Swali kwako mkuu wangu, katika hii trial and error taifa la Tanzania limeingia hasara kiasi gani? Je tukifanya cost benefit analysis ya huu uwekezaji..tukachukua mashirika yote makubwa, je tuko better off leo hii, au ni bora tungeendelea kuyafadhili kwa fedha za Serikali na hivyo kuendelea kulibebesha taifa mzigo mzito wakati tukijifunza kutoka kwa wenzetu Benchmark (nchi zilizofanya ubinafsishaji successfully) na kufanya feasibility studies ya namna ya kuingia kwenye zoezi la ubinafsishaji?wandugu,
..mashirika ya umma yaliuawa na wa-Tanzania wenyewe. matokeo yake yakawa ni mzigo kwa walipa kodi wa Tanzania.
..ubinafsishaji mimi nauchukulia kama TACTICAL RETREAT. kwamba ni hatua ya kurekebisha makosa na kujipanga upya.
..baada ya kuondokana na mzigo wa kutoa ruzuku kwa mashirika ya umma, na kuongeza bidii ktk kukusanya kodi, serikali sasa imeweza kutoa mchango mkubwa zaidi ktk miradi ya maendeleo kwa mfano ujenzi wa barabara.
..kwa upande mwingine sera ya ubinafsishaji siyo "maandiko matakatifu" yanayokataza serikali kuanzisha makampuni ya umma kama itaamua.
..naamini leo hii wa-Tanzania tuna nafasi nzuri zaidi ya kuanzisha makampuni ya umma, na kuyasimamia yasilitie taifa hasara na kuwa mzigo kwa wananchi.
Capital Hill said:Swali kwako mkuu wangu, katika hii trial and error taifa la Tanzania limeingia hasara kiasi gani? Je tukifanya cost benefit analysis ya huu uwekezaji..tukachukua mashirika yote makubwa, je tuko better off leo hii, au ni bora tungeendelea kuyafadhili kwa fedha za Serikali na hivyo kuendelea kulibebesha taifa mzigo mzito wakati tukijifunza kutoka kwa wenzetu Benchmark (nchi zilizofanya ubinafsishaji successfully) na kufanya feasibility studies ya namna ya kuingia kwenye zoezi la ubinafsishaji?
Nafikiri Administration iliyajua haya na these people did not do their homework. Hawakuwa na plan ambayo ilikuwa ni yenye manufaa kwa umma wa waTanzania. Plan yao ilikuwa ni ya wao (wachache) ku get wealthy quickly na kuachia regimes nyingine zije zi clean messy walizoziacha.
Mkandara said:Jokakuu,
Ubinafsishaji wa Mkapa ni sawa na yule Model - Miss Brazil aliyekatwa miguu na mikono kujaribu kumponya lakini matokeo yake amekufa..
Leo hii wataalam wa maradhi yake wanasema hapakuwepo na haja ya kukatwa miguu wala mikono, maradhi yake yaliwezekana kabisa kutibiwa bila kumwondoa viungo!..
Jokakuu,
Ubinafsishaji wa Mkapa ni sawa na yule Model - Miss Brazil aliyekatwa miguu na mikono kujaribu kumponya lakini matokeo yake amekufa..
Leo hii wataalam wa maradhi yake wanasema hapakuwepo na haja ya kukatwa miguu wala mikono, maradhi yake yaliwezekana kabisa kutibiwa bila kumwondoa viungo!..
zamani tulikuwa tunasema "gia ya kuingilia".. naamini hii ni mojawapo.., ya pili itakuwa ni kusikitikia wafanyakazi wa umma kujinufaisha kutokana na nafasi zao na atasikitika sana hawakuweza kusimamia maadili kwani waliamini kila mmoja ni mzalendo..
Pasco ni kweli ni hearsay, lakini tunaweza kufuatilia ili kuhakikisha je, kulikuwa na kikao kilichofanyika Z'bar kilichoandaliwa na UVCCM. Je, Thabo Mbeki hivi karibuni alikuwa Z'bar? kwa shughuli ipi? na je alihudhuria kikao cha UVCCM kilichofanyika Z'bar hivi karibuni? Je, Mkapa alikuwa Z'bar hivi karibuni? kwa shughuli ipi? Tukipata majibu ya maswali hayo ama tunaweza kuukaribia ukweli au kuzidi kuwa mbali nao.
