olimpio
JF-Expert Member
- Apr 5, 2023
- 419
- 867
Nimepitia ripoti ya robo ya pili ya mwaka ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania nimeona TCRA wametujulisha kuhusu kushuka kwa ubora wa mawasiliano ya simu nchini lakini hawajasema wanafanya nini baada ya mawasiliano hayo ubora wake kushuka.
Ripoti imekaa vizuri sana na hawajataka kuficha kitu chochote ,sasa swali linakuja makampuni ya simu kwa nini yanaendelea kunyamazia ubora wa mawasiliano yao kushuka? sio Vodacom , Tigo sijui YAS,Airtel na TTCL.
Ninawashauri TCRA wawapige faini kali mitandao ya simu ili ubora wa mawasiliano urejee kuwa sawa, siku hizi ukipiga simu ukiongea kwa dakika sita ,lazima ukate upige tena kwa nini?
Hii mitandao ya simu isichekewe ,haiwezekani niongee kwa dakika sita then dakika moja simsikii ninayeongea naye ,kuna silent calls nyingi sana.
Ukiangalia Ripoti ya TCRA inaonyesha kila mtoa huduma amepata asilimia zaidi ya 95% ya ubora, kuna haja ya kutofautisha ubora wa kila category ,hapa imejumuishwa sana ,watu wanalalamikia simu za kupiga hazina ubora ,lakini hapa imechanganywa simu na intaneti, nashauri wabadirishe wakitenganisha intanet na simu za kupiga wataona maajabu.