Ubungo: Wanajeshi wampa kisago traffic police...!

safi sana hawa ma trafiki wananiudhigi sana hata mimi wawapo barabarani...kuna wengine wanajua kazi zao na kuna wengine wakiwa wanaongoza magari hata mie ninakuaga na hamu ya kushuka na kuwazaba vibao

Kwa nini tulaumu trafiki badala ya kuangalia miundo mbinu ambayo itaondoa misongamano isiyokuwa na lazima! tafakari
 
Wana JF
Ni hivi juzi tu tumeshuhudia wanajeshi wakimpiga trafiki eti kawachelewesha kwenye foleni!
Sasa mimi ninajiuliza maswali kadhaa ambayo naamini hata wengine inawezekana wakawa wanajiuliza kama mimi

1. Je ni kweli trafiki aliwachelewesha wao wanajeshi tu au kulikuwa na watu wengine wa kawaida?

2. Je bara bara hiyo ilipaswa kutumiwa na wanajeshi peke yao? kwa maana ya kwamba vyombo vingine vya moto na
visivyo vya moto havistahili kutumia bara bara hiyo?

3.Au trafiki yule alishindwa kazi ya kuongoza magari na hivyo wao walitaka ku take charge kwenye kazi ile ya kuongoza
magari?

4. Kwa kitendo kile cha kumpiga trafiki je wananchi wa kawaida waamini kuwa trafiki anastahili kupigwa pale ambapo wanahisi wamecheleweshwa?
5.Je itakuwaje ikiwa watumiaji wa bara bara wakawa na tabia ya kuwapiga trafiki?
Tujadili kwa busara na sio kwa hisia binafsi
Nawasilisha

Kwanini Hausomi HOJA zilizopo hapa kwanza? HAO WANAJESHI walikuwa ni FAKE; Walikuwa kwenye TRIP ya kuenda kuiba SILAHA...

SOMA THREADS zingine zina Majibu..
 
Matraffick huwa wanaboaaaa, bora walivyopewa kichapo! Mfyuuuuu! Wanaongoza kwa rushwa ol over, wa mikoani ndio usiseme, ni nUksi, watandikwe na bado!

Afu weweee.....

Nikikukamataaaaaa.....!
 
Kwa Tanzania wao ni mabosi wa mapolisi...hata kwenye ghasia juzi..walifika maeneo ya tukio..wakala shushi tu, wakati wenzao wanakimbizana na mashehe ubwabwa.

Kasome katiba inakueleza tafsiri sahihi ya wanajeshi na sio kama unavyodhani
 
Unajua hii dunia wakati mwingine tamu sana, hawa polisi huwaonea sana raia kwa kuwapiga, kuwachukulia centi zao za ugali na hata kuwaua sasa kiboko yao nao ni wanajeshi, waache wawatie mkongóto wamezidi. Hebu tuambie huyo polisi akikukosea utampeleka wapi?wanalindana siku zote.
 
huwa nashangaa kama taa zinawaka na zinaongoza magari trafiki wa nini?
huwa wanaudhi sana mnaweza kukaa hata nusu saa nzima
trafiki awepo kama hakuna umeme.sishabikii tarfiki kupigwa ila wapo wanaoudhi kwa kweli
tena ukimpigia honi ndio kabisa mtakesha hata kama una mgonjwa atafia hapo mataa.
 
safi sana hawa ma trafiki wananiudhigi sana hata mimi wawapo barabarani...kuna wengine wanajua kazi zao na kuna wengine wakiwa wanaongoza magari hata mie ninakuaga na hamu ya kushuka na kuwazaba vibao

Mwenzenu Nina ushuuda tofauti jamani.

