Melubo Letema
JF-Expert Member
- Apr 1, 2020
- 374
- 363
BAADA ukimya wa muda mrefu , Timu ya Taifa ya Riadha ipo kambini Sakina , Arusha tayari kuanza kuendela na maandalizi ya mashindano makubwa ya Olimpiki ambazo zitafanyika mwezi Julai 26 hadi Agosti 11 huko Paris Ufaransa.
Tanzania itawakilishwa na wanariadha wanne ambao wanakimbia mbio ndefu kilometa 42 ,Alphonce Simbu,Gabriel Geay,Magdalena Shauri na Jackilne Sakilu.
Simbu alifuzu kupitia Shangai Marathon za China akitumia muda wa 2:05:39,huku Jackline Sakilu nae akifuzu kupitia mbio hizo kwa muda wa 2:26:50,mbio zilifanyika Novemba 26,2023.
Magdalena yeye alipenya kupitia Berlin Marathon zilizofanyika Septemba 24,2023 nchini Ujerumani akitumia 2:18:41 huku Geay akitokea Valencia Marathon ambazo zilitimua vumbi Disemba 2,2023 Hispania kwa 2:04:33.
Wanariadha Andrew Rhobi anaekimbia mita 1500,John Wele mita 5000,Failuna Abdi Matanga,,Josephat Gisemo,Faraja Lazaro na Aloyce Simbu wanaokimbia mbio ndefu wao walishindwa kufuzu.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT),Jackson Ndaweka alisema kambi hiyo imeanza toka jumatatu iliyopita na itakuwa Sakina, Arusha chini ya makocha wawili.
Makocha hao ni Michael Washa wa jeshi la Magereza na Antony Mwingereza kutoka jeshi la wananchi (Jwtz),ambaye wanariadha wake watatu wamefuzu kushiriki Olimpiki,Simbu,Jackline na Magdalena.
"Wachezaji wetu wote wapo kwenye hali nzuri ya kimashindano kwani wana viwango bora na wana uwezo wa kucheza chini ya muda ambayo itawafanya kurudi na medali”,alisema Ndaweka.
Aliongeza licha ya kwamba Olimpiki za mwaka huu zitakuwa na ushindani mkubwa sana kwani wanariadha wengi wenye ubora kwa sasa watashiriki.
Lakini pia kutolewa zawadi za fedha kwa mara ya kwanza kwa washindi ambao watapata medali kwa upande wa Riadha ila wana matumaini makubwa na viijana wao katika kwenda kupambania medali zingine baada ya kupita miaka 44.
“Tunafanya kila kitu ili kambi iwe bora kuanzia kwenye morali na motisha pia kamati ya Olimpiki Tanzania itakuja kutuongezea nguvu”,alisema.
Tangu Tanzania ilipopata medali mbili za shaba katika mashindano hayo kwenye mbio za mita 5000 na 3000.Olimpiki za Moscow Urusi mwaka 1980.
Moja ilitwaliwa na mwanariadha Suleiman Nyambui aliyeshika nafasi ya pili katika mbio za Mita 5000 na nyingine ikichukuliwa na Filbert Bayi katika mbio za Mita 3000.