Habari za uhakika>
Wakuu ni kweli moto ulitokea katika engine hiyo kama ilivyoelezwa hapo awali na ulidhibitiwa na wafanyakazi wa zamu. Suala hili si dogo kama linavyofikirika kwani hadi sasa mtambo huo wenye uwezo wa kuzalisha 40MW umezimwa na wahandisi wa kampuni hiyo wanaendelea kufanya uchunguzi wa kina kujua chanzo ili kuweza kutatua tatizo hilo. Yote yanawezekana, huenda ikachukua muda mfupi au mrefu kwa mtambo huu kurudi kwenye operations lakini kwa sasa umezimwa. Hii itazidisha athari za mgawo wa umeme. Nitaendelea kuwajuza.