Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Katika miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia vijana wengi wakipewa nafasi za juu huko serikalini na katika hutumishi wa umma kwa ujumla. Tofauti na matarajio, kuongezeka huko kwa idadi ya vijana, katika utumishi wa umma, kunaenda sambamba na kuporomoka kwa maadili na weledi katika utendaji kazi. Baadhi yetu tunaihusisha hali hiyo, pamoja na mambo mengine na kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.