kuheshimu vikao vya chama changu na kuwa mwanachama hai ingawa sijajua wametumia vigezo gani kuteua majina hayo," alisema Dk Kigwangalla.

  Bashe
  Kwa upande wake Bashe alisema kilichotokea ni uamuzi wa chama na vikao halali vilivyokaa na kuchukua uamuazi huo.

  "Sijui kwa nini jina langu halikupitishwa, lakini nitaendela kuwa mwanachama na kuwatumikia wananchi wenzangu wa Nzega," alisema Bashe.

  Katika kuhakikisha hilo, Bashe alisema leo anakwenda Nzega kupeleka mifuko ya saruji tani 18 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za kata za chama hicho wilayani humo.

  Nape ajibu
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alitaka makada waliotoswa na wenye kinyongo wawasilishe malalamiko yao CCM kwa maandishi badala ya kulalamika nje ya utaratibu."Wathibitishe kwa maandishi nasi chama tutajua la kufanya, kwani wabunge hao hawakuingia katika vikao vilivyotoa maamuzi sasa nashangaa kusikia katika vikao tuliwajadili na hoja iliyowaondoa ni hiyo," alisema Nape.
  Maoni ya wasomi

  Wakizungumzia uteuzi huo wasomi na wanasiasa walitoa maoni tofauti huku baadhi wakisema chama kinatakiwa kuwa na sera na mtizamo wa kuliletea maendeleo taifa bila kujali kama chama kinaongozwa na wazee au vijana.

  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema uamuzi huo wa CCM umeonyesha kuwa, ndani ya chama hicho hakuna aliye juu kuliko mwenzake.

  "Wapo waliosema wakitoswa patachimbika, lakini wametoswa na hapajachimbika, uamuzi wa kuwatosa watu wa aina hii utarejesha nidhamu ndani ya chama hicho licha ya kuwa kazi bado ni kubwa," alisema Dk Bana.

  Profesa Gaudence Mpangala alisema vijana kupewa nafasi kubwa ya kugombea nafasi mbalimbali ndani ya CCM, hakuna maana kuwa sera na mtizamo wa chama hicho utabadilika.

  "Kuwa na wanachama au wagombea wenye umri wa wastani(vijana) sio kigezo cha chama kufanya vyema kwa sababu hawawezi kubadili sera na mtizamo wa chama husika," alisema Mpangala.

  Dk Kitila Mkumbo alisema kuingiza vijana wengi katika mpambano huo ni hatua ya ukomavu wa kisiasa kwa kuwa chama hicho awali hakikuwa na utaratibu mzuri wa kuwapa nafasi ya uongozi vijana.

  "Awali Chadema ndio kilionekana chama kinachowapa nafasi zaidi vijana, lakini kwa hatua hii ya CCM ni nzuri, sasa tunasubiri utendaji wao kama utakuwa na manufaa kwa taifa," alisema Mkumbo.

  Bashiru Ally alisema kama kigezo cha kuweka vijana wengi kitazingatia msimamo, fikra na ufanisi katika utendaji kazi wao basi taifa lina kila sababu ya kuunga mkono hatua hiyo.

  Alisema kwa kuwa vijana ndio chachu ya maendeleo kwa mataifa mbalimbali duniani, hatua ya CCM kuwapa nafasi vijana ni nzuri kama wakiifanya kazi hiyo kwa manufaa ya taifa kwanza.

  Habari hii imeandikwa na Ibrahim Yamola, Fidelis Butahe, Elizabeth Edward na Joseph Zablon
   
 18. i

  iseesa JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Siyo huyu aliyeshindwa kumvua GAMBA EL?
   
 19. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Huyo ndiyo JK anafanya mambo hata Mwalimu hakuwahi fanya. CCM ni mali yake, "msiopenda ondokeni" Kama ningekuwa Nkono, Ningeanza mara moja
   
 20. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  SIKU moja baada ya Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), kutangaza majina ya wagombea, baadhi ya vigogo walioachwa kwenye uteuzi huo wameeleza ya moyoni, huku Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe akisema anaamini ametoswa kwa sababu alitia saini ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

  Katika Bunge la 10 lililoketi Aprili mwaka huu, baadhi ya Wabunge wa CCM akiwamo Filikunjombe, Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono na Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola, waliunga mkono hoja ya kutokuwa na imani na Pinda iliyokuwa imeanzishwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe wa CHADEMA.

  Wabunge hao wa chama tawala, waliungana na wenzao wa upinzani kutaka kupiga kura za kutokuwa na imani na Pinda kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ameshindwa kuisimamia Serikali kwa kuwawajibisha mawaziri wazembe.

  Hata hivyo, mpango huo haukufanikiwa baada ya Spika wa Bunge Anne Makinda kueleza kuwa haukufuata taratibu zinazotakiwa.

  Filikunjombe

  Filikunjombe alipotakiwa jana kuzungumzia kuenguliwa kwake kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa ndani ya chama, alisema anaamini yeye na wenzake hao wa CCM, wametoswa kwa sababu ya kushiriki mpango wa kumng'oa Waziri Mkuu Pinda.

  Hata hivyo, alisema amelazimika kukubali hali hiyo na kupokea matokeo, kwa kuwa hatua yake ya kusaini kitabu hicho ilitokana na nia njema kutaka Waziri Mkuu ajiuzulu ili mambo fulani muhimu katika jamii yafanyike. Filikunjombe alibainisha kuwa alisaini kitabu hicho cha kutokuwa na imani na Pinda akiwa na akili timamu na alikuwa anajua kinachoweza kutokea kutokana na hatua yake hiyo.

