Ubungo Riverside na biashara ya ukahaba mpaka lini?

Ubungo Riverside na biashara ya ukahaba mpaka lini?

Wakuu,

Inasiikitisha kuona eneo la Ubungo riverside kukizidi kukua na kushamiri biashara ya ukahaba tena mapema yaani kuanzia mida ya kumi na moja jioni. Mbaya zaidi watoto wadogo Na wanafunzi ndo unakuta wanapita hapo kutoka mashuleni ambapo kukutana na hawa dada zao Na wengine wakiwa ni sawa na mama zao wamejipanga barabarani wakisubiri wateja wakiwa Na mavazi ya nusu uchi.




Pembezoni mwa Baa ya Zambezi iliyopo River Side, Ubungo wasichana hujipanga kuanzia karibu na kituo cha mafuta na kuzunguka baa hiyo kuanzia majira ya saa 11 jioni. Wasichana hao wana vyumba vyao katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo jirani na baa hiyo.

Wasichana hao wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 16 hadi 25 wamegeuza eneo hilo kuwa kijiwe chao maarufu, jambo ambalo huwashtua wageni wanaotembelea maeneo hayo kwa mara ya kwanza.

Ni wakati sasa serekali kuchukua hatua kwani watoto wanajifunza maadili yasiyofaa kutoka kwa makahaba hao kuanzia wanavyovaa, wanavyozungumza na wanavyotembea.

Acheni bwana sie madomo zege sasa mtataka tubake wanafunzi. Waacheni hao dada poa, wanatusaidia sie madomo zege tusibake.
 
Hii biashara ialalishwe tu na waanze kulipa Kodi km baadhi ya majiji ulaya huku wakitafutiwa sehemu maalum ili isilete bughudha Kwa watu wengine

Haiwezi kufutika maana imekuwepo tangu enzi na enzi

Serikali inahangaika na tozo Kwa wananchi wakati kuna maeneo km haya hagajaangaliwa km fursa
Hizi sasa ndio akili za magreat thinkers
 
Bodaboda wanateketea hapo,maana anambeba akimaliza ukahaba hapo,then nayeye anaomba wakati anajua ametoka kujiuza......ukisikiliza story za eneo hilo kuanzia Mabibo hostel stand kuja Mikasa, Zambezi,Chonya Inn bar, Kinyaiya pale au vuka Riverside bar........eneo la pale unaingia Mchichani (zamani stand ya kwenda Makoka) Kuna kibaa katikati hapo ndiyo Kinyambi (yule comedian aliyefariki) alipopatia ngoma,pale kuna wadada wengii,bar,guest na michemsho ila ngoma nje nje.
 
Hao Malaya nyuma yao kuna mawakili wakikamatwa wanapewa masaada wa kisheria,

Kwanza hapo wamesimama kama raia wengine ukimkamata unapaswa uthibitishe kama hapo alikuwa anafanya umalaya,

Waachane nao tu wafanye shughuli nyingine
 
Watu wamesimama barabaran unasema wanajiuza 😀😀😀😀
Hujamuhoji hata mmoja kuuliza kwann wapo hapo zaidi ya yote naona unaingilia faragha za watu maana camera unaelekeza kwa kila mtu hata ambaye hausiki
 
Back
Top Bottom