Ubungo Songas engine no. 3 inawaka moto

mkumbamasaka

Member
Nov 1, 2010
15
7
Jamani habari nilizozipata ni kuwa injini namba 3 pale SONGAS imepata hitilafu na inawaka tafadhali mtujuze mlio karibu.

===========================

UPDATES: (Maxence)

Ni kweli moto ulitokea mwendo wa saa 9 kasoro lakini ulidhibitiwa kabla hali haijawa mbaya. No serious damages
Kwa mujibu wa Msemaji wa TANESCO
 
Jamani utani na ukweli uwe mbali tujadili vitu na kupashana mambo kwa njia iliyo chanya, inasemekana mpaka sasa wameudhibiti kwa kiasi fulani usilete madhara makubwa kwani umeme ungekatika kwa muda mrefu kama ilivyokuwa 2004 yalipoungua matenki ya mafuta jet A1 hapo hapo yaliyokuwa yakihifadhiwa kwa kazi ya uendfeshaji kabla ya Gesi
 
Nchi ni yetu sote wewe na mimi lazima tuwe na uchungu nayo, na haki ya kupata habari ni muhimu ili tujue na tuwe na mahali pa kuanzia
 
Ndugu zangu mi ndo na alee, naenda jipumzisha, nasubiri taarifa za habari jioni, tuko pamoja but "me and you we are all responsible in safeguarding the countries interests"
 
Duh!! Jamani tusiombe liwake, maana makali ya mgao yako critical, sitaki kukumbuka mgao wa 2004!!!
 
hii habari sidhani kama ni kweli, ingekua kweli basi muda wote huu tungeshapata confirmation... na kama ni kweli basi mkumbamasaka unatakiwa utupe habari kamili
 
Ninaanza kuogopa! Inaonekana wapo baadhi yetu tunaopenda kuchafua JF kama kianzia cha uhakika cha habari. Mtu anazusha tu na wengine wanapanga hoja juu ya hoja. Ukweli wa hii taarifa ya Engine No. 3 kuwaka moto pale Ubungo ni wa mashaka sana.
 
Updated first post:

Ni kweli moto ulitokea mwendo wa saa 9 kasoro lakini ulidhibitiwa kabla hali haijawa mbaya. No serious damages
Hii ni kwa mujibu wa Msemaji wa TANESCO
 
Jamani hii nchi inaenda wapi sasa. Hizi ni Vita za Amani na Utulivu. Tuwe kama Tunisia au Libya tujue moja...
 
Haya laana za kuiba ushindi wa watu inaturudia kila kitu hakiendi kama tunavyotaka. Ahadi za kampeni zaidi ya 100 matatizo lukuki sijui tunaelekea wapi, na mkwere ndo huyo Mauritania!!!!!!!!!!!!. Nadhani mgao utaongezeka zaidi!
Pole yetu Watanzania
 
Back
Top Bottom