  "Nimesaini kitabu kile kwa nia njema, nikiwa na akili timamu na sijutii uamuzi wangu huo, ila siwezi kuwasemea Kigwangalla (Khamis mbunge wa Nzega) na Bashe (Hussein). Lakini sisi watatu (yeye, Lugola, Mkono) tumeenguliwa kwa sababu hiyo (ya kutokuwa na imani na Pinda)." Aliendelea: "Nashangaa leo naonekana adui wa chama wakati nilikuwa nakinusuru na kusema kweli adui wa CCM ni Wabunge wa chama hicho ambao hawakusaini kitabu hicho cha kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, " alisema Filikunjombe.

  Mkono

  Mbunge wa Musomo Vijijini, Nimrod Mkono alisema kutoswa kwake ni uamuzi wa watu aliowaita wenye chama.
  "Walikata jina langu nikakata rufaa, likarudishwa Dodoma, lakini walipokutana wakaona sifai. Wakaamua kunifukuza sasa hapo mimi nifanye nini?" alihoji Mkono.

  Mkono alisema huu ni utaratibu wa chama chao cha CCM ambao umewapa baadhi ya watu haki ya kuwafukuza wengine bila kuwapa fursa ya kujitetea, "Kama ilivyotokea kwangu wamekaa na kuona Mkono hafai, fukuza basi wakafanya hivyo na hiyo haijalishi kama nilisaini kutokuwa na imani na Waziri Mkuu au la. Suala la msingi ni kuwa Mkono amefukuzwa na atarudi kama ilivyokuwa kwa mwana mpotevu." alisema bila kufafanua.

  Kigwangalla

  Mbunge wa Nzega, Dkt. Hamis Kigwangalla alisema anaheshimu uamuzi wa vikao vilivyokaa na kufikia uamuzi uliochukuliwa na kwamba, ataendelea kuwa mwanachama na kukitumikia chama pamoja na wananchi kwa nguvu zote bila kinyongo, "Nitaendelea kuheshimu vikao vya chama changu na kuwa mwanachama hai ingawa sijajua wametumia vigezo gani kuteua majina hayo," alisema Dkt. Kigwangalla.

  Bashe

  Kwa upande wake Bashe alisema kilichotokea ni uamuzi wa chama na vikao halali vilivyokaa na kuchukua uamuazi huo, "Sijui kwa nini jina langu halikupitishwa, lakini nitaendela kuwa mwanachama na kuwatumikia wananchi wenzangu wa Nzega," alisema Bashe. Katika kuhakikisha hilo, Bashe alisema leo anakwenda Nzega kupeleka mifuko ya saruji tani 18 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za kata za chama hicho wilayani humo.

  Kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alitaka makada waliotoswa na wenye kinyongo wawasilishe malalamiko yao CCM kwa maandishi badala ya kulalamika nje ya utaratibu."Wathibitishe kwa maandishi nasi chama tutajua la kufanya, kwani wabunge hao hawakuingia katika vikao vilivyotoa maamuzi sasa nashangaa kusikia katika vikao tuliwajadili na hoja iliyowaondoa ni hiyo," alisema Nape.

  Maoni ya wasomi

  Wakizungumzia uteuzi huo wasomi na wanasiasa walitoa maoni tofauti huku baadhi wakisema chama kinatakiwa kuwa na sera na mtizamo wa kuliletea maendeleo taifa bila kujali kama chama kinaongozwa na wazee au vijana.

  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Benson Bana alisema uamuzi huo wa CCM umeonyesha kuwa, ndani ya chama hicho hakuna aliye juu kuliko mwenzake, "Wapo waliosema wakitoswa patachimbika, lakini wametoswa na hapajachimbika, uamuzi wa kuwatosa watu wa aina hii utarejesha nidhamu ndani ya chama hicho licha ya kuwa kazi bado ni kubwa," alisema Dk Bana.

  Profesa Gaudence Mpangala alisema vijana kupewa nafasi kubwa ya kugombea nafasi mbalimbali ndani ya CCM, hakuna maana kuwa sera na mtizamo wa chama hicho utabadilika, "Kuwa na wanachama au wagombea wenye umri wa wastani(vijana) sio kigezo cha chama kufanya vyema kwa sababu hawawezi kubadili sera na mtizamo wa chama husika," alisema Mpangala.

  Dkt. Kitila Mkumbo alisema kuingiza vijana wengi katika mpambano huo ni hatua ya ukomavu wa kisiasa kwa kuwa chama hicho awali hakikuwa na utaratibu mzuri wa kuwapa nafasi ya uongozi vijana, "Awali CHADEMA ndio kilionekana chama kinachowapa nafasi zaidi vijana, lakini kwa hatua hii ya CCM ni nzuri, sasa tunasubiri utendaji wao kama utakuwa na manufaa kwa taifa," alisema Mkumbo.

  Bashiru Ally alisema kama kigezo cha kuweka vijana wengi kitazingatia msimamo, fikra na ufanisi katika utendaji kazi wao basi taifa lina kila sababu ya kuunga mkono hatua hiyo. Alisema kwa kuwa vijana ndio chachu ya maendeleo kwa mataifa mbalimbali duniani, hatua ya CCM kuwapa nafasi vijana ni nzuri kama wakiifanya kazi hiyo kwa manufaa ya taifa kwanza.

  ---
  Habari hii imeandikwa na Ibrahim Yamola, Fidelis Butahe, Elizabeth Edward na Joseph Zablon viagazeti la Mwananchi.

  Source: wavuti.com - wavuti
   
Loading...