Ubunge wa Mgimwa Kutenguliwa na Mahakama

Ubunge wa Mgimwa Kutenguliwa na Mahakama

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,705
Reaction score
29,136
Nikiuangalia ubunge wa Mgimwa kwa jicho la kisheria, naona kama ubunge wake unaning'inia kwa utando wa buibui? Kwa nini? Kuna sababu mbili kuu (na nyingine nisizozijua) ambazo kama zikitiliwa nyama za kisheria, zinaweza kupelekea Mgimwa kunyanganywa ubunge wake:

Mosi, wakati Bw Nchemba akimnadi Mgimwa huko Kalenga alitamka hadaharani kwamba yeye alikuwa akimnadi mgombea huyo akiwa kama Naibu Katibu Mkuu na kama Naibu Waziri wa Fedha. Alisikika akiwaomba wananchi wampe ubunge Mgimwa kwa kuwa kama wakichagua mbunge wa upinzani, hatampa ushirikiano wowote ila kama wakimchagua Mgimwa atahakikisha anatenga fedha kwa ajili ya maendeleo ya jimbo la Kalenga.

Naomba turejee nyuma hadi kule Igunga kwenye ‘daraja la Magufuli'. Magufuli aliwaahidi wanaIgunga kwamba wakimchagua mgombea wa CCM atawajengea daraja. Hii sababu ilitosha kabisa kutengua ubunge wa Dr Kafumu. Hakuna tofauti yoyote kati ya ahadi hii ya Magufuli na ahadi ya Nchemba.

Pili, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inadaiwa kuchomekea kimyakimya majina zaidi ya 10,000 ya wanaCCM kwa kisingizio cha kuboresha daftari la wapiga kura huku ikiwa inajulikana wazi kwamba maboresho hayo yamefanywa kinyemela kwa lengo la kuibeba CCM. Hili dai linaweza likawa gumu kuthibitisha lakini likisimamiwa na wakili mashuhuri kama Tundu Lissu, Profesa Safari au Peter Kibatala, linaweza kujengewa hoja za kisheria na hatimaye kupelekea kutenguliwa kwa ubunge wa Mgimwa.

Hizi hoja mbili, ukizitazama kwa jicho la ushabiki wa kisiasa, unaweza ukadhani kwamba sio nzito kihivyo lakini ukizitazama kwa jicho angavu la kisheria, utagundua kwamba ubunge wa Mgimwa unananing'inia kwenye kuti kavu. Nina uhakika ushahidi huu ukiunganishwa na ushahidi mwigine utakaokusanywa kutoka eneo la uchaguzi, unatosha kabisa kupelekea ubunge wa Mgimwa kutenguliwa mahakamani.
:yield:
 
Ngoja nifikili vizuri nitarudi.!!! kama naona kuna jambo zito hapa..
 
Nilishasema, kimya kingi kina mshindo Mkuu. Hebu tusubiri.

Sent from my Lumia phone using Tapatalk
 
Mkuu kama hilo la kwanza ni kweli madelu alilitamka na ushahidi ukapatikana wa video na sauti isiyo na shaka basi hapo ni shida mahakamani, na ni kweli ya igunga yatajirudia kabisa.

Hilo la pili chadema wakiamua kujua ukweli unabainika kama kuna hao watu 10,000 waliongezwa basi hapo ni shida pia, nami nilisikia hilo daftari lililotumika ni la 2014, sasa nikajiuliza limeboreshwa lini na kwa maeneo yapi sikupata jibu..

Ngoja tusubiri wajuvi wa mambo haya waje watueleweshe sheria zimekaaje...

Wadau karibuni kwa mawazo na mwenye ushahidi wa lolote kuhusu haya tafadhali..
 
kwani ile judgement ya igunga on appeal ili hold water? waweza nipatia kama unayo
 
CDM mjipange upya...kunahitajika strategies za ukweli kuweza kuwashinda CCM wenye vyombo vya dola, Mahakama, Tume ya Uchaguzi, Fedha nyingi, Majangili wa Kijani na hata the so called wawekezaji wenye kuipigia CCM chapuo kwa maslahi yao....
 
Hamna lolote, tunawasubil tenaaaaaaaa CHALINZE.
 
Hamna lolote, tunawasubil tenaaaaaaaa CHALINZE.
chalinze nako mmeshabadili daftari la wapiga kura kinyemela na kuweka makada wenu?kuna wasiojua kusoma wa kutosha,mtawapa karatasi zaidi ya moja wapiga kura ili wapige kura, mtaweka kituo sebuleni kwa kiongozi wa CCM?Bado mgombe wenu akachaguliwa na uchaguzi waliopiga kura ni chini ya asilimia 50 ya watu wote waliojiandikisha kupiga kura. unhaguzi walioshinda na kushangilia walikuwa wachache kuliko waliosikitika kw akilichotokea?
 
safari ya ukombozi bado ni ndefu sana, ccm wame wapumbaza watz sana hebu tizama mambo yaliyotokea ktk taifa hili na kutopatiwa majibu kutekwa kwa dr Ulimboka mauaji ya Mwongosi Dr Mvungi Mabomu Olasiti kanisani Mabomu soweto Arusha.... yaani nimegundua kila likiwanyika tukio lisilo la kawaida polisi wanakamata mtu yeyote kama yule mkenya wa Dr Ulimboka ili kutuliza maboya.
 
Hili suala limewakalia vibaya CCM---ngoja tusubiri mawakili wa CHADEMA wajipange kupeleleka utetezi wao mahakamani. Hakika CCM mtaangukua pua mahakamani.
 
Kiukweli ni upuuzi mkubwa kwa chama chetu,kushiriki uchaguzi kwa sheria na kanuni zile zile,daftari lile lile la 2010.
 
Hata uchaguzi ukirudiwa mara 20 Chadema hawawezi kushinda Kalenga huo ndio ukweli.
 
Kwa sasa kukata appeal haitasaidia kwani mpaka appeal kuja kusikilizwa tayari tutakuwa tunaingia kwenye uchaguzi mwingine.
 
Jana nilisema na nikabainisha kuhusu biashara zinazoendelea ndani ya CHADEMA.

Kwa sasa kitakachotengenezwa tena ni deal kwa mawakili ndani ya chama ili na wao wapate ulaji kiutaratibu kama ilivyo kwa viongozi wakuu na mmiliki wa chama. Keki ya CHADEMA kutoka hazina inawafikia wajanja pekee ndani ya chama.

Jana nilisema hivi,
Biashara ya CHADEMA na huyu mama kuanzia leo imeisha.

CHADEMA walitegemea kupitia ubunge wake wangeongeza pesa za ruzuku kutoka hazina lakini hawako tayari kutoa pesa zaidi kumsaidia yeye katika manufaa yake ya kimaisha bila CHADEMA kupata faida zaidi kifedha.

Inawezekana baadhi ya mawakili ndani ya chama wakamshawishi kufungua kesi ili na wao wapate ulaji kwa njia nyingine. Kina Peter Kibatala, Tundu Lissu and co- wanajiandaa kwa biashara nyingine.

Ndani ya CHADEMA na hasa kwa wamiliki wa chama, kauli mbiu yao ni biashara kwanza siasa baadaye.

Under CHADEMA phoney manifesto, she is outcast from today.

Ndani ya thread hii,
 
Back
Top Bottom