Ubingwa ni Simba na Yanga Tu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubingwa ni Simba na Yanga Tu?

Discussion in 'Sports' started by dazu, Mar 19, 2011.

 1. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni kwa muda mrefu sasa ubingwa wa ligi yetu umekua ukipokezana timu za simba na Yanga tu, na kwa jinsi mwaka huu muelekeo wa ligi unavyoendelea, ni wazi ubingwa utaelekea msimbazi au wakiteleza basi yanga iliyo nafasi ya pili. Timu ya mwisho kuchukua kombe nje ya yanga na simba ni mtibwa zaidi ya miaka 6 iliyopita. Maoni yangu ni kwamba hii imekua ikiua msisimko wa ligi yenyewe, hivyo hata kushindwa kupata timu nzuri ya taifa. Nakumbuka enzi za timu ya pamba ya akina Paul Rwechungura, Hussein Marsha, George Massatu, James Washokera, Fumo Felician, Hamza Mponda, Halfan Ngasa, na wengineo walivyokua wakileta changamoto kwenye ligi; au Reli ya akina Mkali Abdallah, Mbui Yondan, na wengine, ligi ilikua tamu sana na haitabiriki. Je Timu zetu za mikoani zimekua dhaifu sana? Au Simba na Yanga zimekua Strong sana, au kuna uchakachuaji?
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Timu za mikoni hazija jipanga mfano AFC ambayo mpaka sasa ina pointi 11, msimu mzima haina uongozi wa kueleweka....hawana kipato wanategemea pesa ya mlangoni hasa mechi zao Yanga na Simba ndiyo wapate pesa ya kutosha...hakuna wakuyafata makampuni na kuyaomba msaada matokeo yake timu inaenda mikoani inakosa chakula, nauri...Simba na Yanga bado wataendelea kuchukua kombe mpaka tutakapo pata timu zenye uwezo wa kifedha kama Azam FC, kwani kwa muundo wa timu za mikoani kwasasa ni vigumu sana kupambana na Simba na Yanga kwa vyovyote vile yaani kifedha, viwango vya wachezaji kwani timu hizi huchukua wacheza karibu wote wazuri ndani ya Tanzania na hata EA...
   
 3. n

  nyuki dume JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mbona ligi ya Spain ni Bac na R/Madrid kwa miaka mingi wanapokezana,hivyo hatuwezi kulaumu Simba na Yanga ,Timu za mikoani zijipange tu kama miaka ya nyuma ilivyokua Coastal Union,Pamba,african spotrs n.k
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ni ubvu tu wa mfumo mzima wa soka.
  Kuna timu zinakuwaga tishio kwa muda tuu, wachezaji wake waking'ara basi wanakimbilia kuzichezea simba au Yanga.
   
Loading...