Hatua nilizopitia mpaka kufika Ukraine, na bado niko njiani kwenda nchi ya ahadi Norway

kyaibumba

JF-Expert Member
Sep 8, 2017
715
989
Hello wakuu habari za siku mbili tatu,

Jamani mimi ni kijana Mtanzania ambaye nimekulia Tanzania, nimesomea shule zote Tanzania mpaka elimu ya chuo kikuu.

Kwa bahati mbaya sikumaliza mwaka wangu wa mwishoni wa chuo kikuu kutokana na tatizo la ada maana mimi ni miongoni mwa vijana ambao hatukupata mkopo na wazazi wangu ni masikini sana uko vijijini.

Niliishia mwaka wa tatu semester ya kwanza ikabidi niandike barua ya kuomba kupewa HIGHER DIPOLMA IN CORPORATE FINANCE NTA level 7 badala ya Bachelor degree NTA level 8.

Maana kwa hatua hiyo nimeshavuka kigezo cha Ordinary Diploma, ila sijafika bachelor level kati kati ya NTA LEVEL SIX NA NTA LEVEL 8,
mliosoma vyuo kama IFM, IAA, Nairobi university, na Makerere mnajua utaratibu huo.


BAADA YA KUACHA CHUO NA KUPEWA HIGHER DIPLOMA YANGU

Nilisaka ajira kwa udi na uvumba nikapata kampuni moja ya wahindi wanauza pikipiki Kingshen, wakawa wananilipa 400,000 kwa mwezi kama msimamizi wa mauzo na kuandaa report zao, pale bapo hela sikuifaidi niliitumia yote kuwasomesha wadogo zangu , nikawa naishi maisha magumu mnoo.

Ila nikafanya nao mwaka mmoja nikapata kazi ya Sales executive Access bank, nikakaa hapo kanshahara ni 520,000 tu Ila nikawa nakula commission kwa wateja na wengine wakipata mkopo wananihurumia wananipa hata 50,000 kama zawadi ya kuwafanyia vema.

Access mkataba ulikuwa miezi sita ukaisha sikurenew, nikaomba kwengineko wapi maisha yakawa magumu mno, nikaamua kukokaa sana nikakaa nikawa mtu wa kukopa kila mahali, maduka yote yakanijua mkopaji.

Wazazi wakashindwa kuwalipia wadogo zangu nikaamua kuwashauri waachane na vyuo kwanza wakakubaliana na mimi.

Mafao yangu yakatoka milioni 2 tu yaan nikaamua ninunue kiwanja Mwasonga Kigamboni, nikapata kwa milion 1.5 kipindi hicho ila kikubwa, nikatumia shillings laki 2 nikaendelea kusaka ajira saa nyingine nikawapa watu hela ya maji wakanidanganya kuna mtu mmoja ni mfanyakazi wa insurance moja alikula 400,000 yangu akanidanganya kuniunganisha kazi bandarini wapi.

Nikakaa nikatafakari nikaja na jibu kwamba yawezekana maisha mazuri hayako Tanzania ngoja nijaribu nje.

Mwaka 2015

Nikapita sehemu nikakuta kuna watu wanasema visa za Dubai, lilikuwa Tangazo, mwanaume nikawauliza wakasema visa ni laki 3 ya miezi mitatu, ila kwakuwa wewe hatukujui tutakupa ya wiki mbili, nikasema sawa, nikadhani Dubai ni kama Morogoro unaenda tu unafika unaanza kutafuta kazi, kumbe kuna hata muda unaoruhusiwa kukaa kwenye visa, sikuwa najua neno overstay wala nini, nikaenda Kigamboni nikauza shamba langu kwa milion 2.8 lilikiwa nimeshapataga value, nikapata visa 150 USD na hela ya ticket 400 USD Emirates lilikuwa msimu wa punguzo wa ramadhani, nikapanda mpaka Dubai , hapo sijui mtu yeyote uko naenda tu.

Nikafika nikapata hotel nikalala siku moja alafu nikaamua kusaka chumba cha kupanga, aisee kumbe hakuna chumba cha kupanga wana Bed spaces mnashare rooms, ni AED 500 Sawa na laki 3 ya Tanzania kwa mwezi, hela yangu ilikuwa ndogo sana nikalipa week mbili nkidhani kwamba nitapata kazi mapema nihame, week mbili zikaisha na visa ya week mbili inaisha hakuna kazi nilipata ilikuwa ni ni presha mno.

