ANKO JEI
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 1,278
- 2,364
Kwa jinsi nilivyo na haraka nikusalimu kifupi tu, Uhali gani?
Baada ya kukaa kuwaza nimekuja kujua wengi wetu ni wabinafsi sana, na wengine hata hatujui kuwa tunachofanya ni ubinafsi wa kutisha.
Wewe unajiona kabisa una familia au niseme mtoto ili uelewe vizuri, ila still una mawazo mgando ya kushikilia hako kaajira kako, miaka inaenda huwazii hawa watoto wako itakuaje, na unajua kuwa wewe mwenyewe ulipata hiyo kazi kwa bahati nasibu tu kama sio kuhonga na kuna asilimia kubwa ni kazi ambayo huwezi kumrithisha mwanao.
Badala uwaze kufanya jambo ambalo litawaandalia watoto wako future nzuri, we umetulia tu unawaza kutembea na wake za watu hapo ofisini. Tengeneza connection ambazo watoto wako hawatakuja pata tabu bro! asikudanganye mtu connection zitakuja isha, yani kwajinsi dunia ilivyochafuka nadhani hapo baadae bila connection huwezi pata kazi.
Usikute una mtoto wakike lakini hata huwazi kuanza kumuandalia mazingira yake akisoma asije pata tabu kupata kazi au kujiajiri, we kazi yako kumpeleka mlimani city akachorwe kama spiderman na kula ice cream, sisemi ni vibaya lakini usijipige kifua kuona ndo umemaliza jukumu lako, huyo mtoto atakua mkubwa atakua na chura atavutia wanaume humo maofisini, bro atatafunwa sana ili kupata kazi.
Ishi na watu vizuri kununua gari haimaanishi majirani zako hawana juhudi za maisha, ukiishi nawatu vizuri hao watoto wako au familia yako itafurahi baadae,watasaidiwa na watu wasio wajua kwasababu uliishi nao vizuri.Kuna watu leo wanaogopa hata kutumia bini zao kutokana na upuuzi wa wazazi wao miaka ya nyuma, na kuna watu akitaja ubini tu ataulizwa baba ako ni yupi.
Usijiwazie wewe tu ndugu yangu, kuna kizazi kinasubiri kuja kufurahia maajabu uliyofanya ukiwa hai.
Ni hayo tu.
Anko Jei