Ubalozi wa Tanzania Washington DC boresheni mfumo wenu

Somi

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
3,605
4,360
Imenisikitisha Sana Kuna mgeni wangu aliomba visa ubalozini Washington dc imemchukua zaidi ya wiki mbili kurudishiwa passport yake yenye visa.
Ilibidi amwombe msaada afisa ubalozi WA nchi ya kiafrika kwenda kuwaona watu WA ubalozi WA Tanzania kuuliza kulikoni ndiyo ufumbuzi ukapatikana.

Yeye hakai Washington alitumia courier services.
simu zote za ubalozini hazipokelewi na mfanyakazi yoyote ni answering machine inajibu tuu.
Matokeo yake ameahirisha safari.
Anasema nchi nyingine za kiafrika ndani ya siku tatu passport inarudi na visa.
Kwa hali hii tutapoteza watalii na wafanyabiashara.
Ushauri wekeni mtu maalumu WA kushugulika na kupokea simu na kupeleka tatizo kwa mfanyakazi husika kwa utatuzi.

Ongezeni kasi ya ufanyaji kazi na umakini.
Nafahamu wapo wafanyakazi makini lakini hao wazembe waliopo acheni uzembe fanyeni kazi
 
Hiyo inatokea sana kwenye balozi zetu,hata mm rafiki zangu wengi hulalamika wanapoomba Visa ya Tz kupitia ubalozi wa Moscow,Russia.
Wanasubiria muda mwingi sana.
Kama tunataka kupata watalii wengi,nashauri balozi zetu zifanye kazi kwa haraka na pia waruhusu nchi nyingi wapate Visa upon arrival.
 
Imenisikitisha Sana Kuna mgeni wangu aliomba visa ubalozini Washington dc imemchukua zaidi ya wiki mbili kurudishiwa passport yake yenye visa.
Ilibidi amwombe msaada afisa ubalozi WA nchi ya kiafrika kwenda kuwaona watu WA ubalozi WA Tanzania kuuliza kulikoni ndiyo ufumbuzi ukapatikana.

Yeye hakai Washington alitumia courier services.
simu zote za ubalozini hazipokelewi na mfanyakazi yoyote ni answering machine inajibu tuu.
Matokeo yake ameahirisha safari.
Anasema nchi nyingine za kiafrika ndani ya siku tatu passport inarudi na visa.
Kwa hali hii tutapoteza watalii na wafanyabiashara.
Ushauri wekeni mtu maalumu WA kushugulika na kupokea simu na kupeleka tatizo kwa mfanyakazi husika kwa utatuzi.

Ongezeni kasi ya ufanyaji kazi na umakini.
Nafahamu wapo wafanyakazi makini lakini hao wazembe waliopo acheni uzembe fanyeni kazi
Balozi nyingi ziko namna hii. Ila kwa awamu hii wataanyooka tu hasa kama tutakuwa tunatoa malalamiko hadharani bila kuficha.
 
Back
Top Bottom