Makau Js
Member
- May 25, 2017
- 93
- 233
Ubora wa mwanamke upo katika kutunza haiba yake:kuwa na utajiri wa tabia njema na kinywa kitamu cha kunena maneno matamu na ya hekima na busara kwa kila amsikiaye.
Mwanamke mjinga ambaye ni mwerevu hutafutwa na wanaume wajinga ambao ni waerevu kwa dua na maombi, pia husitiri maungo yake kwa mavazi nadhifu na yenye staha.
Ndege wafananao huruka pamoja na siku zote ndege mwenye mabawa hujua mahali mtama unapolimwa.
Ukitaka kupata mke mwema yatakiwa na wewe uwe mwema .Mwenyenzi Mungu ni fundi asiyeishiwa kuumba wanawake :wazuri,bora na watamu kwa waume bora.
Mwanamke anaweza kuvaa nusu uchi na micro-Mini-Skirt na asiwavutie wanaume wajinga na waerevu bali akawavutia wanaume :warafi ,wajuaji na wenya tamaa ya penzi.
Ila mwanamke mjinga na mwerevu anaweza akavaa kwa kujisitiri maungo yake na kuficha ubora wa shape yake ila uzuri na ubora wake ukagunduliwa na wanaume wajinga na waerevu. The most beautiful thing about a person isn’t looks, but heart and personaility.
[HASHTAG]#HaibaYaMwanamke[/HASHTAG].