Uboreshwaji wa data za wanandoa hasa kwa dini ya Kikristo

Mingendeu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
293
Reaction score
572
Habari..

Kumekuwa na udanganyifu kwenye baadhi ya ndoa za kikristo. Kwa sheria na taratibu zao imeruhusiwa ndoa moja tu. (Nyingine zitafungwa ikiwa mwanandoa mmoja amefariki au ndoa kubatilishwa na kanisa)

Nimeshahudia kesi za watu watatu wakristo, mmoja alifunga ndoa na mwanamke ambaye alishafunga ndoa mkoani Kilimanjaro na baadae kuamia Dar Es Salaam. Mwanamke alidanganya kuwa hakuwahi kuolewa. Baada ya kesi kuunguruma- ndoa ilibatilishwa.

Pia kuna ndoa mbili wanaume wamefunga ndoa mikoani (nje ya dar), baadae wakagundulika kuwa walishafunga ndoa.

Ushauri: ingekuwa vyema swala La ndoa lingewekwa kwenye mtandao. Taarifa za ndoa zingekuwa kama kwenye google sheet ili taarifa ziweze kuonekana katika makanisa. Wachungaji na mapadri wapewe access ya hiyo program ili kuondoa duplicate.
 
Kwenye Kanisa Moja Takatifu Katoliki La Mitume La Kimisionari ni ngumu sana kuwa na ndoa mbili hata uende nje ya nchi.
 
Labda hizo ndoa hazina vyeti. Kama unaoa mama mwenye mtoto ni lazima umuulize aliko baba wa mtoto ili ujiridhishe kama huyo si mke wa mtu
 
Ndugu, mimi pia mkatoliki. Na hizo ndoa nilizozishuhudia ni za kikatoliki. Sisi wakatoliki hatuna database zaidi ya matangazo ya kanisani, mtu anadanganya sehemu alizoishi.

Kama upo karibu na padri yeyote, jaribu kuuliza hili. Jimboni kuna mahakama ya kanisa. Kesi za namna hii, ni nyingi. Na kila siku ndoa zinabatilishwa. Fanya utafiti.
 
Labda hizo ndoa hazina vyeti. Kama unaoa mama mwenye mtoto ni lazima umuulize aliko baba wa mtoto ili ujiridhishe kama huyo si mke wa mtu
Mtu anaweza kukwambia mumewe alifariki, au hakufunga ndoa, alitelekezwa nk

Mwisho wa siku unafunga ndoa then unakuja kusikia alishafunga ndoa. Na kitu kinachosababisha kujulikana hizi ndoa ni pamoja na maMC. MaMC wengi ni maarufu wanafatiliwa na watu wengi, hivyo wanavyorusha zile part huwa zinaenda sanaa
 
Hata kwenye dhamana ya ardhi, mtu anadanganya hajaoa, benki inatoa mkopo
 
Habari..

Kumekuwa na udanganyifu kwenye baadhi ya ndoa za kikristo. Kwa sheria na taratibu zao imeruhusiwa ndoa moja tu. (Nyingine zitafungwa ikiwa mwanandoa mmoja amefariki au ndoa kubatilishwa na kanisa)

Nimeshahudia kesi za watu watatu wakristo, mmoja alifunga ndoa na mwanamke ambaye alishafunga ndoa mkoani Kilimanjaro na baadae kuamia Dar Es Salaam. Mwanamke alidanganya kuwa hakuwahi kuolewa. Baada ya kesi kuunguruma- ndoa ilibatilishwa.

Pia kuna ndoa mbili wanaume wamefunga ndoa mikoani (nje ya dar), baadae wakagundulika kuwa walishafunga ndoa.

Ushauri: ingekuwa vyema swala La ndoa lingewekwa kwenye mtandao. Taarifa za ndoa zingekuwa kama kwenye google sheet ili taarifa ziweze kuonekana katika makanisa. Wachungaji na mapadri wapewe access ya hiyo program ili kuondoa duplicate.

