Ubungo Riverside na biashara ya ukahaba mpaka lini?

kazuramimba

Senior Member
Jun 14, 2011
126
57
Wakuu,

Inasiikitisha kuona eneo la Ubungo River Side kukizidi kukua na kushamiri biashara ya ukahaba tena mapema yaani kuanzia mida ya kumi na moja jioni. Mbaya zaidi watoto wadogo Na wanafunzi ndo unakuta wanapita hapo kutoka mashuleni ambapo kukutana na hawa dada zao na wengine wakiwa ni sawa na mama zao wamejipanga barabarani wakisubiri wateja wakiwa na mavazi ya nusu uchi.Pembezoni mwa Baa ya Zambezi iliyopo River Side, Ubungo wasichana hujipanga kuanzia karibu na kituo cha mafuta na kuzunguka baa hiyo kuanzia majira ya saa 11 jioni. Wasichana hao wana vyumba vyao katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo jirani na baa hiyo.

Wasichana hao wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 16 hadi 25 wamegeuza eneo hilo kuwa kijiwe chao maarufu, jambo ambalo huwashtua wageni wanaotembelea maeneo hayo kwa mara ya kwanza.

Ni wakati sasa serekali kuchukua hatua kwani watoto wanajifunza maadili yasiyofaa kutoka kwa makahaba hao kuanzia wanavyovaa, wanavyozungumza na wanavyotembea.
 
Wakuu,

Inasiikitisha kuona eneo la Ubungo riverside kukizidi kukua na kushamiri biashara ya ukahaba tena mapema yaani kuanzia mida ya kumi na moja jioni. Mbaya zaidi watoto wadogo Na wanafunzi ndo unakuta wanapita hapo kutoka mashuleni ambapo kukutana na hawa dada zao Na wengine wakiwa ni sawa na mama zao wamejipanga barabarani wakisubiri wateja wakiwa Na mavazi ya nusu uchi.
Pembezoni mwa Baa ya Zambezi iliyopo River Side, Ubungo wasichana hujipanga kuanzia karibu na kituo cha mafuta na kuzunguka baa hiyo kuanzia majira ya saa 11 jioni. Wasichana hao wana vyumba vyao katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo jirani na baa hiyo.

Wasichana hao wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 16 hadi 25 wamegeuza eneo hilo kuwa kijiwe chao maarufu, jambo ambalo huwashtua wageni wanaotembelea maeneo hayo kwa mara ya kwanza.

Ni wakati sasa serekali kuchukua hatua kwani watoto wanajifunza maadili yasiyofaa kutoka kwa makahaba hao kuanzia wanavyovaa, wanavyozungumza na wanavyotembea.

Mkuu wewe daily unaangazia Malaya tatuta content za msingi views utapata tu
 
Mkuu wewe daily unaangazia Malaya tatuta content za msingi views utapata tu

Mkuu mimi sitafuti views na wala siishi kwa views! Nina onyesha changamoto tulizo nazo kwenye jamii na namna gani tunaweza tafuta jawabu la pamoja ili kuokoa kizazi kijacho.

Kumbuka kesho Na kesho kutwa mtoto wako au ndugu Yako anaweza dumbukia kwenye hii changamoto hivyo zungumza kama mtu mwenye akili sio kukumaji anayefikiria Kwa kutumia kamasi
 
Hii biashara ialalishwe tu na waanze kulipa Kodi km baadhi ya majiji ulaya huku wakitafutiwa sehemu maalum ili isilete bughudha Kwa watu wengine

Haiwezi kufutika maana imekuwepo tangu enzi na enzi

Serikali inahangaika na tozo Kwa wananchi wakati kuna maeneo km haya hagajaangaliwa km fursa

Khaaaaa!!!
 
Mkuu nahiitaji ni-kicomment maandishi yangu yawe na wino mweusi Kama kwako nafanyaje? Mkuu
unatumia browser au app?

fuata hii link

Mkuu mimi sitafuti views na wala siishi kwa views! Nina onyesha changamoto tulizo nazo kwenye jamii na namna gani tunaweza tafuta jawabu la pamoja ili kuokoa kizazi kijacho. Kumbuka kesho Na kesho kutwa mtoto wako au ndugu Yako anaweza dumbukia kwenye hii changamoto hivyo zungumza kama mtu mwenye akili sio kukumaji anayefikiria Kwa kutumia kamasi
Moja ya biashara kongwe
Hii haiondoki leo wala kesho
Hawa walianzaga kujiuza ohio
St mjini,Tunisia Road kinondoni
Sahv wamepanua wigo lao

Ova
 
Hii biashara ialalishwe tu na waanze kulipa Kodi km baadhi ya majiji ulaya huku wakitafutiwa sehemu maalum ili isilete bughudha Kwa watu wengine

Haiwezi kufutika maana imekuwepo tangu enzi na enzi

Serikali inahangaika na tozo Kwa wananchi wakati kuna maeneo km haya hagajaangaliwa km fursa
Naunga mkono wazo lako

Ova
 
Wakiamishwa hapo wataenda sehem nyengine. Ila means ya kupunguza wanaojiuza ipo
 
Mkuu mimi sitafuti views na wala siishi kwa views! Nina onyesha changamoto tulizo nazo kwenye jamii na namna gani tunaweza tafuta jawabu la pamoja ili kuokoa kizazi kijacho. Kumbuka kesho Na kesho kutwa mtoto wako au ndugu Yako anaweza dumbukia kwenye hii changamoto hivyo zungumza kama mtu mwenye akili sio kukumaji anayefikiria Kwa kutumia kamasi
Mkuu unatoka uokoe kizazi gani,Kama Yesu mwana was Mungu aliikuta akaiacha kama ilivyo wewe unahitaji nini zaidi?
 
Back
Top Bottom