Agent aliyenikatia Visa akaanza kunipigia na vitisho juu akaanza kulaumu kwamba una overstay nimefungiwa visa mpya nazo apply.

Hapo tarehe ya ndege ya kurudi ishapita sina nauli ya kurudi Tanzania, nikafikiria nifany e nini, nikaanza kusaka kazi ndani ya overstay days, nikapata kazi moja ya mauzo kampuni ya Alhairay Printing services.

Nikawapa makaratasi yangu yote wakaenda kuapply work permit ikabounse maana nilikuwa kwenye overstay fines, wakasema hatuwezi kukuajili wewe uko kwenye overstay.

Mzee mmoja wa Pakistan akasema nitakusaidia akanilipia nauli nirudi Tanzania ila nikamuomba kwamba naomba unilipie niende Rwanda maana Tanzania wale ma agent walisema wamefungua kesi kesi niwalipe fidia za kukosesha kazi zao kwa u overstay miez miwili na nusu.

Lakini suala ni kwamba airport lazima ulipe fine.

Kwa kila siku unayozidisha ni 100 AED Sawa na 60,000 ya Tanzania na hapo nishaoverstay karibia siku 80, na sina kitu ilibidi nilipe kama milioni 3 ya Tanzania,

Nikajitosa kwamba naenda hivo hivo, nikafika airport wakanizuia kwamba nilipe fine au niende ku surrender wanajifungu watu wanifunge miezi Mitatu kama sina faini dahhhhhhh!


Naendelea Chini hapa sasa

NIKAAMUA KUFANYA YAFUATAYO
Nikausaka ubalozi wa Tanzania ulipo,nikaambiwa nipande basi ni AED 25 mpaka Abu Dhabi ndo ubalozi wa Tanzania ulipo, nikaenda ubalozini sikupata majibu mazuri nikaambiwa na wahudumu wa pale nikutane na mheshimiwa mmoja, nikaeleza, huyo Afisa akanijibu nenda ukafungwe maana mkianza safari zenu hamutuhusishi mkipata matatizo mnakuja, hatuna jinsi ya kukusaidia nenda kafungwe wapo watanzania wengi wamefungwa humo magerezani.

Kwakweli nilisononeka.
Akili hukumu ya kiçhwa ukilemaa utaachwa feri nikaitumia akili hiyo.

Nikachukua yake makaratasi yangu ambavyo walinisainisha kwamba nimepata nikachukua maform ya kuapply permit nilojaza na waliyonirejeshea baada ya kuteject nikatudi zangu Dubai baada ya kufika Dubai nikamtafta yule Mzee mpakistani nikasema wamenikatalia akanipa AED 1000 Sawa na laki 6 za Tanzania, kwamba zinisaidie kwenye kula wakati akitafta ufumbuzi,
maana wangeniajili ila hakujua sheria vema alidhani hata ukilipa faini huwezi ajiriwa tena ukisha overstay, hata permit haiwezekani toka.

Nikashika makatasi yangu nikaenda Al weel ni ofisi za uhamiaji za Dubai na kuna gereza kubwa hapo ni nje kidogo ya mji, nikashika tax nikapata nikamuelekeza dereva kwamba naenda Al weel akashtuka nikamwambia niko kwenye overstay nataka kuondoka akasema unaenda kufungwa wewe dah akanikatisha tamaa sana, nikasema sawa basi mimi ngoja niende liwalo na liwe.

Nlipofika nikanyoosha maelezo vema kwamba mimi ni fulani nimepata kazi lakini permit yangu haitoki nimepewa mkataba zamani na ilivyokataa naomba mniruhusu niende nyumbani maana naendelea kukaa kwenye overstay na faini sitaweza.

Nikaona wakasema kaa hapo kwenye kiti leta passport yako wakagonga muhuri mwekundu, kati kati na wakasema angalia kwenye machine hii, wakascan macho yangu baada ya hapo kadada kamoja kakasema you and Dubai krasss means ndo basi hautakanyaga tena, wakaniruhusu kuondoka.

Nikasema potelea mbali nikaenda kurebook tena kwa kusema ndege iliniacha hivo wakanitoza dillsdo 50 basi nikakata tikecket mpaka Kigali Rwanda.

