Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,399
Tangu kuanzishwa kwa huduma ya kufanya maombi ya viza mtandaoni kwa wageni wanaotarajiwa kutembelea Tanzania, huduma hiyo imezorota katika siku za karibuni.
Muombaji viza anaetaka kutembelea Tanzania kwa kusudio lolote inanmbidi ajaze fomu ya maombi mtandaoni ambapo idara ya uhamiaji makao makuu kupitia mtandao huo itashughulikia maombi ya mgeni huyo na miwsho kutoa viza ya kwenye karatasi.
Viza hiyo ya kwenye karatasi ambayo huitwa e-visa itabebwa na mgeni huyo bila kuhitaji pasi yake ya kusafiria kuwekwa ganda maalum su sticker ya viza.
Tatizo ambalo limejitikeza hadi sasa ni kwamba wageni watarajiwa wamekumbwa na vikwazo vya kimtandao kama kusimama kwa zoezi zima la kujaza fomu hiyo mtandaoni kitendo kinachoitwa "freeze" ambapo muombaji hujikuta anashindwa kuendelea kufanya maombi na hivyo kuachana na zoezi zima.
Tatizo hilo linaonyesha kwamba kuna maombi mengi sana yanayofanywa mtandaoni na mfumo wa kompyuta kushindwa kuhimili uwingi wa maombi hayo.
Hivyo hali hii inapelekea kuleta mashaka juu ya utayari wa idara hiyo ya uhamiaji katika kuwezesha wateja wao kufanya maombi bila vikwazo na kisha kuingiza fedha za kigeni mbalimbali na watalii nchini kutokea Uingereza.
Hali hiyo imepelekea kuwafanya baadhi ya wageni hao watarajiwa kufunga safari kwenda ubalozini ili kuweza kupata habari zaidi kuhusu matatizo hayo, jambo ambalo linazaa tatizo jingine kwamba hakuna taarifa zaidi za kutosheleza juu ya mabadiliko katika kufanya maombi kwamba kwa sasa maombihayo yanafanywa mtandaoni.
Mara nyingi katika kufanya mabadiliko makubwa kama haya huwa ofisi za balozi mbalimbali za nchi zingine huweka alama nyekundu tembezi za kutahadharisha katika tovuti za balozi zao alama ziitwazo kwa kiingereza "Marquee sign" ambayo hujitokkeza kila sekunde.
Pia alama zingine zinazoashiria mabadiliko ni zile ziitwazo "News Alert" na pia taarifa zaidi za kusaidia wageni watarajiwa kupata msaada zaidi wa kuelewa kinachoendelea.
Tatizo jingine kubwa zaidi ambalo limelalamikiwa chinichini na wageni watarajiwa hao ni kitendo cha ubalozi huo kutopokea simu mbalimbali za maulizo au "enquiries" ambapo simu yaweza ikaita siku nzima na kisha kwenda katika sehemu ya mzungumzaji au switchboard ambapo pana maelezo mengi ya jinsi ya kupata huduma kwa kubonyeza namba toka 1 hadi 4.
Mpigaji simu anapochagua moja ya namba hizo khasa namba 2 au 3 kuambiwa asubiri na kwamba yupo kwenye msururu na kisha simu hiyo ya ubalizi hukata bila kutarajia.
Hali hiyo imekuwa ikisababisha usumbufu kwa wageni wengi ambao wengine wanaishi katika miji mingine ambapo huanza kufikiria kusafiri hadi London ili kuweza kuulizia shida zao zinazohusiana na maombi yao ya viza.
Kwa upande wa watanzania ambao wengi wao wamefanya maombi yao kuanzia mwezi wa August wamekuwa wakikumbana na tatizo hilohilo la simu kutopokelewa inapopigwa kiasi cha kuleta masuali kwamba huenda wahusika wanaogopa au wanakwepa kwa makusudi kuzungumza lugha ya kiingereza na kujibu masuali kadha wa kadha.
Katika kutatua tatizo hlo ubalozi ungeweza kuweka options mbalimbali katika switchboard yake kwa kuelekeza nini kifanywe na wapigaji simu.
Au pia kwa upande wa watanzania, ubalozi unaweza kutumia njia ya ujumbe wa maandishi au text messages alert kuwataarifu wale watanzania ambao pasi zao za kusafiria zinakuwa zimekwisharudi ubalozini kutoka Tanzania.
Hivyo basi katika mwaka mpya ujao wa 2020 ni budi ubalozi wetu ubadilike na kuendana na kasi ya matumizi ya mawasiiano iwe ni ujumbe mfupi wa maandishi au barua pepe.
Pia Ubaloizi waweza kabisa kujiunga na mitandao kama facebook na twitter ambapo mawasiliano na watanzania yanakuwa yapo au "available" wakati wowote.
Ikumbukwe kwamba Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza ni moja ya balozi muhimu sana kwa nchi yetu na unatakiwa khasa katika eneo la ajira uwe makini na aina ya watumishi inaowaajiri.