Issue ni official Talaka, kuvunja mkataba, na sio Ukristo au Uongo.
 
kwanza Serikali ingepitisha ndoa ya wake wengi bila kujali dini maana serikali haina dini
Serikali inafungisha hizo ndoa,kwenye cheti cha ndoa(nakala zote mbili) lazima mseme kuwa ni ya mke mmoja au wake wengi
 
Duh,
Hata wanawake??

Ila huwezi kuzuia mtu aliyedhamiria kuongeza "mzigo" kwa kuboresha data.
Atafungia bomani au atasilimu kwa muda
 
unataka uwakomoe madereva wa masafa sio,,coz wameoa kila mkoa
 
Shida suala la TALAKA kwa wakristo ni kipengele. Viongozi wa dini zao hawakubali kusaini fomu ya mgogoro wa ndoa kabisa na wengine hawataki kabisa. Kwa kuwa ndoa ni hiyari ya mtu basi wakati wowote mhusika aruhusiwe kuwa na mtu anayemtaka kwa afya ya akili na mwili wake ila ni kwa watu wazima. Mwanaume usikimbilie kuoa jipange kimaisha kwani ni mzigo kwa mwanaume yeyote
 
Habari..

Kumekuwa na udanganyifu kwenye baadhi ya ndoa za kikristo. Kwa sheria na taratibu zao imeruhusiwa ndoa moja tu. (Nyingine zitafungwa ikiwa mwanandoa mmoja amefariki au ndoa kubatilishwa na kanisa)

Nimeshahudia kesi za watu watatu wakristo, mmoja alifunga ndoa na mwanamke ambaye alishafunga ndoa mkoani Kilimanjaro na baadae kuamia Dar Es Salaam. Mwanamke alidanganya kuwa hakuwahi kuolewa. Baada ya kesi kuunguruma- ndoa ilibatilishwa.

Pia kuna ndoa mbili wanaume wamefunga ndoa mikoani (nje ya dar), baadae wakagundulika kuwa walishafunga ndoa.

Ushauri: ingekuwa vyema swala La ndoa lingewekwa kwenye mtandao. Taarifa za ndoa zingekuwa kama kwenye google sheet ili taarifa ziweze kuonekana katika makanisa. Wachungaji na mapadri wapewe access ya hiyo program ili kuondoa duplicate.
Sheria ya Ndoa inaeleza kuwa mtu unaweza kupata taarifa za kindoa za mtu unayetaka kuoana nae kwa kufanya upekuzi (SEARCH) kwenye ofisi za RITA.

Gharama ya kufanya search ni Tshs. 40,000/= hivi.

Tatizo moja ni kuwa, wafungisha ndoa wengi huwa hawapeleki RITA daftari la usajili wa ndoa walizofungisha ili ziwekwe katika database ya RITA, kwa hiyo kwa sasa limekuwa ni jukumu la mwanandoa mwenyewe kupeleka cheti chake cha ndoa RITA ili kihakikiwe na kuthibitishwa na RITA. Gharama ni Tshs. 50,000/= hivi

Kwa lugha rahisi ni kuwa, kwa sasa hata wenye vyeti vya ndoa na ndoa zao hazina migogoro wanatakiwa waende RITA kuboresha taarifa zao, ndio zitasomeka nchi nzima.

Ushauri:
RITA wawape wafungisha ndoa, sharti la lazima kusajili ndoa kwenye mfumo mara tu baada ya kufungisha (kusajili)
 
Kumbee..hii iko vzr nadhani linatakiwa litiliwe mkazo...
 
Ndiyo. Ukienda na cheti cha ndoa kwenye ofisi za RITA wanakufanyia huo uhakiki na mzigo utakua unatambulika. Kwa sasa nasikia hata baadhi ya huduma, kama bima ya afya wanapomsajili mwanachama mpya hawakubali cheti cha ndoa ambacho hakijahakikiwa.
 
Back
Top Bottom