Maisha ndani ya Rwanda sasa inaendelea;



Nikafika Rwanda Kigali nikaanza kusaka ajira nikapata jamaa mmoja anaitwa David Aloboza akanipa kazi ya kusaidiana naye kuchomelea vyuma ananipa hela ya kula tu na kulala, nikasema sasa nikope sehemu hela, mjomba wangu akanikopesha 1.6 milioni nikapiga nyumbani wakauza shamba moja hivi nikawa na milion 3.

Nikaanza kusema naelekea wapi maana Afrika sipataki.

Nijaribu visa sehemu mbali mbali wanagoma wanangoma, nikatafuta nchi ambazo tunaenda bila visa mwanaume nikalipa nauli kwenda Malaysia
Kufika uko wakanikatalia kuingia kwamba sikidhi vigezo;
1. Sina barua ya mwaliko
2. Sina hela ambayo ni 1000 USD kama private visitor ya ku declear pale aiporat maana nilikuwa na dollars 400 tu mfukoni

3. Sina pa kulala sijabook hotel

4. Sina kazi yaani barua ya kuonesha nikiingia Malaysia sitabaki

Wakachukua passport yangu waka stamp entry denied wakanipa karatasi inayoonesha sababu za kuzuiliwa entry,

Nikapelekwa chumba cha wanaosafiri kurudishwa kwao,

Nikavua viatu na begi unakabidhi, nikatulia nikakosa tumaini lolote lile,

Nikawa napewa chakula na chai na sabuni za kuoga dawa ya Meno na mswaki daily

Nikahakikikisha naangalia TV kupoteza mawazo,

Sasa wale Qatar airways waliokuwa nimeenda nao wakasema nilipe 100 USD kubadilisha ile tarehe ya kurudi ili iwe karibu nirud mapema au nisubiri tarehe yangu ifike, yaani mwezi upite niko pale nikagoma wakasema haya twende wakanipeleka ila nikapigiwa mahesabu ya gharama nilizotumia wakakata kwenye hela niliyodeclear airport.

Kuingia room tunapopaki mizigo nikakuta begi langu dogo wale wa Nigeria walionitagulia kuondoka wamepita nalo aisee.

Hata simu na kilaptop changu cha CV na kuapply kazi wamesepa nacho, nikasema siondoki mpaka nivipate, wale qatar airways wakasema tunakuacha sisi.

Ikabidi nikubali nikapanda ndege ndani ya ndege watu wanapokuwa deported haukai siti mchanganyiko na wengine unakaa nyuma kabisa karibu na wale cabin crew, hapo nilichofanya nikawa nina mawazo, nimevaa kandambili maana nilipewa pale Kuala Lumpur baada ya wanaigeria kuiba hata viatu vyangu.

Akaja Mwarabu mmoja kukaa karibu na mimi tumbo lilikuwa linamsumbua sana akakaa karibu nilipo maana ni karibu na chooni, bwana huyo tukae marafiki nikampa mkasa mzima akanipa namba jina lake anaitwa HASSAN wa Iran, yeye alishukia doha mimi nikakonect nikashushwa kigali, baada ya kufika.

Nikaamua niende Tanzania kwetu, nikakaa hapo.

Mara paap nikaona simu ya Hasan kupitia kwa simu ya baba yangu nilimpa namba kwamba kwakuwa sina simu nipate hapa, akauliza na kunipa michongo lakin mchongo wake ulikuwa ngumu mnoo,

Akanitumia dollars 1500 kama mkopo

Nikaenda Nairobi kutafta visa ya Ukraine ikawa ngumu, nikapata jamaa mmoja ni agent akanipa mchongo mzima, na kunielekeza

Nikatimba Ukraine maana hapo ni njia panda ya Nchi nyingi,

Bahati nzuri nikapata kibarua hapa hapa


KWANINI TALAWARY (MPAKISTAN)NA HASSAN WALINIPA HELA?

Mpakistan ni mwenye kampuni nilipoajiriwa baada ya kuona nina tatizo na yeye alilichukulia tatizo kubwa mno, nikamuomba anilipie fine atakata mshahara, akasema kwamba niende ofisini atanipa kiasi hicho na baadae akanifanyia utaratibu wa ticket na kiasi baada ya kuhisi labda naweza naikubaliwe permit pamoja na kulipa fine,

Alafu pale pamoja na kwamba nilikuwa nasubiria permit nilikuwa napewa introduction ya vitu mbalimbali na jinsi ya ufanyaji kazi ndani ya ofis yake,

Hivo alikuwa kanizoea kwa week mbili tulizosubiri permit haitoki.