Pale makutano ya Kawawa na Bagamoyo pana Katrafiki fulani ka kike yaani kananivutia sijapata kuona.
Kakamavu, shepu bomba, magari kanaruusu fastafasta, yaani basi tu. Yule naomba asiguswe!!!
Wale wa Ubungo goi goi sana. Njaa zikiwauma jioni wanaanza njiapanda chuo kikuu au Ubungo tanesco kucheki vioo eti wanakagua road license kumbe ukaguzi wa pochi. Magari yanasimama muda mrefu sana makundi yakiwa yako bize kufanya uo ukaguzi. Haraka za watokao buguruni, mwenge, au chuo kikuu mwisho pale. Inakera sana. Kuna siku nilikuwa nataka kujaza mafuta pale sheli ya ubungo mbona mafuta yameniishia gari tatu kabla ya trafiki ikawa so kweli. Kisa, kasimamisha magari karibia nusu saa. Kuna siku nimetamani nimzabe yule trafiki pale basi tu sikuwa na jiwe begani angenitambua! Kuna wakati utakuta hata sababu ya kuzuia magari kwa Muda mrefu hivo upande mmoja haionekani--hasa upande wa mandela na Mwenge. WE ukitaka kujua inakuwaje sikilizia honi za watu pale wanapozidiwa .

Kuzabwa vibao mbona nasikia kawaida tu jeshini unapochelewa kutekeleza oda, au?. Askari polisi si nao ni askari tu?!
where is the problem. Kama alikuwa hasikii oda utafanyaje...Zaba vibao afunguke!
Mzabaji alikuwa na mawe mangapi...
 
Trafiki polisi yeyote nchini hapa anastahili kipigo maana mambo wanayotufanyia wananchi,rushwa wanayochukua toka kwetu na makosa wanayotubambika sisi waendesha bodaboda tukiwa barabarani ni uonevu mtupu! Yaani total harassment
 
Haikuwa sahihi kwa hao askari wa JWTZ kumpiga huyo askari wa trafiki. Hii ni tabia mbaya sana ambayo inaweza kuleta maafa makubwa isipothibitiwa mapema. Trafiki anapokuwa barabarani anaongoza magari pia anapata mawasiliano kwa radio call kutoka maeneo mengine kuhusu hali ya barabara. Na hapo ndipo anajipanga kikazi zaidi kujua wapi anaruhusu magari kwa muda gani, nk nk Yawezekana akapata taarifa ya msafara wa viongozi au chochote. Sasa yeye sio wa kulaumiwa eti amechelesha magari.

Siombei, lakini inawezekana siku moja wakawapiga hao polisi na wao wakajibu mapigo. Hawa wote wanabeba silaha za moto - itakuwaje?

Mwanajamii mmoja anasema alichelewesha ili apate rushwa kutoka kwa madereva... nadhani hii sio sahihi kwani hivi kweli madereva wana muda wa kujiorganize na kuchangisha hiyo pesa wakiwa ktk jam??? Trafiki wanatuhumiwa kwa kupokea rushwa sana... na ni kweli kbs, lkn sio ktk mazingira hayo!

Mara kadhaa tumesikia askari wa JWTZ wamepiga raia hovyo bila sababu ya msingi. Kuna wakati utasikia eti wamepiga watu eneo kama stendi kisa eti mwnzao kaibiwa simu- very stupid. Inawezekana yameathirika kisaikollojia kutokana na kufungiwa kambini muda mrefu.

Huo ni upumbavu na ulimbukeni wa kufikiri kwa kutumia makalio kwamba wao juu ya sheria. Viongozi wa majeshi yote na wananchi wote tunapaswa kukemea huu ujinga wa hao majambazi kwa nguvu zote.
 
Kwa nini tulaumu trafiki badala ya kuangalia miundo mbinu ambayo itaondoa misongamano isiyokuwa na lazima! tafakari

hapo umeongea cha maana maana taa nyingi za barabarani ni mbovu na nyingine unakuta ziko mahali ambako umeme hua haupogi maana sasa hivi tumefikia mahali ambako hata kama taa za barabarani zinafanya kazi tunakua hatuziamini kwa sababu watu siku hizi hasa bodaboda hawajali mataa ziwe nyekundu au kijani wao wanapita tu ndio maana wengi wao huishi muhimbili...hii nchi sasa hivi kila mtu anafanya la kwake..hakuna utawala wala sheria...ndio maana na ajali barabarani zinazidi
 
trafiki polisi yeyote nchini hapa anastahili kipigo maana mambo wanayotufanyia wananchi,rushwa wanayochukua toka kwetu na makosa wanayotubambika sisi waendesha bodaboda tukiwa barabarani ni uonevu mtupu! Yaani total harassment

huo ni upumbavu wenu nyie mnaoendesha bodaboda. Wengi wenu hamjui sheria za barabarani, mnabeba abiria zaidi "mshkaki" ,hamna leseni ndio maana mmekuwa chanzo kikuu cha ajali nchini.
 
