Ubovu wa barabara toka TANESCO Kidatu kwenda Ifakara

FORWARD

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
740
293
Salamu ziwafikie wahusika,

Tunaambiwa "turudi shambani tukalime" lakini kwa barabara zisizo na ubora tutachelewa sana, toka Mikumi mpaka Ifakara (kwenye mashamba ya mpunga) kuna umbali wa kilometa 100. Kwa usafiri wa basi utatumia mpaka masaa manne na kuendelea, barabara ina Mashimo na haifanyiwi matengenezo yanayoridhisha.

Tunaomba wahusika muikumbuke hii barabara maana vipuri vya magari vinaharibika sana ukipita barabara hii kubwa ya Mikumi kuelekea Ifakara.
 
Salamu ziwafikie wahusika, tunaambiwa "turudi shambani tukalime" lakini kwa barabara zisizo na ubora tutachelewa sana, toka Mikumi mpaka Ifakara (kwenye mashamba ya mpunga) kuna umbali wa kilometa 100. Kwa usafiri wa basi utatumia mpaka manne na kuendelea, barabara ina Mashimo na haifanyiwi matengenezo yanayoridhisha!

Tunaomba wahusika muikumbuke hii barabara maana magari vipuri vya magari vinaharibika sana ukipita barabara hii kubwa ya Mikumi kuelekea Ifakara.

Hii barabara ina umuhimu mkubwa sana kiuchumi. Inaelekea kwenye mashamba ya mpunga ya wakulia wadogo na wakubwa kilombero, inaelekea kwenye misitu yenye thamani kubwa ya mitiki, inaelekea kwenye mitambo ya kufua umeme ya kihansi, chuo kikuu cha afya cha st. francis pamoja na hospitali teule ya st francis etc etc. Lakini inaonekana hizo Kilometa 100 hazijapewa umuhimu wowote na serikali. Serikali ya Uswiswi ilijenga Km 30 toka mikumi hadi kidatu miaka kadhaa iliyopita kwa mategemeo kwamba serikali ya tanzania nayo pia ingeweza kupunguza walau kilometa 30 toka kidatu kelekea ifakara... lakini inaonekana bado uchambuzi yakinifu unaendelea
 
Hata kama bado ipo kwenye "feasibility study", lakini wanapaswa kuirekebisha kwa kiwango kizuri cha "gravel" na kuwekeka mitaro ili kupunguza ghasia iliyopo kwa sasa.
 
Salamu ziwafikie wahusika,

Tunaambiwa "turudi shambani tukalime" lakini kwa barabara zisizo na ubora tutachelewa sana, toka Mikumi mpaka Ifakara (kwenye mashamba ya mpunga) kuna umbali wa kilometa 100. Kwa usafiri wa basi utatumia mpaka masaa manne na kuendelea, barabara ina Mashimo na haifanyiwi matengenezo yanayoridhisha.

Tunaomba wahusika muikumbuke hii barabara maana vipuri vya magari vinaharibika sana ukipita barabara hii kubwa ya Mikumi kuelekea Ifakara.

Umenikumbusha Tanesco Kidatu...dah long time!
 
Hii barabara ni nyoko imenifanya nipande tren ambalo lina kila aina ya karaha
 
Tanroads mbona mmeitelekeza njia hii? Mkipata wakandarasi wazur wanaweza hata kuipendezesha kwa kiwango cha vumbi tukisubiri mmalize michakato ya utengenezaji kwa kiwango cha lami.

Siku moja mpande basi la kwenda ifakara mtaiona karaha nayoizungumzia.
 
Hii barabara ya ifakara yaani bado haijajengwa?!nmetoka ifakara mwaka 2007..!barabara ile mbovu ajabu..yaani unatembea kwa Massa 12 kwa bus kutoka ifakara mpaka Moro town.
 
Salamu ziwafikie wahusika,

Tunaambiwa "turudi shambani tukalime" lakini kwa barabara zisizo na ubora tutachelewa sana, toka Mikumi mpaka Ifakara (kwenye mashamba ya mpunga) kuna umbali wa kilometa 100. Kwa usafiri wa basi utatumia mpaka masaa manne na kuendelea, barabara ina Mashimo na haifanyiwi matengenezo yanayoridhisha.

Tunaomba wahusika muikumbuke hii barabara maana vipuri vya magari vinaharibika sana ukipita barabara hii kubwa ya Mikumi kuelekea Ifakara.
Nilipita barabara hiyo mwaka jana Septemba,kwa kweli hali ni mbala sana kwa hiyo barabara amabayo ina mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi,shida ni kwamba wenyeji wa huko wandamba,wapogoro nk wengi wao ni wavivu kufikiri na kuchagua wabunge wasio jali kwao na kuishi muda mwingi DAR na kudhani ndio kwao,si mlisikia mbunge wa Ulanga Mashariki (Mahenge) akimpigia chapuo Diamond,badala ya kuzungumzia changamoto za barabara hiyo ambayo ni kiunganishi kikubwa cha kufika Mahenge/jimboni kwake.

Kuna watu wengi walipata kushika madaraka makubwa kutokea pande hizo,lakini wote wapo kuangalia mambo yao tu kwa kuwa wanatumia magari ya serikali nk.
Ninapata shida sana kila nitakapo kwenda kwetu Ifakara,Chita,Merera nk
Ila nashindwa uwezo tu,nipo tayari kuchangia ikiwa kutakuwa na mfuko maalumu wa kujenga barabara hiyo!!
 
Barabara ya kidatu--kilombero haina tofauti kabisa na ile ya nyololo--mgololo! zote zipo chini ya tanroad na ni muhimu kiuchumi lakini suala la kuzipiga lami limetawaliwa na siasa na porojo tu! Mara sijui tupo kwenye upembuzi yakinifu!! mara sijui tupo kwenye visibility study!!
 
Back
Top Bottom