Uchafu uliokithiri jijini arusha

Uchafu uliokithiri jijini arusha

Qsm

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2008
Posts
450
Reaction score
263
Wana JF nawaomba ushauri wenu kuhusiana na jiji la Arusha kuwa chafu kupindukia! hakuna magari ya kubeba uchafu hivyo uchafu umetapakaa kila mahali. kumekuwa na vikao vya wananchi na madiwani wao kuzungumzia suala hilo lakini wale wenye magari wanadai kuwa wananchi hawalipi ada kwa ajili ya huduma hiyo lakini si kweli kwamba wote hawalipi kuna wanaolipa na wasiolipa. Nimekuwa najiuliza utaratibu gani utumike ili kuondokana na kadhia hii. Hali inatisha jamani kila pembe kuna lundo la takataka! Naamini michango yenu itafika kwa wahusika kwani wengi huwa wanachungulia humu.

Wana JF mnaoishi Arusha mtaniunga mkono kwa hili kwani hali halisi mnaijua.
 
geneva ya afrika chafu,kazi kwelikweli
 
Haya magari yapo ila kuna maeneo hayafiki ambapo ndo makazi ya watu wengi!
 
Sio uchafu pekee yake stand ya vdalala hapa france kona ndio balaa wakati mita chache kuna trafik light na mida ya jioni eneo hilo hugeuka soko na kuwa kizuizi kwa waenda kwa miguu pamoja na magari.Manispaa ya arusha kama iko likizo vle haijui cha kufanya
 
soko kuu hapafai achilia mbali kilombero mji hausomeki kabisa hayo masoko yanatakiwa kuwekwa mbali na mjini fikiria soko kuu uchafu upande wa nyuma pale imekuwa kama dampo
 
Muulize mwakilishi wetu mbunge siku akitoka kumsakama zitto dar
 
Arusha ni pachafu kweli. Kuna ulazima wa meya kwa kushirikiana na mkurugenzi wa jiji watembelee Manispaa ya Moshi then waje wakafanye kuiga. Jiji chafu sana hasa sewarge system, mtaani vinyesi kedekede kama vya biashara.

Tulitunze jiji letu.
 
Walio yaondoa yale makontena ya kukusanyia uchafu wayarudishe itapunguza uchafu.Yalikuwepo maeneo mbalimbali kama Mianzin na Sakina darajan.Sasa hiv kuna vijana(wengi wao ni walevi na mateja)wanapita kwenye majumba ya watu wanakusanya uchafu wanapewa pesa,na huo uchafu wanautelekeza njian,hawafikishi panapostahili.
 
Arusha ni pachafu kweli. Kuna ulazima wa meya kwa kushirikiana na mkurugenzi wa jiji watembelee Manispaa ya Moshi then waje wakafanye kuiga. Jiji chafu sana hasa sewarge system, mtaani vinyesi kedekede kama vya biashara.

Tulitunze jiji letu.
Usiwape sababu ya kutafuna pesa za walipa kodi, dawa ya mtu mchavu ni kumlazimisha kuwa msafi siyo kumtembeza akaone show za wasafi.
 
Muulize mwakilishi wetu mbunge siku akitoka kumsakama zitto dar
Mbunge anayezoa taka majumbani? Nafikiri kuna haja ya serikali kurudisha kisoma cha elimu ya watu wazima na kuwalazimisha watu wote kusoma, hasa hasa somo la uraia.
 
nilijua ni uchafu wa ngono. kumbe takataka. hata kwetu zipo

Wewe akili yako fupi unafikiria ngono tu? Je ngono uliambiwa ni uchafu?uwe mstaarabu bwana halafu soma uzi vizuri usikurupuke tu. Kama huna la kuchangia unapotezea.
 
Ukweli mleta uzi ameliona ambalo ni la kweli kabisa. Mji huu hausomeki kabisa kuna vitu vingi sana vya kujiuliza ambapo majibu yake ni utata mtupu. Hebu fikiria madiwani wapo wanaliona, mikakatj ipo na inajadiliwa utekelezaji ziro. Mfano magari ya kuzolea taka yanaonekana lkn mbona uchafu hauishi?? Kingine chaa ajabu watu wanaojitolea kupeleka uchafu kule dampo kwa usafiri wao binafsi wakifika pale ni lazima walipe ushuru tena mkubwa tu. 20000 kwa gari ndogo. Kokoteni 5000 sasa tunajiuliza hayo ya kwao hayatoshi. Wakisaidiwa unalazimika kulipia japo umetumia mafuta yako muda wako bila kujali kitu. Hivi kweli hawa viongozi wana mkakati wa dhati wa kuliweka hii jiji safi kama miji mingine. Tozo mbali kama wrong packing 50000 eti za kuboresha jiji. Packing fees za magari nk zote hizi zinaenda wapi? Wahusika kwa kweli hajawajibika ipasavyo. Watu tunaona barabara zinajeuzwa soko la machinga kila kona sijui viongozi wako wapi. No plan at all.
 
Arusha inanuka sana, kama Dar es Salaam vile.
 
Jifunzeni kutoka jirani zenu wa Moshi. Ni kilomita 80 tu kutoka Arusha.
 
Tuwe na subira. Lema alisema watazibeba na kuzipeleka ofisini kwa mkuu wa mkoa.
 
Back
Top Bottom