Ubunge Ubungo: Karata au zawadi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubunge Ubungo: Karata au zawadi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ABEDNEGO, Feb 21, 2010.

 1. ABEDNEGO

  ABEDNEGO Senior Member

  #1
  Feb 21, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tumechoshwa na hadidu rejea Kiti cha Ubunge Jimbo la Ubungo kinanadiwa na CCM kana kwamba Ubungo haina wenyewe,Alikuja Lamwai(NCCR kwa malumbano m,azito maendeleo hayakuonekana),Kafuata Keenja(vipindi viwili bila lolote) sasa tunaandaliwa kumpokea Mwangunga(Ambaye wizara ya mali asili imemshinda tunaletewa atusaidie nini??!!Sasa sisi wananchi wa Ubungo tunashindwa kuelewa kupewa ubunge wa Ubungo ni zawadi tuu au ni ushindani?
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,120
  Likes Received: 27,077
  Trophy Points: 280
  Mnyika hamumuoni? wapiga kura ni kina nani kwani?
   
 3. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,515
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 160
  Na huyo Nape ameishia wapi maana nilisikia na yeye alikuwa analitaka hilo jimbo. Ukweli ni kwamba CCM haijawahi kushinda kihalali jimbo la Ubungo. Mara zote wanafanya wizi tu. Mara ya mwisho Chadema walishinda lakini tume ikaamua vinginevyo. Na kwa mtindo wa sasa kwamba wawakilishi wa vyama kwenye vituo hawalipwi tena na tume ya uchanguzi (nafikiri ndivyo ilivyo kwa sasa), CCM wanakuja na rushwa yao na kuwaonga mawakala wa vyama na kusaini matokeo ya uongo kwenye vituo kuonyesha kwamba CCM imeshinda. Kuna haja ya kuangalia ni jinsi gani tunaweza kulinda kura zetu badala ya kutegemea watu wachache wanaowekwa na vyama kama mawakala.

  Na wana Ubungo inabidi tufike mahali tuchoke kulazimishwa na CCM kuwa na wabunge wasioijua ubungo. Wagombea wote walioletwa na CCM kugombea ubungo hakuna hata mmoja anakaa Ubungo. Hatutaki mtu akae Masaki au Osterbay halafu eti aje kugombea kuwa mbunge wa jimbo la ubungo. Huyu atayajuaje matatizo yaliyopo Ubungo? Kwa kuambiwa tu? No tunataka mtu anayekaa kati ya wakazi wa Ubungo ndiye aje tumpe Ubunge.

  Mnyika, Usiache kugombea tena lakini tengeneza utaratibu mzuri wa kulinda zetu.

  Tiba
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  Feb 21, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,235
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Rafiki yangu wewe hukai ubungo kwanza uko ubungo gani mimi naishi ubungo toka mwaka 90 najua mengi kuhusu hapa ubungo unachojaribu kufanya wewe ni kupata mawazo ya wengine pengine uandae makala , nenda gide kwa mfano uliza kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita mpaka sasa kuna maendeleo gani haswa kwenye sekta ya maji mtandao wa maji ,
   
 5. ABEDNEGO

  ABEDNEGO Senior Member

  #5
  Feb 22, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu mimi ni mzaliwa wa Ubungo nimekulia Ubungo na kusoma Ubungo sasa nazeekea Ubungo hayo unayoyasema ni sehemu ndogo sana ya maendeleo kwani hata huo mradi wa maji Gide siyo juhudi za hao watu unaowaita Wabunge wakuja,Ni mpango wa miaka kadhaa wa serikali baada ya kuona wananchi wanatoboa bomba linalopita Ubungo kwani wao walikuwa hawapati hayo maji,
   
 6. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,878
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Mbona huo mtandao wa maji, hasa ule wa Mchina kule Kimara yote una kizaazaa? Kuna watu hawapati kabisa maji na wengine mara wanapata kwa nusu saa, mara robo saa tu, maximum masaa mawili!! Nini hii? Any way, Shy waweza kudokeza hao ndugu zetu wa Makoka, Kilungule, King'onko, Baruti, Msewe, Kibo, Rombo, Suca, Kwa Msuguri etc watapata lini maji ya uhakika? Wabunge wa huko wana ajenda gani ya kuhakikisha angalau hayo mabomba ya Mchina yanatoa maji? Unajua kuwa hali hii inachosha?
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,196
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Mbunge wa Ubungo anajulikana, wakamuulize Keenja.
   
 8. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuletewa ??? !!!!!! Wacha nikushangae kidogo. Mnaletewa na nani ?? Kwani mmlazimishwa ?????? Nawe ukitaka si kagombee.....unalalamika wakati kisu unacho mkononi !!! Usijidhalilishe wakwetu.
   
 9. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,834
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 180
  Mzee Kibiongo,

  Wananchi wa Ubungo HAWANA MWAMKO wa Maendeleo!