Mara kadhaa tumesikia askari wa JWTZ wamepiga raia hovyo bila sababu ya msingi. Kuna wakati utasikia eti wamepiga watu eneo kama stendi kisa eti mwnzao kaibiwa simu- very stupid. Inawezekana yameathirika kisaikollojia kutokana na kufungiwa kambini muda mrefu.

Who let the dogs out....woof!woof, woof
 
Wana JF
Ni hivi juzi tu tumeshuhudia wanajeshi wakimpiga trafiki eti kawachelewesha kwenye foleni!
Sasa mimi ninajiuliza maswali kadhaa ambayo naamini hata wengine inawezekana wakawa wanajiuliza kama mimi

1. Je ni kweli trafiki aliwachelewesha wao wanajeshi tu au kulikuwa na watu wengine wa kawaida?

2. Je bara bara hiyo ilipaswa kutumiwa na wanajeshi peke yao? kwa maana ya kwamba vyombo vingine vya moto na
visivyo vya moto havistahili kutumia bara bara hiyo?

3.Au trafiki yule alishindwa kazi ya kuongoza magari na hivyo wao walitaka ku take charge kwenye kazi ile ya kuongoza
magari?

4. Kwa kitendo kile cha kumpiga trafiki je wananchi wa kawaida waamini kuwa trafiki anastahili kupigwa pale ambapo wanahisi wamecheleweshwa?
5.Je itakuwaje ikiwa watumiaji wa bara bara wakawa na tabia ya kuwapiga trafiki?
Tujadili kwa busara na sio kwa hisia binafsi
Nawasilisha

Asilimia 60% ya matrafiki ni wajinga na hawajui sheria mimi mwenyewe nilishamtandika trafic mmoja na kesi ilikuwa mahakama ya wilaya na ikafutwa January 14 mwaka huu baada ya kunilazimisha nivae helmet wakati naingia mgahawani kwa hilo nawapa bravo wanajeshi
 
Haikuwa sahihi kwa hao askari wa JWTZ kumpiga huyo askari wa trafiki. Hii ni tabia mbaya sana ambayo inaweza kuleta maafa makubwa isipothibitiwa mapema. Trafiki anapokuwa barabarani anaongoza magari pia anapata mawasiliano kwa radio call kutoka maeneo mengine kuhusu hali ya barabara. Na hapo ndipo anajipanga kikazi zaidi kujua wapi anaruhusu magari kwa muda gani, nk nk Yawezekana akapata taarifa ya msafara wa viongozi au chochote. Sasa yeye sio wa kulaumiwa eti amechelesha magari.

Siombei, lakini inawezekana siku moja wakawapiga hao polisi na wao wakajibu mapigo. Hawa wote wanabeba silaha za moto - itakuwaje?

Mwanajamii mmoja anasema alichelewesha ili apate rushwa kutoka kwa madereva... nadhani hii sio sahihi kwani hivi kweli madereva wana muda wa kujiorganize na kuchangisha hiyo pesa wakiwa ktk jam??? Trafiki wanatuhumiwa kwa kupokea rushwa sana... na ni kweli kbs, lkn sio ktk mazingira hayo!

Mara kadhaa tumesikia askari wa JWTZ wamepiga raia hovyo bila sababu ya msingi. Kuna wakati utasikia eti wamepiga watu eneo kama stendi kisa eti mwnzao kaibiwa simu- very stupid. Inawezekana yameathirika kisaikollojia kutokana na kufungiwa kambini muda mrefu.

Huo ni upumbavu na ulimbukeni wa kufikiri kwa kutumia makalio kwamba wao juu ya sheria. Viongozi wa majeshi yote na wananchi wote tunapaswa kukemea huu ujinga wa hao majambazi kwa nguvu zote.

Kwa uelewa wako mdogo mpaka tunakwenda kaburini polisi wote duniani hawataweza kushindana na WANAJESHI
 
Back
Top Bottom