Elections 2010 Ubunge jimbo la Hai

watanzania viva! hakuna kulala mpaka kieleweke!
mabadiliko ya kweliuhuru wa kweli!
chadema viva
mbowe viva
silaa viva
ndesa pesa viva
maendele ya kweli hayawezi kuletwa na mafisadi yale yale eti kwa ari mpya na nguvu mpya na kasi mpya
KIla mtanzania mwenye akili huu ni wakati wa kujiuliza ajira million moja kila mwaka ziko wapi? maisha bora yako wapi? kasi imefikia wapi? au ni kasi ya kwenda kutanua ughaibuni? au ni kasi ya kimbita kwenda kuuliza mtutu wa kuulia nyani? au ni kasi ya richmond? au ni kasi ya kupeleka mafisadi uchwara mahakamani na kuacha mapapa yakitamba? vp deep green na mereremeta?
kuna sababu ya kumwachia mwewe chakula cha mtoto?
wabunge tunaongeza na rais mwaka huu ni mali ya chadema
freeman hana haja ya kushindana na na fuya au mushi kwani hayo ni magerersha. ndesa pesa usijali Mengi akitoa lazima atoke ITV kwani kuna mtu amfahamu.
sijui Mengi unijipendekeza nini huko CCm wakati ukweli ni kwamba hawakupendi. sophia si alishakueleza ukweli. rostam umemsahau. je masha. je umesahau ndesa ilimbidi ajiuzulu kamati ya nidhamu kwa ajili ya hao ccm kuhongwa umeshau zengwe lako na malima?
mwaka huu kila mtanzania tunasababu ya kuondoa kila uchafu ulioko ccm.
na anayetaka kutest kiberiti atest.
awenia mushi ni mtu mdogo sana kwenye siasa
hata ukiwa na akili kama za prof sarungi ukiwa ccm wewe ni bure kabisa
ccm ya kina nyerere , sokoine ,eliufoo, nsilo swai sio ccm ya kikwete,mengi ,vicky nsilo swai, fuya ukweli ni kwamba hii ya sasa wamechoka kimawazo,sio kwamba nawachukia ukweli ni hamna kitu kichwani
watu hamuoni ambulence lakini mahindra za kampeni, na sasa ni cruiser hardtop zinaonekana ili watu waweze kubakiza ulaji wao lakini mkifa kwa kukosa afya aaa hiyo haina noma. hivi kuna nini hadi mtumie billon 50. kweli ningekuwa na roho mbaya ningekuwa ccm ili nizile. ila nimezisusia sitakia hata senti
nataka haki yangu
pesa haiwezi kunifanya mtu .mimi ni mimi nikiwa maskini ni mimi nikiwa tajiri ni mimi. haki yangu utu wa wangu
 
Mkuu Cathbert,

Kuna ahadi ambazo Mbowe alituahidi wapiga kura wake kwenye kampeni mwaka 2000,alitekeleza 100% na zingine akatekeleza hata amabazo hazikua kwenye ahadi zake za kampeni kama umaliziaji wa majengo Lyamungo sekondari,vifaa kama computer nk

Mzee hebu sasa kuwa fair.

Pia vipi huyo jama aliyepewa ukamanda wa wilaya ya Rombo huyo ndugu Prosper Silayo?

Naomba unitajie ahadi zake tano tu alizotekeleza.
 
Hilo nalo ni tatizo ila jamaa nguvu yake kubwa inatoka kwa Mwenyekiti wa mkoa wa Kilimanjaro Vicki Nsilo Swai

View attachment 9848
Mama Vicki Nsilo Swai (ktk)

Huyu Mama ana nguvu sana kwa mkoa wa Kilimanjaro na yeye ndiye anasuka mpago wa kumngoa Mzee Ndesamburo jimbo la Moshi mjini.N hivi karibuni wataitisha harambee maalumu ya kuchangia CCM ili kumngoa Mzee Ndesa.

Hana nguvu yoyote CCM hawajawahi kuchukua jimbo la Moshi Mjini tangu vyama vya upinzani vimeanza
 
Mkuu,itakuwa vizuri kama ungetujulisha huyo Bw.Meena ni nani? au tupatie jina lake kamili!
Hana lolote alisha gombea akashishindwa, sasa hivi Mh Fuya amepata neema barabara aliyo ahidi wapiga kura itajengwa inajengwa ambayo ilikuwa ni kero kubwa kwa watu wa masama hivyo ni vigumu mtu kumshinda
 
CCM hawalitaki jimbo la Moshi. Wangekuwa wanalitaka wangebadili namna wanavyolitafuta.
 