  Na ndio maana unaona mitaa hiyo mambo hayaende popote - mtaletewa Wabunge mpaka mkome! Nadhani tatizo pia sehemu kubwa ya Ubungo ni Makazi yasiyo rasmi! Ni maeneo machache ya Ubungo gari inaweza kufika nyumbani kwa mkaazi!
   
 10. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 370
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mkuu unauhakika wanafanya wizi wa kura, weka vithibitisho hapa jamvini na si kuongea kinadharia tu.
   
 11. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #11
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,235
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Hata kile cha juu ulichoongea mwanzo ni mipango ya serikali hata hivyo maeneo mengi yaliyobakiwa na matatizo ya maji mpaka sasa hivi ambapo mradi huo umepita wao wenyewe ndio tatizo kwa sababu walikuwa wanahonga wale vijana wachimba mitaro wapeleka maji maeneo yao ambayo hayakwepo kwenye ramani sasa mtu anapokosa maji ana mlaumu tani ? wewe uliza wengi walio kosa maji utaambiwa walihonga vijana wakaunganishiwa ndivyo sivyo

  Na hilo neno la wabunge wakuja mimi sielewi huu ni ubaguzi
   
 12. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kitu kimoja ambacho baadhi ya watu wanadharau kukizingatia ni kuwa, Ubungo inakua kwa kasi sana. Ongezeko la makazi ya watu katika jimbo hilo ni kubwa na la haraka kuliko sehemu yoyote ya Jiji. Na kila inapotokea ongezeko hilo, mahitaji mapya hujitokeza na yanapojitokeza yanasababisha malalamiko mapya.

  Ukweli ni kwamba, Ubungo ya leo sio ilivyokuwa miaka michache ya nyuma. Nakumbuka mwaka 2000 sehemu kama Mavurunza, King'ong'o na nyinginezo zilikuwa hazifikiki na wala hayakuwa makazi ya kutarajiwa. Sehemu kama Goba ambazo zinapitika kwa urahisi sasa zilikuwa ngumu pia. Ukienda Goba leo, utashuhudia ukuaji wa kasi uliofanyika. Ni sehemu ambayo kupata ardhi ni ngumu kama sehemu nyingi za Jiji ambazo zimeendelea sana. Nina rafiki yangu mmoja alinunua ardhi mwaka 2000 kwa shilingi 3.5mil (nusu eka), sasa ardhi kama hiyo ni 35mil na haipatikani kwa urahisi.

  Ukweli utabaki kuwa, hakuna Mbunge anaeweza kufanya kila kitu kinachotarajiwa na watu wote hasa katika nchi masikini na yenye mahitaji mengi kama Tanzania. Hakuna Mbunge anaeweza kuhakikisha maji yanamfikia kila mtu, kwa wakati yanapohitajika bila kuwa na malalamiko yoyote.

  Miaka mitano iliyopita, maji lilikuwa tatizo kubwa sana Ubungo. Na kama wengine watakumbuka, wananchi wengi walitaka hilo ndio liwe tatizo la kufanyiwa kazi pekee (ingetosha). Angalau leo yanapatikana walau kidogo (kwa mgao). Tofauti na umeme au baadhi ya mahitaji mengine, maji hayatengenezwi kwa mitambo au viwandani. Yanakusanywa na kusambazwa. Kiasi kinachoweza kumfikia mtu mahali alipo, kinategemea sana miundombinu iliyopo na umbali, terrain na kadhalika ambazo mtu huyo anaishi.

  Anyway, mwaka wa uchaguzi umefika. Ubungo itakuwa na Mbunge mpya ifikapo mwisho wa mwaka huu. Inawezekana akaja na maajabu.
   
 13. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #13
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,235
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  mbunge hawezi kutuletea maendeleo wala viongozi maendeleo yanaletwa na watu wenyewe wanapoamua na kuwa na mipango imara tunaweza kuwatumia wabunge kama chambo tu , ndugu abed wewe ni mwanachama wa kikundi chochote cha maendeleo ubungo ukiacha vinavyofadhliwa na vyama vya siasa ?

  Kama ni mwanachama wa vikundi hivyo naamini huwa unahudhuria mikutano ya vikundi na kupokea taarifa za mara kwamara kuhusu maendeleo ya sehemu kadhaa ambapo vikundi hivyo vipo naomba unitajie jina la kikundi chako kama hakikuwahi kuwapa ripoti ya miaka 2 tu iliyopita
   
 14. ABEDNEGO

  ABEDNEGO Senior Member

  #14
  Feb 22, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kibiongo wewe uko wapi??Mbona kura tulimpigia Mnyika akachaguliwa Keenja?Mbona hilo liko wazi kabisa?Uchaguzi wa 2005 kituo kimoja wapiga kura waliojiandikisha pale Royal EDP ni 3561 Waliopiga kura jumla walikuwa 4,005 tofauti hiyo ilitoka wapi?Tunajua kinachoendelea ndani ya Uchaguzi wa nchi maskini,Hili la Ubungo tunalielewa sisi wakaazi wa huku,Hakuna Mbunge aliyechaguliwa wa chama tawala ambaye maskani yake ni Ubungo.a shida za ubungo siyo maji tuu Mbunge kukutana na watu wake,kujua matatizo ya watu wake nk
   
