Ubaya wa kushiba kabla ya karamu.. Ama kulewa

Ubaya wa kushiba kabla ya karamu.. Ama kulewa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
375,728
Reaction score
870,463
Nina mifano mingi.. Lakini kuwa na subra na kufuata utaratibu daima humpa mtu matokeo bora tena kwa wivu mkubwa Sana
Subiri wakati sahihi ufike ndio ufanye jambo lako kwa utaratibu uliowekwa.. Utajikuta unapewa maua yako bila hata kutarajia

Kuna matukio ya suprise..hayapaswi kujulikana na wahusika kabla ya muda wake kutimia.. Maana yatakosa ladha na yatakosa mvuto

Ni sawa na binti kigori siku ya ndoa
Sawa na zawadi ya birthday siku ya kuzaliwa
Sawa na engagement ring siku ya kuchumbiwa rasmi
Sawa na first date.. Kwa mwali aliyekusumbua Sana

Magari yale ya gia.. Dereva anapopanda mlima huanza na gia ndogo ili gia kubwa ndio imalizie kazi
Kwenye vita majeshi mahiri ya mtaa kwa mtaa huwekwa mwishoni pamoja na zile silaha bora kabisa
Kwenye kutongoza hufunguki yote siku ya kwanza.. Kuna verse utazitumia mwishoni kama silaha ya mwisho
Nguo mpya hufichwa mpaka siku ya shughuli

Wavimba macho wana karamu ya vyakula 12 ( twelve dishes ceremony) wanaanzaga na vya kawaida halafu vile vitamu sana huja mwishoni.. Ukiwa mroho utashiba round ya tano. Kisha vitamu zaidi vikija huna pa kuviweka!
Kwanini natoa mifano yote hii.. Wenzetu wameshalala usingizi wote sass wanakesha na kukodoa macho tu kama bundi

Mapicha picha yamechapishwa mpaka kwenye leso na kusambazwa kila kona ya kaya.. Sijui wamebakisha nini huko.. Wameshatumia kila aina ya kisingizio kufanya kampeni za kabla ya muda.. Sasa hawana cha kuonesha tena wala cha kusema!
Cha wizi ni kitamu sana lakini kisiwe mazoea.. Usiruhusu adui ajue mbinu zako zote kabla ya muda sahihi kutimia

Ukiwa hivyo umeshamaliza kila kitu
Huna hoja tena
Huna cha kuonesha tena
Huna cha kusema tena... Ni lazima utapata hofu ya mshindani wako na hapo utaingiwa na hisia mbaya za kumfanyia figisu ili asifike karamuni
Lakini kwenye kufanya hivyo utafanya makosa mengi kutokana na uchovu kuvimbiwa na kulewa mapema

Na ndipo hapo mshindani wako ataku surprise na pigo moja tu la maana nawe utaanguka chini puuu! Usiweze kusimama tena!

Alamsiki Tanganyika💗💗
1747499646648.jpg
 
Bandiko lako nimelielewa sana Mkurugenzi....

Unaweza kushiba mchuzi kumbe Kuna sinia la rosti kuku linakuja au (Mbuzi Katoliki kwa tunaoipenda).... Ukaishia kula kwa Macho wakati wenzio ndo wanasosomola vitamu....

.....Andiko muhimu sana hili.....
 
Bandiko lako nimelielewa sana Mkurugenzi....

Unaweza kushiba mchuzi kumbe Kuna sinia la rosti kuku linakuja au (Mbuzi Katoliki kwa tunaoipenda).... Ukaishia kula kwa Macho wakati wenzio ndo wanasosomola vitamu....

.....Andiko muhimu sana hili.....
❤❤❤💪🏿
 
Bandiko lako nimelielewa sana Mkurugenzi....

Unaweza kushiba mchuzi kumbe Kuna sinia la rosti kuku linakuja au (Mbuzi Katoliki kwa tunaoipenda).... Ukaishia kula kwa Macho wakati wenzio ndo wanasosomola vitamu....

.....Andiko muhimu sana hili.....
Watajitapisha ili kupata nafasi ya kuweka vilivyo kuja baadae, kama kuteka, Kununua wapinzani
 
Mfa maji hutapatapa badala ya kuwekeza kwenye kuleta maendeleo waliwekeza kwenye upigaji wakidhani watanganyika ni mburula hawatang'amua sasa imekuwa kinyume mambo ni magumu upande wao.
Waliona mgombea wao hakubaliki wakaja na mbinu za kumtangaza kila mahali bila kujua kuwa WA VIWANGO HAHITAJI BANGO
 
AY ameweka wazi kuwa wazo la Samia Kings lilikuja kwaajili ya kumsupport Rais Dr. Samia Suluhu Hassan na aliyekuja na hilo jina ni Chege, na anafanya kama mtu aliyeamua kuunga juhudi za Mh. Rais.

Mbali na hilo, AY pia amedai kinacho fanywa na Samia Kings, hakifanyiki bure, hata kama ni Support, wanalipwa kufanya hivyo kama ambavyo watu wa matangazo na stage wanavyolipwa kwenye kampeni hizo.

AY ni moja ya wasanii ambao mitandao iliripuka kuona ameingia kwenye mambo ya siasa na akichagua upande wa Chama Tawala, hili lilikuja kwasababu msanii huyo ambaye mwaka huu anatimiza miaka 25 kwenye muziki, hakuwahi kuonekana kwenye jukwaa lolote la siasa huko nyuma na watu wakiamini pesa imehamisha jabali mahali pake.

AY amefunguka haya kwenye Jahazi HD la Clouds FM.
1748042166905.jpg
 
Back
Top Bottom