Ubungo, Dar: Ubomoaji jengo la TANESCO waanza

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,561
21,556
UBUNGO, DAR: Jengo la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeanza kubomolewa muda huu kutokana na sehemu ya jengo hilo kuwa ndani ya hifadhi ya barabara.

=========

PIC+TANESCO.jpg


Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) umesema umeanza utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kubomoa jengo lake lililo ndani ya hifadhi ya barabara eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam.

Kazi hiyo iliyoanza leo Jumatatu Novemba 27,2017 ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli aliyeagiza majengo ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji na ghorofa la Tanesco kuwekwa alama ya X kwa ajili ya kubomolewa.

Novemba 15,2017 akitokea Chato alipokwenda kwa mapumziko baada ya ziara ya Uganda, Rais Magufuli aliagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuweka alama ya X katika majengo hayo sehemu zilizo katika hifadhi ya barabara.

Taarifa ya TANESCO kwa umma imesema kuanzia leo Jumatatu Novemba 27,2017 wameanza kubomoa ukuta wa mbele ya jengo.

TANESCO imesema baadhi ya watumishi wa shirika hilo wameanza kuhamishiwa katika ofisi nyingine za shirika zilizopo jijini Dar es Salaam ili kupisha shughuli za ubomoaji kufanyika kwa usalama.

Uongozi wa shirika hilo na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) unaendelea kufanya utaratibu utakaowezesha ubomoaji wa jengo hilo la ghorofa kufanyika bila kuathiri huduma kwa wateja wa TANESCO.

“Katika kipindi hiki cha utekelezaji wa agizo la Rais. Tunapenda kuwahakikishia wateja na Watanzania kwa jumla kuwa, huduma za umeme zitaendelea kupatikana kama kawaida ikiwemo huduma ya ununuzi wa Luku,” imesema taarifa hiyo.

Uongozi wa shirika hilo umesema utaendelea kutoa taarifa kwa kadri kazi hiyo itakavyokuwa ikiendelea.


Chanzo: Mwananchi
 
UBUNGO, DAR: Jengo la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeanza kubomolewa muda huu kutokana na sehemu ya jengo hilo kuwa ndani ya hifadhi ya barabara

Tupia ka picha kidogo walau na sisi tunaoishi huku Nanjirinji tuweze kuona
 
Hapo halibomolewi jengo literally inateketezwa fedha ya walala hoi walipa kodi
Unajua utofauti ya bomoa bomoa tuliyoizoea kwa wananchi na hiyo? alie plan mwenyewe na sasa anabomoa mwenyewe"
Kama hospital utampeleka wodi gani akafanye vipimo gani mtu kama huyo?
 
aiseee.Okay.Kwa hio ndio maana lilijengwa kwenye road reserve?

libomolewe tu.Lowasa Fisadi sana.Nilikuwa najiuliza ..how come serikali ijenge kwenye road reserve..kumbe ni mwizi Lowasa

wabomoe haraka sana[/QUOTE]

Kwa hiyo Jengo la Idara ya Maji sio La Serikali?

Lowassa naye anahuka?
 
Back
Top Bottom