Alafu yeye kwa siku anauza mpaka AED 80,000 NA AED moja ni sawa na 600 za Tanzania piga mahesabu hapo, anaitwa TALAWAR jina lake hivo hizo ni hela ndogo kwake tena mno, tena mwanzoni akijicommit kunilipia faini nahisi walimwambia kwamba hata kama utamlipia haitasaidia maana hataruhusiwa kufanya kazi hapa na lengo ilikuwa alipe aliajiri, nadhani akashindwa kunikaushia mazima.

Huyo Hassan yeye alinipa assignment moja mpaka sasa ila ni ngumu japo sijamwambia kama ni ngumu, mengine ni siri si ya kuweka hapa
IPO SIKU NTAIWEKA HAPA KAMA VIJANA WANAWEZA WAJIRUSHE, (BLACK DOLLARS) ndo maana alinipa hela hiyo kwa kumkamilishia assignment ya kumshughulikia suala lake.


Maisha safari ndefu

Mimi nitakaa hapa muda alafu niende Norway

Kuna Deal nilipewa na Hassan wa Iran nnikapaogopa Iran

IMG_20180302_135909.jpg
received_1052652394781936.jpeg
 
Hello wakuu habari za siku mbili tatu,

Jaman Mimi ni Kijana Mtanzania ambaye nimekulia Tanzania ,
Nimesomea shule zote Tanzania mpaka elimu ya chuo kikuu,

Kwa bahati mbaya sikumaliza mwaka wangu wa mwishoni wa chuo kikuu kutokana na tatizo la Ada maana Mimi ni miongoni mwa vijana ambao hatukupata mkopo na wazazi wangu ni maskini Sana uko vijijini,

Niliishia mwaka wa Tatu semester ya Kwanza ikabidi niandike barua ya kuomba kupewa HIGHER DIPOLMA IN CORPORATE FINANCE NTA level 7 Badala ya Bachelor degree NTA level 8

Maana Kwa hatua hiyo nimeshavuka kigezo cha Ordinary Diploma, Ila sijafika bachelor level Kati Kati ya NTA LEVEL SIX NA NTA LEVEL 8,
mliosoma Vyuo kama IFM, IAA, Nairobi university, Na Makerere mnajua utaratibu huo,


BAADA YA KUACHA CHUO NA KUPEWA HIGHER DIPLOMA YANGU

Nilisaka ajira Kwa udi na uvumba nikapata kampuni moja ya wahindi wanauza pikipiki Kingshen, wakawa wananilipa 400,000 Kwa mwezi kama msimamizi wa mauzo na kuandaa report zao, pale bapo hela sikuifaidi niliitumia yote kuwasomesha wadogo zangu , nikawa naishi maisha magumu mnoo,

Ila nikafanya nao mwaka mmoja nikapata kazi ya Sales executive Access bank , nikakaa hapo kanshahara ni 520,000 Tu Ila nikawa nakula commission Kwa wateja na wengine wakipata mkopo wananihurumia wananipa Hata 50,000 kama zawadi ya kuwafanyia vema,

Access mkataba ulikuwa miez sita ukaisha sikurenew, nikaomba kweingineko wapi maisha yakawa magumu mnoo, nikaamua kukokaa Sana nikakaa nikawa mtu wa kukopa kila mahari, Maduka yote yakanijua mkopaji,

Wazazi wakashindwa kuwalipia wadogo zangu nikaamua kuwashauri waachane na Vyuo Kwanza wakakubaliana na mimi,

Mafao yangu yakatoka milion 2 Tu yaan nikaamua ninunue kiwanja Mwasonga kigamboni, nikapata Kwa milion 1.5 kipindi hicho Ila kikubwa, nikatumia shillings laki 2 nikaendelea kusaka ajira saa nyingine nikawapa watu hela ya maji wakanidanganya kuna mtu mmoja ni mfanyakazi wa insurance moja alikula 400,000 yangu akanidanganya kuniunganisha kazi bandarini wapi ,

Nikakaa nikatafakari nikaja na jibu kwamba yawezekana maisha mazuri hayako Tanzania ngoja nijaribu nje

