Uchaguzi 2010 chanzo cha jamii forums foundation, (jff). | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi 2010 chanzo cha jamii forums foundation, (jff).

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Israel 18, Oct 14, 2010.

 1. I

  Israel 18 Member

  #1
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu ndugu zangu watanzania, natoa shukrani za dhati kwa wote wlioniomba niwatumie kitabu JE TUMWAMBIE RAIS?pia nashukuru kwa maoni yote ya wachangiaji wa mada nilioitoa, ingawa kuna alieniuliza kwa kejeli kama siogopi kufa kwanini nilikimbia?napenda kuwakumbusha ya kwamba kukimbia si kuogopa kwani historia inatufundisha ya kwamba wanamapinduzi wa kweli hukimbia na kujipanga vizuri kisha hurudi, mfano fidel castro alikimbilia argentina na kukutana na akina Che guevara na badae alirudi na kujificha santiago kisha akafanikisha mapinduzi, mahatma gandhi alikimbia afrika kusini, nae vladimiri ilich lenin wa urusi alikimbilia ujerumani na badae wakafanikisha mapinduzi ya wa bolsheviki 1917, hivyo basi nasisitiza ya kwamba mapinduzi yataendelea nikiwa hai au mfu kwani mi sio wa kwanza kukumbwa na mikasa hii.

  Ombi langu leo ni kwamba jamii forums ianzishe foundation ambayo itatuunganisha kwa vitendo ili tuikomboe nchi yetu, nimegundua sisi wana JF tuna upeo wa hali ya juu na pia Mungu katuwezesha ili tuisadie jamii ya Watanzania ambao wengi wao bado wamefunikwa na giza la ujinga, umasikini na maraddhi,
  Uchaguzi huu uwe ni chanzo cha kutuunganisha popote pale tulipo duniani na kisha tuandae katiba yetu naamini kunawataalamu wengi hapa Jf, na baada ya katiba tusajiliwe kisheria kisha tufungue akaunti bank yenye mtaji wa bilion 1 tsh, amabayo itumike kuanzisha miradi mbalimbali kwa mfano shamba la heka 200 likitumika vizuri kwa umwagiliaji tutaweza kuvuna zaidi ya tani 1500 za mchele na mahindi kwa mwaka kisha tutafute masoko nje ya nchi kisha pesa zingine zitumike kuanzisha miradi mingine kama migahawa ya JFF katika miji mikubwa duniani kama vile nassau bahamas, newyork, washington na london, kisha tuuze bidhaa zetu za asili ambazo zitatuwezesha kupata pesa ambazo naamini kabisa utakuwa ndio mwanzo wa kufanya mapinduzi halisi.

  JAMII FORUMS FOUNDATION ITAWEZA FANYA YAFUATAYO.
  1.Kuchapa nakala za mada mbalimbali zinazojadiliwa na kusisambaza katika maktaba mbalimbali nchini pamoja na mashuleni, pia kufadhili uandishi wa vitabu na makala mbali mbali za uzalendo, utawala bora pamoja na haki na wajibu wa wananchi.
  2.kuanda makongamano na midahalo mbalimbali kuanzia shule za sekondari mpaka vyuo vya elimu ya juu.
  3.kufadhili na kuwezesha tafiti mbalimbali ambazo zitafanywa kwa lengo lakuwafikia wana vijiji na kujua matatizo yao pamoja na kuwaelimisha njia sahihi za kutatua matatizo mbalimbali ya kijamii.
  4, jamii forums foundation itaweza kuzalisha wataalamu na wazalendo wa kweli wenye uchungu na maslahi ya taifa lao ambao baadae watapata baraka za JFF na kugombe nyanzifa mbalimbali na kisha tukifikia hatua hiyo hapo tutakuwa tumefanya mapinduzi halisi.

  naomba ifahamike ya kwamba kazi inayofanywa na jamii forums haina tofauti na kazi zilizofanya na akina Socrates, aristato, Plato, pythagoras, thales pamoja na wanafalsafa mbalimbali ambao walikua na upeo wa juu wa kufikiria ambao walikua wakijadili mambo mablimbali yanayo husu maendeleo ya watu na kuyafanya kwa vitendo na matokeo ustarabu ukatufikia hadi kizazi hiki.
  tutumia akili na uwezo aliotupa Mungu kuwafumbua macho watanzania pamoja na kufanya kwa vitendo kama walivyofanya wa nihilist wafuasi wa Lenin ambao walizunguka katia vijiji vyote vya urusi na kuhubiri mapinduzi ambayo yalifanyika na kuuangusha utawala wa akina tsar nicolas.
  Dr Slaa peke yake bila juhudi zetu hatoweza kutukomboa yatupasa kushirikiana na kuungana na kuwa na sauti moja kisha tutafika katika safari yetu ambayo tayari mimi nimeishaanza kukutana na vikwazo vyake ambavyo kwa njia moja au nyingine vinazidi kunikomaza na kunijenga zaidi kimapinduzi.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRIKA.
   
 2. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  mbona umetutoa kwenye mada ya ukombozi na kutuingiza kwenye ujasiriamali, nani kakuambia kuwa hatuna ajira wala vipato? Inaonekana hata kitabu chako kilikuwa childish ndio maana mzee mengi akamtishia nyau jk kuwa hata watoto wanakupinga.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Swali la kwanza ni kuwa kile kitabu kiko wapi?
  Mbona aliingia mitini jana bila kuki'upload hapa ili wataalamu wakisome?
   
 4. I

  Israel 18 Member

  #4
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JATROPHA,
  pole sana kwa mtazamo potofu na watu kama nyie Dr Napoleaon hills amesema mna mtazo potofu au negative thoughts, sijasema hamna pesa ila ninachoongelea sio kuongea sana,kama mnavyofanya lakini hakuna lolote zaidi ya kupinga na kuonyesha mapungufu. Huyo Dr Slaa tunaemtaka na tunae mpigia kura za maoni hapa Jf hatuzidi hata milioni 5 na ikumbukwe kuna watanzania zaidi ya milion 35 hawajui hata kutumia hii teknolojia.
  Tuache unafiki na tuongelee ukombozi wa kweli. pia kuhusu kitabu nimewatumia waliotuma adress zao.
  Sawa waheshimiwa watanzania tunaongoza kwa ujuaji na ndio maana tunazidi kukandamizwa na kuibiwa na kama hatutobadilika kimtazamo na kuacha majungu hatutafika popote.
  na mwisho kabisa nawatakia kila la heri.
   
Loading...