Sasa majina ya baadhi ya waliohudhuria kikao hicho yamewekwa hadharani. Basi ni wajibu wao kukanusha habari hii kama Mkapa hakutamka maneno hayo. Kukaa kwao kimya kuhusiana na habari hii ni ufisadi wa aina yake.
Mkuu Pasco , pamoja na kuwa inawezekana kuwa ni hearsay laikini habari imeandikwa na haijakanushwa.
Lets wait and see.
Hata hivyo inaelekea the sentiments are geunine hata kama hazikuwa for public consumption.
- Mkuu Bob, nimekusikia sana nilichouliza ni kwamba unasema kuna mahali Mwalimu alikubali hadharani mbele yetu wananchi kuwa Ujamaa wake ulishindwa? Alisema exactly that au?
Mkuu Kuhani, heshima mbele.Pasco,
Hiki ki-habari cha TanzaniaDaima ni udaku mtupu. Mkapa ana soo la kubinafsisha mgodi na partner in crime wake Daniel Yona ana kesi mahakamani kuhusiana na haya haya ma hanky-panky ya dealings za serikali na wawekezaji, hawezi kujitia kitanzi kukiri makosa saa hizi.
Sio principle za journalism tu, hata za stori za mtaani haziendi hivyo. Hivi tukiwa tunamtafuta Juma atujibu kuhusu mali zetu halafu tunakuja kuambiwa kuna fulani kasema Juma kakiri kosa, hatutataka kujua huyo fulani anaesema Juma katubu ni nani, na nani mwingine alisikia wakati anatubu? Halafu alipokubali makosa alisema nini kuhusu mali zetu going forward? You know?
Halafu ki-habari kina misrepresent ukweli kwa kusema pressure ya kumshitaki Mkapa imeongezeka. Kila kukicha tunasikia padri so and so mbunge huyu na yule wanasema let this Mkapa character alone, sasa hiyo pressure iko wapi? Na Pinda keshapayuka kwamba it's a complicated process.
Kinga yenyewe walivyoiongelea ni misrepresentation tupu. Hakuna sehemu kwenye Katiba paliposema Wabunge wanaweza kuondoa kinga. Itabidili Wabunge waandike kipengele hicho cha Katiba upya, na hiyo ndio itahitaji theluthi mbili za wabunge, tena inabidi ipatikane kote Zanzibar na Bara separately.
Halafu Pasco, notice kwamba kwenye misingi journalism, ilibidi pale kwenye paragraph ya kwanza, au ya pili at the latest, waseme kwamba wanaripoti based on stori ya kuambiwa na anonymous source. Walivyoiweka ni kama wao Tanzania Daima ndio wanaripoti wakati hawana uhakika. Wakishitakiwa watasema sisi tumeambiwa na mtu, lakini hapa wameitengeneza kuwa-fool unwary readers kama wana uhakika vile. Wadaku.
Halafu, notice vi-taarifa ambavyo hawana uhakika hawatoi jina la mwandishi, wanavunja cardinal rule of journalism, inayotakiwa kuleta credibility na accontability.
Eti gazeti linaripoti kwa kuambiwa na mjumbe mmoja, udaku, uzushi, vilaza wakutupwa nje ya press room.
Mwalimu alikubali makosa alipotangaza Azimio la Arusha alisema itatuchukua miaka 30 kuujenga ujamaa. Baada ya miaka 20 akakubali tulikosea, akasema itachukua muda mrefu kuujenga ujamaa, hata hivyo akasisitiza, kuna makosa mengi tumefanya huko nyuma ila nanukuu"Kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa". Mwisho wa kunukuu.Kwenye hotuba/press conference,sikumbuki katika tukio gani nyerere alisema 'tulifanya makosa,tulifanya makosa,hatukuwa malaika sisi,tulichukua nchi tukiwa na wasomi wachache,kama kitoto kilichotupwa baharini kinatapatapa,hakina msaada...lakini sasa hawa wenzetu wanaacha kuendeleza yale mazuri tuliyoyafanya wanachukua mabaya..'
Halafu aliulizwa sikumbuki kama na BBC au la na sikumbuki vizuri swali lilikuwaje lakini muulizaji alitaka kujua kama nyerere angeweza kurudi tena na kuongoza tanzania,nyerere akasema kama alishindwa na ujamaa wake kwa miaka zaidi ya ishirini itakuwa wakati huu wa kuongoza kwa vipindi vya miaka mitano mitano..
Kitu kama hicho.Wanaokumbuka vizuri watatufahamisha.