Ubepari utakufa duniani, tusiusogelee.

Ubepari utakufa duniani, tusiusogelee.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,176
Reaction score
17,511
Huwezi kumiliki utajiri mwingi katikati ya watu wengi masikini ukabaki salama. Ni swala la muda tu iko siku watakunyang'anya kutegemea na hali yao itakavyoendelea kuwa bora au mbaya zaidi. Kama hali ya wengi kiuchumi itaendelea kuboreka watakuheshimu kwa utajiri wako, lakini kama hali zao zikizidi kuwa mbaya utajiri wako utageuka kuwa laana kwako. Utakosa usingizi, watauchukua na wanaweza kukuua pia. Maana njaa haizoeleki hata kidogo.

Wananchi wa nchi za Magharibi sasa wameanza kuuona ubaya wa ubepari, hawataki tena haki, demokrasia na uhuru wa kutukana, bali wanataka haki ya kula chakula, matibabu, elimu, malazi na malipo ya haki kwa wote.

Wananchi wa Magharibi wameshaanza kuwapora mali na kuwanyima kura matajiri na wanaokumbatia ubepari mkali. Wameshaanza kutamani mifumo ya kijamaa kama ile ya Uchina, Urusi, Korea, Tanzania, Cuba na Ulaya mashariki ambako hakuna anaekosa mahali pa kulala, chakula, elimu, matibabu, na mavazi hata kama ni maskini wa kutupwa.

Nyerere na Karume walikuwa na maono ya kutoka kwa Mungu moja kwa moja kuuchagua ujamaa na kujitegemea. Hata kama tunaona Tanzania tuna amani na utulivu kidogo kuliko mataifa mengine Afrika basi ni kutokana na ujamaa na kujitegemea. Mfumo ambao unamhakikishia kila mtu kupata ardhi, chakula, elimu, matibabu, malazi, mavazi na usafiri kwa bei nafuu. Ardhi ni mali ya serikali hivyo kila mtu yuko huru kwenda kupata ardhi na kuishi kokote ilimradi tu asivunje sheria na taratibu za nchi na za kule anakohamia.

Vyama vyote vya siasa vinavyotaka kubadilishana na CCM katika kuiongoza nchi hii lazima viikubali misingi waliyoiacha Nyerere na Karume. Vingine wananchi wataipatia baraka zote CCM kuvizuia kwenda Ikulu hata ikibidi kwa kutumia nguvu vyama vyote vinavyohisi Nyerere na Karume walikosea sana kutujengea mfumo huu wa ujamaa na kujitegema, aina ya muungano, utawala wa mikoa na umiliki wa ardhi. Vyama vya siasa vishindane kwenye mambo mengine lakini sio kwenye hii misingi.

Sisi watanzania lazima tuwe wakali na ikibidi kumkemea na muondoa kiongozi wa umma aliyejilimbikizia mali; tuzichukue na kuzirejesha kwa umma mali hizo.

View: https://youtu.be/d_jI6d9LsXo?si=-hZ5pSka6150ScOD
 
View: https://www.youtube.com/live/VESe5ZcwP5c?si=Zy8Xp2ZwbiHoTtGN

Tatizo si kuwa na utajiri, bali ni namna utajiri huo unavyopatikana na kutumika. Ubepari usio na mipaka una mapungufu yake, lakini pia ujamaa hauwezi kuwa suluhisho la kila tatizo. Taifa linahitaji haki, fursa sawa, uwajibikaji na mfumo unaompa kila mtu nafasi ya kujikwamua kiuchumi. Tusipambane na utajiri, tupambane na umasikini na mifumo inayozalisha dhuluma.
 
Bila katiba mpya hiyo nguvu ya kuwabananisha mafisadi nani anayo?
Hapo nakukubalia, katiba yetu inakosa kipengele cha kumwadhibu vikali aliyekula rushwa na kutumia vibaya rasilimali za umma kwa manufaa yake.. Hicho ni kipengele muhimu kwenye ujamaa na kujitegemea.
 
Una maana Tanzania ya kina Kikwete, Samia, Rostam, Mo, SSB, nk ni ya kijamaa?
 
Huwezi kumiliki utajiri mwingi katikati ya watu wengi masikini ukabaki salama. Ni swala la muda tu iko siku watakunyang'anya kutegemea na hali yao itakavyoendelea kuwa bora au mbaya zaidi. Kama hali ya wengi kiuchumi itaendelea kuboreka watakuheshimu kwa utajiri wako, lakini kama hali zao zikizidi kuwa mbaya utajiri wako utageuka kuwa laana kwako. Utakosa usingizi, watauchukua na wanaweza kukuua pia. Maana njaa haizoeleki hata kidogo.

Wananchi wa nchi za Magharibi sasa wameanza kuuona ubaya wa ubepari, hawataki tena haki, demokrasia na uhuru wa kutukana, bali wanataka haki ya kula chakula, matibabu, elimu, malazi na malipo ya haki kwa wote.

Wananchi wa Magharibi wameshaanza kuwapora mali na kuwanyima kura matajiri na wanaokumbatia ubepari mkali. Wameshaanza kutamani mifumo ya kijamaa kama ile ya Uchina, Urusi, Korea, Tanzania, Cuba na Ulaya mashariki ambako hakuna anaekosa mahali pa kulala, chakula, elimu, matibabu, na mavazi hata kama ni maskini wa kutupwa.

Nyerere na Karume walikuwa na maono ya kutoka kwa Mungu moja kwa moja kuuchagua ujamaa na kujitegemea. Hata kama tunaona Tanzania tuna amani na utulivu kidogo kuliko mataifa mengine Afrika basi ni kutokana na ujamaa na kujitegemea. Mfumo ambao unamhakikishia kila mtu kupata ardhi, chakula, elimu, matibabu, malazi, mavazi na usafiri kwa bei nafuu. Ardhi ni mali ya serikali hivyo kila mtu yuko huru kwenda kupata ardhi na kuishi kokote ilimradi tu asivunje sheria na taratibu za nchi na za kule anakohamia.

Vyama vyote vya siasa vinavyotaka kubadilishana na CCM katika kuiongoza nchi hii lazima viikubali misingi waliyoiacha Nyerere na Karume. Vingine wananchi wataipatia baraka zote CCM kuvizuia kwenda Ikulu hata ikibidi kwa kutumia nguvu vyama vyote vinavyohisi Nyerere na Karume walikosea sana kutujengea mfumo huu wa ujamaa na kujitegema, aina ya muungano, utawala wa mikoa na umiliki wa ardhi. Vyama vya siasa vishindane kwenye mambo mengine lakini sio kwenye hii misingi.

Sisi watanzania lazima tuwe wakali na ikibidi kumkemea na muondoa kiongozi wa umma aliyejilimbikizia mali; tuzichukue na kuzirejesha kwa umma mali hizo.

View: https://youtu.be/d_jI6d9LsXo?si=-hZ5pSka6150ScOD

Acha kutisha watu mkuu.
Yaani pesa ya kwangu then nipate laana Kwasababu ya watu kuwa maskini Sasa Kwani Mimi ndy nimewapatia huo umaskini?
Kama mungu ndy anae toa utajiri na yeye ndy anaetoa umaskini Sasa shida Iko wapi hapo ya wao kuwa maskini?
 
Back
Top Bottom