Nikitilia maani uwiano wa idadi ya watu wanaopita hapo kwa nikilinganisha na sehemu nyingine; mbona hapo pana uafadhali!!
Mara ya mwisho nimecheck kama wiki tatu hivi, vyoo vilikuwa na maji na viko katika kiwango cha kutumika kwa mtu aliyebanwa!!! Kumbuka kuna pahala penye mikusanyiko nimefika, yaani hata kama haja imekubana, unconsciously unajikuta umepata ahueni baada ya kuona mazingira yenye kinyaa chakupindukia pahala pa kujisaidia.
Wizi wa vitu pia umepungua, maana hawaruhusu tena wapokeaji kuingia ndani ya uzio kiurahisi kama ilivyokuwa mwanzo. Mabasi pia yanaondoka on time kuanza safari zake.
Uchafu kama unavyoonekana hapo kwenye picha ni matokeo ya hulka za wengi wetu. Ndivyo tulivyo; haswa Dar na 'umjini-umjini' kama sifa'!!! Inaudhi sana na ni kero kubwa.