 15. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #15
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,235
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Ndugu kinachotakiwa ni mipango inayotekelezeka kwa kuanzia na wananchi wenyewe wa maeneo husika kama wananchi hawataki kufanya kazi , kupeleka watoto wao shule , kupigania haki zao mpaka mbunge aje tena anayekaa hapo hapo unataka nini zaidi ? anza michakato hiyo mitaani humu jf kuna wachache sana wanaoishi ubungo pia ni watu wachache sana waliounganishwa kwenye mtandao wa kompyuta ubungo jitihada hizi angalia upya
   
 16. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 366
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Shy Ubungo ni Jimbo muhimu sana kwa uchaguzi ndani ya nchi hii,Acha watu watoe maoni yao!!Hapo kuna jambo la kuongea!
   
 17. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #17
  Feb 22, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Sijui kama una uhakika na unachokisema. Lakini ngoja nichukulie kuwa unachokisema una uhakika nacho.

  Mkuu, mwaka 2005 Mnyika alijitahidi sana. Maana alipata kura nyingi kuliko wagombea wote wa upinzani. Baadhi ya wagombea hao ni maharufu sana tu. Ila ukumbuke pia kuwa, mwaka huo huo, CCM walipata kura zaidi ya wagombea wote wa upinzani kwa pamoja (walikuwa 13 kwa ujumla).

  Inawezekana kuwa wewe na wengine wachache walimpigia Mnyika kura na nmaamini kura zenu ni lazima ziwe za ushindi (confidence nzuri, naipenda). Ila inaelekea wengi zaidi hawakumpigia kura Mnyika, hivyo hazikutosha. Tusubiri mwaka huu, namuombea sana ndugu yangu Mnyika apate kura za kutosha ili aweze kujaribu kufanya anayokusudia kwa wananchi wa Ubungo.

  Kwa jinsi jimbo la Ubungo lilivyo, si rahisi sana kwa upinzani kushinda Ubunge pale. Sio rahisi zaidi kutokana na wingi wa wapinzani ambao hujitokeza kugombea Ubunge pale. Utaendelea kushuhudia wapinzani wakishindwa pale kwasababu hii zaidi ya nyingine mnazo jaribu kutabiri.

  Jimbo la Ubungo limewahi kuwa na wabunge wa upinzani mara kadhaa, tena watu maharufu tu. Wananchi wa Ubungo wanajua nini wanachoweza kukipata kutoka upinzani. Lakini hilo pekee sio tatizo. Tatizo ni kuwa CCM imejiweka sawa sana Ubungo.

  Mgombea wa CCM akikubalika na chama chake, ni rahisi sana kumshinda mgombea mwingine yeyote wa upinzani kwenye uchaguzi mkuu. Hiyo ndio siri ambayo si ajabu huijui.
   
 18. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,515
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 160
  Mkuu Nyuki,

  Wewe ni mmoja wa akina Tomaso!!!!!! Ushahidi unaoutaka sitauweka hapa kama unavyotaka lakini ukweli utabaki kuwa ukweli.

  Tiba
   
 19. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Majimbo ya DSM yanagawanywa: Jimbo la Ubungo litakuwa majimbo mawili, Jimbo la Ubungo lenye kata za Ubungo, Sinza, Manzese, Mabibo, Makurumla, Mburahati na Kigogo. Jimbo jipya la Kibamba litakuwa na kata za makuburi, kimara, mbezi na kibamba. Jimbo la Kawe litakuwa na Jimbo jipya la Bunju. Jimbo la Ukonga litazaa jimbo jipya la Segerea, Majimbo ya Temeke na Kigamboni yatazaa jimbo jipya la Mbagala. Hayo ni mapendekezo ya RCC iliyofanyika leo

  PM
   
 20. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2010
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 369
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  MPs work for something larger than themselves. The lead by example and maintain an open and honest dialog with their direct reports and everyone in-between. They have the desire and ability to utilize vision for the benefit of the people. They protect the people and constuency at any cost. They always speak the truth no matter how difficult. They have the complete trust of their wananchi and even non-wapiga kura due to it being earned through years of leading by example, critical conversations, and alignment with people of similar character/karma. They consider it a requirement to mentor others and allow them to grow. They always give credit to the wananchi. They understand they are only as good as the people that follow them. A Mbunge always listens to both sides before making a decision. A Mbunge doesn’t micro-manage because it simply is not required. A leader always gives the benefit of the doubt. A leader recognizes that people can be expendable but will do everything they can to motivate, improve, et cetera before making that final decision. Consider the case of Keenja and other Ubunge aspirant for Ubungo !
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...