Ni vizuri kuacha watu watoe maoni yao, kama alivyozungunza manasaikolojia mmoja kuwa usimzuie mtu kusema hata kama anaongea na ukuta. Ukiangalia yale watanzania wakereketwa wa hali ndivyo sivyo ya serikali ya CCM, ni kama vile wanaongea na ukuta, itawasaidia kuondoa stress, ingawa ukuta hautakusikiliza, labda tu uigize sauti yako kwa kile kunachoitwa mwangwi. Yaliyosemwa juu ya CCM na serikali yake ni mengi ila sidhani kama wanawasikiliza. Ila tuendelee kuzungunza kuondoa stress.

Kuhusu jimbo hili la Hai ni kati ya majimbo ya kushangaza sana. Utaniuliza kwa nini? Sina kumbukumbu kama alishawahi kutokea mbunge aliyeweza kutetea kiti chake ktk jimbo hili (Naomba wenye historia sahihi wanijuze). Kabla ya kuuliza nani agombee mwaka huu na atoke chama gani, ni lazima tujiulize kama hawa wananchi wa Hai wanamwitaji mbunge au la? Walishajaribu wabunge wa CCM, TLP, na CHADEMA lakini bado hawajapata mwakilishi wanayemtaka. Ni lazima tuwaulize watu wa hai kuwa wanamtaka mwakilishi wa namna gani na awafanyie nini? Ukiangalia mbunge wa sasa Ndg. Fuya hakuna alichokifanya kwa kipindi cha miaka karibia mitano.

Ninaomba tufahamu wazi kabisa jimbo la Hai linahitaji a serious person, sio watu kama akina Fuya. Wanaowafahamu wakazi wa eneo hili watakubaliana nami kuwa ni watu wasio na maneno mengi bali vitendo. Kwa maoni yangu hili jimbo linamwitaji mtu makini kuliko tunavyoonekana wengi kujadili hapa. Kama hayupo ni vyema wakae bila mbunge kwa kipindi cha miaka mitano ili pia wapime faida na hasara za kuwa na kuto kuwa na mbunge.

Ninazungunza kama mzawa wa Wilaya na jimbo hili.
 
Kati ya hawa wagombea watatu hakuna hata mmoja ambaye anaweza kuwarizisha wakazi wa hai, Mbowe alikuwa mbunge wako kwa kipindi cha miaka mitano hakuna la maana alilo lifanya zaidi ya kutoa misaada kama alivyo sema Kwayu,Fuya naye hakuna alichokifanya naye.

Huyu Mushi nae anaonekana sio mtu makini kabisa, kama ameweza kutoa pesa za kujenga daraja na akashindwa kuzi simamia hafai kabisa..

Tanzania ya sasa inahitaji watu makini na wenye uchungu na hii nchi siyo hawa wanao angalia matumbo yao tu, na kuuza nchi kwa wageni.
 
Huko Moshi kwenu kuna kazi. Nasikia kuna na mwanamke mmoja naye anataka kujitosa, mtauana wachaga.
 
Hilo nalo ni tatizo ila jamaa nguvu yake kubwa inatoka kwa Mwenyekiti wa mkoa wa Kilimanjaro Vicki Nsilo Swai

Mama Vicki Nsilo Swai (ktk)

Huyu Mama ana nguvu sana kwa mkoa wa Kilimanjaro na yeye ndiye anasuka mpago wa kumngoa Mzee Ndesamburo jimbo la Moshi mjini.N hivi karibuni wataitisha harambee maalumu ya kuchangia CCM ili kumngoa Mzee Ndesa.

Hana ushawishi mkubwa kihivyo. Na wala hawezi kuongea chochote kwa sasa mbele ya Ndesa Pesa. Vyeo vingine vya kusaidiana tu. Mi sijaona ushawishi wa huyu mama. Tutaonana baada ya uchaguzi
 
Kumshinda Ndesa Moshi ni ndoto.. labda aamue tu mwenyewe kuwapisha.Watu wa Moshi Mjini washapita kwenye level za kuhongwa pilau na Kanga, wanafahamu nini wajibu wao kama wananchi na ni nani wamchague atakayesimamia mambo yao. Mama Kilango alipita pale kujaribu kutikisa kiberiti nafikiri anayo majibu mazuri tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom