Ubungo, Dar: Ubomoaji jengo la TANESCO waanza

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
TAARIFA KWA UMMA

Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) unawafahamisha Wateja wake wote na Wananchi kwa ujumla kuwa;

TANESCO imeanza utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli, kuhusu kubomolewa kwa Jengo la Ofisi za TANESCO Makao Makuu, liliopo Ubungo Jijini Dar es salam.

Kuanzia Jumatatu Novemba 27, 2017. Ukuta wa mbele ya jengo umesha vunjwa , pia baadhi ya Watumishi wa Shirika wameanza kuhamishiwa katika Ofisi nyingine za TANESCO zilizopo jijini Dar es salaam ili kupisha shughuli za ubomoaji kufanyika kwa usalama zaidi.

Uongozi wa Shirika pamoja na Wakala wa Majengo (TBA) wanaendelea kufanya taratibu zitakazo wezesha zoezi la ubomoaji wa Jengo kufanyika bila kuathiri huduma kwa Wateja wa Shirika.

Katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais. Tunapenda kuwahakikishia Wateja wetu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa Huduma za Umeme zitaendelea kupatikana kama kawaida ikiwemo huduma ya manunuzi ya LUKU.

Uongozi wa Shirika utaendelea kutoa taarifa kwa kadri zoezi hili linavyo endelea,

TANESCO ‘‘Tunayaangaza Maisha yako’’

Kwa mawasiliano

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii

www.facebook/tanescoyetu

www.twitter.com/tanescoyetu

Imetolewa Na: OFISI YA UHUSIANO
TANESCO- MAKAO MAKUU.

Novemba 27, 2017

UBUNGO, DAR: Jengo la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeanza kubomolewa muda huu kutokana na sehemu ya jengo hilo kuwa ndani ya hifadhi ya barabara
 
478477c0a62f49e56610d38a1c9502a9.jpg
 
aiseee.Okay.Kwa hio ndio maana lilijengwa kwenye road reserve?

libomolewe tu.Lowasa Fisadi sana.Nilikuwa najiuliza ..how come serikali ijenge kwenye road reserve..kumbe ni mwizi Lowasa

wabomoe haraka sana
Wezi hushtakiwa na wakikutwa na hatia,hufungwa.Huyu Lowassa sijawahi ona anashtakiwa ,najiuliza yeye ni Nani na ana nini? Kwanini serikali na vyombo vyake vimebaki kulalamika tuu?
 
Nenda kachukue vifusi sasa

Ova
 
aiseee.Okay.Kwa hio ndio maana lilijengwa kwenye road reserve?

libomolewe tu.Lowasa Fisadi sana.Nilikuwa najiuliza ..how come serikali ijenge kwenye road reserve..kumbe ni mwizi Lowasa

wabomoe haraka sana
La wizara la maji La tundu lissu nalo

Ova
 
aiseee.Okay.Kwa hio ndio maana lilijengwa kwenye road reserve?

libomolewe tu.Lowasa Fisadi sana.Nilikuwa najiuliza ..how come serikali ijenge kwenye road reserve..kumbe ni mwizi Lowasa

wabomoe haraka sana
Tatizo mmeaminishwa vibaya, nikikuuliza Lowassa amefisadi nini? Hauta kaa ueleze mpaka unakufa.
 
Wezi hushtakiwa na wakikutwa na hatia,hufungwa.Huyu Lowassa sijawahi ona anashtakiwa ,najiuliza yeye ni Nani na ana nini? Kwanini serikali na vyombo vyake vimebaki kulalamika tuu?
Kama walioshtakiwa ndio wezi na mafisadi wa nchi hii basi hii nchi haina wezi na mafisadi maana kwa walioshtakiwa na kukutwa na hatia ni wachache sana.
Kushtakiwa na kuwa fisadi na mwizi ni vitu viwili tofauti na sheria na haki pia ni vitu viwili tofauti.
Kweli wanasiasa mnashida sana yaani unaona madudu ya serikali halafu unawaondoa hao viongozi eti hawahusiki labda uwe unatatizo la akili.
Labda unambie ufisadi huwa unafanyika hewani bila watu kushiriki.
Hakuna viongizi wa ngazi ya juu serikalini walio wasafi 100% awe amehama CCM awe hajahama mimi bado nawaona wanakesi ya kujibu kwetu watanzania.
Wasitwambie tukawashtaki ili mahakama zifuate sheria tunataka haki na haki haipatikani mahakamani kwa kuwa haki na sheria haziko pamoja.
 
Tatizo mmeaminishwa vibaya, nikikuuliza Lowassa amefisadi nini? Hauta kaa ueleze mpaka unakufa.
Ni ajabu waziri kujenga jengo lake kwenye road reserve.. Huo ni ufisadi tosha
Pia hayo mabilioni ameyatoa wapi
 
You are among the fews continuing letting #JF to be untrusted source of news.
Unamjua mmiliki wa hilo jengo? Unajua wenye hisa kubwa kwenye hlo jengo? Kama nimesema uongo bas thibitisha kwa kusema ukweli..if u fail to do so.. u 'r a fuckng pumpkin..
 
Back
Top Bottom