Ubalozi wa Marekani watangaza aina mpya ya miadi (appointment) ya huduma za Viza TANZANIA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubalozi wa Marekani watangaza aina mpya ya miadi (appointment) ya huduma za Viza TANZANIA

Discussion in 'International Forum' started by MaxShimba, Apr 16, 2011.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Aprili 14, 2011

  Kuanzia Ijumaa, Aprili 15, 2011, Ubalozi wa Marekani hapa Dar Es Salaam utaanzisha mchakato mpya ili kurahisisha na kuongeza ufanisi katika kushughulikia maombi ya viza. Maelezo yote katika hili tangazo yanapatikana pia katika tovuti ya ubalozi, Applying for a Nonimmigrant Visa in Tanzania.

  Juu ya mchakato mpya, waombaji wataweza kuchagua miadi kwa ajili ya viza za muda mfupi kupitia tovuti mpya CSC Visa Information Service au kwa kupitia msaada kwa kupiga namba ya kituo cha huduma za wateja +255-22-2194300 ( kwa Tanzania), au +1-703-439-2304 (kwa Marekani), au kwa kupitia huduma ya Skype ID: usvisatanzania. Waombaji watalazimika kufanya malipo ya visa kupitia huduma ya Airtel Money (ZAP) au Citibank Tanzania Limited iliyopo Peugeot House, 36 Upanga Road, Dar es Salaam) KABLA ya kufanya miadi (Appointment).

  Mchakato huu mpya, unasimamiwa na CSC visa information Services, unategemewa kuleta ufanisi na kurahisisha hatua za uombaji wa viza. Mchakato huu mpya wa maombi ya viza unachukua nafasi ya ule wa zamani.

  Kupitia Mchakato huu mpya, wasafiri watalazimika kuuliza habari zote zinazohusu aina zote za viza, mahitaji yake na hatua zake muda wowote kupitia tovuti: CSC Visa Information Service au kwa kupiga simu mida ya saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na mbili kamili jioni (08:00am-06:00pm) kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa kupitia namba +255-22-2194300 ( kwa Tanzania), au +1-703-439-2304 (kwa Marekani), au kupitia Skype ID: usvisatanzania. Huduma zote zitapatikana na kutolewa kwa lugha ya kingereza tu.

  Kuambatana na mabadiliko haya, Zingatia yafuatayo:

  Kuanzia Ijumaa, Aprili 15, 2011, waombaji wote lazima wajaze maombi yao ya visa (DS160) na lazima kulipia gharama za maombi KABLA ya kuchagua siku ya miadi (scheduling appointment).  Waombaji ambao walilipia gharama za maombi ya viza (application fee) kabla ya tarehe Aprili 8, 2011, lakini hawakuchagua siku ya miadi (appointment date) kwa ajili ya mahojiano ya viza, NI LAZIMA wafanye hivyo kabla ya tarehe Aprili 28, 2011.  Malipo ya viza hayawezi kuhamishwa na kutumiwa na mtu mwingine. Malipo ya gharama za viza yataunganishwa na namba za pasipoti ya mwombaji na hayawezi kutumiwa na mtu mwingine yoyote.  Asante kwa ushirikiano na uelewa wenu katika kipindi hiki cha mpito kuelekea huduma bora za mambo ya viza hapa katika ubalozi wa Marekani. Ni mategemeo yetu kwamba huduma hii mpya itaongeza huduma bora za viza kwa wateja.

  Kwa maelezo zaidi kuhusiana na huduma hii yatawekwa katika tovuti yetu: Applying for a Nonimmigrant Visa in Tanzania.


  Article translated in:
  English
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  U.S. Embassy in Dar es Salaam Announces New Visa Appointment Service
  April 14, 2011
  Beginning Friday, April 15, 2011, the U.S. Embassy in Dar es Salaam will implement new procedures to simplify and streamline the visa application process for those traveling to the U.S. All the information found in this press release will be available at the Embassy website, Applying for a Nonimmigrant Visa in Tanzania.


  Under the new procedures, applicants will be able to schedule a non-immigrant visa appointment via a new website at CSC Visa Information Service or through the assistance of a new call center at +255-22-2194300 (in Tanzania), +1-703-439-2304 (in the United States), or using Skype ID: usvisatanzania. Applicants will need to pay applicable fees through Airtel Money or at Tanzania Limited Citibank (Peugeot House, 36 Upanga Road, Dar es Salaam) before booking an appointment.


  These new procedures, managed by CSC Visa Information Services, should greatly improve and simplify the visa application process. The new visa appointment system replaces the previous appointment system.


  Under this new system, travelers will be able to make inquiries on the full range of visa categories, requirements, and procedures online anytime at CSC Visa Information Service or by phone between 8:00 am – 6:00 pm Monday through Friday at +255-222-194-300 (in Tanzania), +1-703-439-2304 (in the United States), or using Skype ID: usvisatanzania. All services are provided in English only.


  In connection with these changes, please note the following:
  Beginning Friday, April 15, 2011, applicants will be required to complete the visa application form (DS-160) and pay the application fee prior to scheduling an appointment.


  Applicants who have paid their application fee prior to Friday, April 8, 2011, but have not scheduled an appointment for a visa interview must schedule a visa interview appointment BEFORE Thursday, April 28, 2011.


  Fee payments will no longer be transferable. The fee payment will be electronically tied to applicant's passport number and cannot be transferred to anyone else.  Thank you for your cooperation and understanding throughout this transition to better visa services at U.S. Embassy Dar es Salaam. We hope that this new service will enhance our customers' visa experience.
  This procedure with more detailed instructions will be posted on our website, Applying for a Nonimmigrant Visa in Tanzania.
   
Loading...