Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,914
Kila mmoja wetu ameshawahi kusiki kuwa mtu fulani anamuoa/olea na mwingine kwa madai kuwa wanapendana au anampenda huyo anaeingia nae kwenye ndoa,madai haya yapo na huenda hata wewe unafikiri hivyo hivyo.
Leo nataka nikupe ushahidi kuwa sio kweli kuwa watu wanaoana kwasababu ya kupendana au kupenda bali ni kwasababu ya ubinafsi tu ni vigumu sana kusema kuna watu ambao wanaoana kwasababu wanapendana au mmoja kumpenda mwenzake,hili linatokana na mfumo wa kimaisha tulio nao leo pamoja na wengi kutokujua hata upendo ni kitu gani.
Kupenda kuna maana ya kumkubali mwenzako bila masharti ikiwa ni pamoja na kujitoa kwaajili ya furaha yake na sio furaha yako, sasa tukija kwenye suala la ndoa na mahusiano kwa ujumla wake mara nyingi watu wanaingia kwenye uhusiano na wale ambao wanajisikia raha kuwa nao karibu au kwa kifupi wanahisia chanya nao.
Watu hawa wamejikuta wakisema kwamba wanawapenda wahusika hivyo kufanya jitihada za kuingia ndoani na wahusika na wamekuwa wakitamani hata kufa pale ambapo wanashindwa kuingia kwenye ndoa na wahusika,lakini je kwa tafsiri hiyo hapo juu ni kweli kwamba watu hawa wanaongozwa na upendo kutamani kuingia kwenye ndoa au kuna kitu kingine?
Ukweli mchungu ni kwamba hawaongozwi na upendo bali ubinafsi,nasema hivi kwasababu kinachomuongoza mtu kuingia ndoani ni zile hisia zake yeye kwa mhusika na sio hisia za mhusika kwake yeye, yaani iko hivi, wewe unapokutana na mtu halafu ukajisikia amani na furaha kuwa karibu yake utasema unampenda na utataka uendelee kuwa nae.
Karibu maisha yako yote ili uendelee kujisikia vizuri na sio mwenzako kujisikia vizuri, hapoa wala hutajali mwenzako anajisikiaje kwasababu tu wewe unajisikia vizuri unapokuwa nae utataka akuoe au umuoe,huu ni ubinafsi,yaani unajifikiria wewe tu na unaingia humo kwenye ndoa kwasababu wewe unajisikia vizuri na sio mwenzako
Hata wale ambao wanasema wanapendana,yaani wanakutana watu wawili ambao wote wanajisikia vizuri pale ambapo wanakuwa pamoja,hawa nao wanapoingia kwenye ndoa sio kwasababu wanapendana bali ni kwasababu kila mmoja anajisikia vizuri anapokuwa na mwenzake,hii ina maana kwamba kila mmoja anaongozwa na yeye kujisikia vizuri kwa mwenzake na sio kuongozwa na hisia za mwenzake kwake
Kama kweli tungekuwa tunaomngozwa na upendo basi tungeolewa au kuoa wale ambao wao tu wanajisikia vizuri kuwa na sisi,hii inamaana kwamba tunajitoa kwaajili ya furaha za wengine kama maana ya kupenda ilivyo,yaani uende kuoa au kumuoa yule ambae wewe huna hisia chanya nae lakini yeye anazo hisia chanya kwako hapo utakuwa umempenda na kuongozwa na upendo kuingia kwenye ndoa.
Ukweli huu mchungu ni mgumu kukubaliwa na wengi, kwasababu tumeaminishwa kuwa upendo ni wa aina fulani wakati sio kweli. Je wewe ni mmoja wa wale wanaoongozwa na ubinafsi au hapana?