Ubora wa simu za Tecno dhidi ya Infinix....

Umeua mkuu 🤣
 
Nawaona hapa mnajichanganya kweli kweli kuelezea simu ipi ni bora kuliko nyingine, mnasahau ukweli kuwa simu ni simu tu, iwe ya bei hii au ile, watumiaji wananunua na kuzitumia na kununua nyingine zinapochakaa, kuhangaikahangaika hapa kutoa majibu yote hayo ni kukosa kazi ya kufanya?
 


Hahaha aisee.
 

Mkuu infinix ni nzuri sana. Kwahiyo badget unapata hot 6 nzuri kabisa. Kwanza nilichopendea ni kuwa inakaa na charge hatari. Nilinunua mwaka jana mwezi wa 4. Nimeuza mwaka huu mwezi wa sita na kununua brand nyingine. Ila infinix ipo pouwa hutojuta.


Chakushangaza nilinunua 250000/= mimi nikauza 320000/=

Na hapo nimetumia mwaka mzima
 
Utakuja kuyajua siku ukikutana na kirusi ambacho kita take control ya simu yako hata ukirestore hakitoki kinakuwa part ya system files mpaka u flash simu. Hii ni weaknes ya chip za mtk
Utakuja kuyajua siku ukirestore sim ikapoteza imei nayo ni weakness nyingine
Hata simu za kichina zenye bei mfano brand ya xiomi hawatumii mtk maana wanajua balaa lake hata hao samsung wakizitumia na kwa simu za bei chee sana kama j1 saunakuta mchina anakuuzia simu laki 4 halafu kakuwekea chip ya mtk.
Wewe kwakuwa unaonaina camera kali tena ukweli camera siyo kali bali ina saturate colors unadanganyika kuwa ni sawa na brand flani
 
Lakini hayo mambo ya virus ni moja moja sana... Mbona mi najua watu zaid ya watatu wana tecno .iaka karibu mi 4
 
Infinix ina umbo zuri napia inakaa na charge Muda mrefu tatizo ya izi simu za bei nafuu kadri inavyo kaa Muda ndivyo ubora unazidi kupungua unaweza kushindwa kupokea simu ya maana na unaiona inaita.
Daah umepiga mule mule,natumia CX yan kimeo hatar kama niko wasap au app yoyote halaf nataka kurud home page au nikapigiwa simu,mtihan sana kupokea yan lazma simu ijifikirie zaid ya sekunde 10 ndio itarespond mamamae kweli mchina😬

Nishawah kutumia Tecno, simu miyeyusho kinyama, nilichukua W4, simu ikawa inaganda tuu, kimbembe Ukifungua data walah, inabdi uipe dk 5 kwanza ndo ikuelewe, nikaipush nikanunua l9 daah mtandao ikawa inasoma E mda wote labda uwe town center ndo inasoma angalau H+, nikasema isiwe tabu nikaona ninunue infinix sjui ndo note 3,nikatumia miez 4, simu ikabadirika rangi kioo, ukipiga picha inatoka nyeusi, nikarudi tecno w3 lite, simu ikawa inawaka dk 5, mara ichore mistari, kilichoniudh kuna siku nilikosa dili la pesa ndefu simu imekataa kupokea nikatamani kuibamiza chini, mwisho ikazima yenyewe, siku hyo hyo nilivunja kibubu kwenda kuchukua Samsung....kiufupi tu tecno na infinix ni toy za kuchezea watoto
 
😁😁😁😁daah hayo majanga sana mkuu
 
Narudi tena nikiwa na narrower options, naomba nisaidiwe kufanya uchaguzi sahihi na ikiwezekana na sababu ili kwa bajeti yangu hii ndogo nisijichanganye. Nimefanya reseach kidogo nimekuta simu 3 za brands tofauti ila specifications karibu sawa..

Ninachotaka kutoka kwenu ni uchaguzi (possibly with reasons) ni ipi nzuri zaidi nikanunue kati ya hizi:

1. INFINIX HOT S4
2. SAMSUNG GALAXY A10
3. TECNO POUVOIR 2 PRO

Msinichoke jamani , natamani kizuri, sema uwezo mdogo.
 
Infinix is the best mkuu sihami wallah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…