UCHAFU: Jiji la Dar es Salaam lipo katika Hatari Kubwa siku chache zijazo

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Messages
489
Points
1,000

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Joined Sep 11, 2017
489 1,000
Katika hali hii ya mvua wakazi wa Jiji la Dar wajiandae kwa magonjwa mengi ya milipuko yanayotokana na uchafu utakaokithiri katika Jiji hili.

Mh Rais,Waziri wa Afya, Mazingira, Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya. Angalieni jambo hili kwa macho makali makavu kuokoa Taifa na Janga linalokuja.

Ni wazi kuwa JIJI/Manispaa ya Ilala imeshindwa kuliendesha Dampo lake lililopo Pugu Kinyamwezi. Wakandarasi wengi wa usafi wameonesha kukata tamaa kutokana na miundo mbinu mibovu kuliko hata ya kwendea Jehanamu iliyopo katika dampo hilo.

Wanasema ni rahisi kwenda jehanamu na kuwa na uhakika wa kurudi salama kuliko kupeleka gari kwenda mwaga taka katika Dampo la Pugu Kinyamwezi.

Gari zimekuwa zikilala huko mpaka siku mbili na wakati mwingine kuharibikia huko huko kutokana na gari hizo maarufu kwa jina la Compactor au Tipper kusukumwa au kuvutwa na Bulldozer. Magari mengi yamekuwa yakivunjiwa windscreen au kingo za nyuma kwenye PTO,taa na Bumpers kwa sababu ya matumizi ya Bulldozers kuya push kwenda kumwaga na kutoka kumwaga.

Barabara zimekuwa ni za taka kiasi kwamba huwezi pita hata getini kuingia ndani kama hujatumia gari au kuvaa gum boots/rain boots.

Ukifika eneo hilo utakuta madereva wengi na wasaidizi wao wakiwa na sura za huzuni na majonzi kutokana na kulazimika kulala eneo hilo wakiwa kwenye foleni ya kwenda mwaga taka.

Pia maisha ya wananchi wanaoishi karibu na eneo hilo yapo hatarini sana kutokana na uchafu na hewa kali,chafu yenye ukakasi mwingi wanayovuta.jambo hili limesababisha wengi wap kuwa na sura za uzee ingawa umri wao bado unadai.

Magonjwa yanayotokana na uchafuzi wa hali ya hewa na mazingira ni wazi kuwa hayachezi mbali na eneo hilo kutokana na uchafu uliokithiri.

Kuharibika kwa magari na kutomwaga kwa wakati kunapelekea jiji kuwa chafu kutokana na utendaji wa kazi kukwama kwa sababu ya kukosekana vitendea kazi.

Maeneo mengi jijini yanaonekana taka zikiwa zina zagaa zagaa tu na unapouliza wakandarasi wanaonesha hali ya dampo ilivyo na magari yao yakiwa katika foleni.au yamepark dampo yakiwa yanahitaji matengenezo.

Mheshimiwa Rais waulize hawa watu

Mawaziri husika, Mkuu wa Mkoa na Wilaya,Mkurugenzi wa Manispaa. Je hali hii wameridhika na mambo haya?


IMG-20200214-WA0019.jpg
IMG-20200214-WA0018.jpg

IMG-20200214-WA0021.jpg


 

Kitaturu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Messages
5,260
Points
2,000

Kitaturu

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2013
5,260 2,000
Moja ya kipimo cha maendeleo ya sehemu mfano familia ama nchi ni kuangalia hall yao ya usafi!!

Ukiona mji ama nchi inashindwa hata kuzibua mitaro ya uchafu, ujue watu was eneo hilo wakiwemo viongozi wao bado ni wajinga was kutupwa, hawana maendeleo yoyote hata kama wanavaa suti za kutoka Italy na kuwa na elimu ya kiwango cha PhD za Chemistry na korosho!!
 

Forum statistics

Threads 1,389,316
Members 527,908
Posts 34,022,741
Top