Mwaka 2015

Nikapita sehem nikakuta kuna watu wanasema visa za dubai, lilikuwa Tangazo,
Mwanaume nikawauliza wakasema visa ni laki 3 ya miez mitatu, Ila kwakuwa we hatukujui tutakupa ya wiki mbili , nikasema Sawa, nikadhani Dubai ni kama morogoro unaenda Tu unafika unaanza kutafta kazi, kumbe kuna hata muda unaoruhusiwa kukaa kwenye visa ,sikuwa najua neno overstay wala nini,
Nikaenda kigamboni nikauza shamba langu Kwa milion 2.8 lilikiwa nimeshapataga value, nikapata visa 150 USD na hela ya ticket 400 USD Emirates lilikuwa msimu wa punguzo wa ramadhani, nikapanda mpaka dubai ,hapo sijui mtu yeyote uko naenda tu,

Nikafika nikapata hotel nikalala siku moja alafu nikaamua kusaka chumba cha kupanga, aisee kumbe hakuna chumba cha kupanga wana Bed spaces mnashare rooms , ni AED 500 Sawa na laki 3 ya tanzania Kwa mwezi, hela yangu ilikuwa ndogo Sana nikalipa week mbili nkidhani kwamba nitapata Kazi mapema nihame, week mbili zikaisha na visa ya week mbili inaisha hakuna kazi nilipata ilikuwa ni ni presha mno,

Agent aliyenikatia Visa akaanza kunipigia na vitisho juu akaanza kulaumu kwamba Una overstay nimefungiwa visa mpya nazo apply,

Hapo tarehe ya ndege ya kurudi ishapita sina nauli ya kurudi Tanzania , nikafikiria NIFANYE nini, nikaanza kusaka kazi ndani ya overstay days, nikapata kazi moja ya mauzo kampuni ya Alhairay Printing services,


Nikawapa makaratasi yangu yote wakaenda kuapply work permit ikabounse maana nilikuwa kwenye overstay fines, wakasema hatuwezi kukuajili wewe uko kwenye overstay,

Mzee mmoja wa Pakistan akasema ntakusaidia akanilipia nauli nirudi Tanzania Ila nikamuomba kwamba naomba unilipie niende Rwanda maana Tanzania wale ma agent walisema wamefungua kesi kesi niwalipe fidia za kukosesha kazi zao Kwa u overstay miez miwili na nusu,

Lakin suala ni kwamba airport lazima ulipe fine

Kwa kila siku unayozidisha ni 100 AED Sawa na 60,000 ya Tanzania na hapo nshaoverstay karibia siku 80, na sina kitu ilibid nilipe kama milion 3 ya Tanzania,

Nikajitosa kwamba naenda hivo hivo, nikafika airport wakanizuia kwamba nilipe fine au niende Ku surrender wanajifungu watu wanifunge miezi Mitatu kama sina faini dahhhhhhh



Naendelea Chini hapa sasa
Safi sana. Mwanaume ni kupambana
 
Mkuu huu ndio uzalendo na ujasiri tunaouhitaji kwa vijana wa kileo yaani unapambana kufuata ndoto yako ilipo na Mungu huwa hakuachi kamwe huzidi kukuangazia.

No sweet without sweating, your a true husler hata kabla ya kumaliza story nakupa hongera
 
Pole sana Mkuu,ila nchi za wenzetu wapo makini sana kwenye masuala ya ulinzi hasa kuingia kwa raia wa kigeni tofauti na hapa kwetu Tz,unaweza kuingia kinyemela na ukaushi miaka mingi sana bila kufuatiliwa na m2 yeyote!
Asante Sana aisee
 
Mkuu huu ndio uzalendo na ujasiri tunaouhitaji kwa vijana wa kileo yaani unapambana kufuata ndoto yako ilipo na Mungu huwa hakuachi kamwe huzidi kukuangazia.

No sweet without sweating, your a true husler hata kabla ya kumaliza story nakupa hongera
Asante Sana mkuu
 
mmmmmh, haya lete muendelezo..
wazee wa fish trawler pale port Elizabeth na Durban wanakusikiliza tu..
Wakanyagaji wa Greece, turkey, Antwerp, Marseilles, Toulouse, Milan na Rotterdam wanakusoma endelea kumwagika..
 
Back
Top Bottom