Marekani haijampatia viza Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ya kuingia UN

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Marekani haijampatia viza Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ya kuingia UN.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ametangaza kuwa Marekani bado haijampatia Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov viza ya kuingia nchini humo kushiriki katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York.

Sergei Ryabkov amesema leo kuwa, Marekani bado haijatoa viza kwa ujumbe wa Russia unaoongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov unaoelekea New York kushiriki katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Afisa huyo wa Russia ameendelea kueleza kwamba Moscow haina msimamo wowote juu ya kufichuliwa na kusambazwa nyaraka za Pentagon, lakini haiwezekani kukana usambazaji wa makusudi wa taarifa bandia uliofanywa na Marekani yenyewe.

Ryabkov amebainisha kwamba, "kwa kuwa upande wa pili katika mzozo uliopo ni Marekani na kwa kutilia maanani ukweli kwamba inaendesha vita vya mchanganyiko dhidi yetu, upo uwezekano wa kufanya hila kama hiyo kwa madhumuni ya kumpotosha adui yake, yaani Russia. Mimi sitoi madai yoyote, lakini ninakiri kuwa aina zote za dhana zinaweza kufikirika hapa".

Wakati huo huo, Bunge la Russia la Duma lilitangaza jana Jumanne kwamba ubalozi wa Marekani nchini Ukraine umekuwa ofisi ya ugani ya wizara ya ulinzi ya nchi hiyo (Pentagon) ili kuendeleza malengo ya kijeshi na kibiolojia ya Washington.

Vyombo vingi vya habari vimeandika kuwa Pentagon inaendelea kuchunguza kuvuja kwa taarifa kwenye mtandao wa kijamii zinazoelezea hali ya wanajeshi wa Ukraine na mipango ya Marekani na NATO ya kuwaimarisha askari hao.

Gazeti la New York Times limeripoti kuwa inavyoonekana, nyaraka zinazohusiana na mapema mwezi Machi zimesambazwa kwenye mtandao wa Telegram na waungaji mkono wa serikali ya Russia.
 
Si Russia ndo mwenyekiti au? sasa watafanyaje vikao bila mwenyekiti?
 
"kwa kuwa upande wa pili katika mzozo uliopo ni Marekani na kwa kutilia maanani ukweli kwamba inaendesha vita vya mchanganyiko dhidi yetu, upo uwezekano wa kufanya hila kama hiyo kwa madhumuni ya kumpotosha adui yake, yaani Russia. Mimi sitoi madai yoyote, lakini ninakiri kuwa aina zote za dhana zinaweza kufikirika hapa".
Watu weupe wanaongea kidogo lakini huwa wanakuwa na point kubwa.
 
Yote kwa yote, Russia ni lidude fulani kubwa hivi......haiwezekani America awe analalamika lalamika kila siku. Mara kuingiliwa uchaguzi 2016, na saaa hv hili suala la Ukraine mlalamikaji mkubwa naona ni US na wenzake wa Ulaya.
Nilishangaa juzi hapa kulikuwa na event fulani ambapo mabalozi mbalimbali waliongea, ghafla tu balozi wa US wakati anaongea akaiingiza hoja ya Ukraine kwa malalamiko makuu. Nikajua eh, kumbe hili lijamaa ni lidude ee!
 
Hapa ndio watu wajiulize UN mali ya Nani
Kama vipi Ihamishwe tu Kupiga nae Umeshindwa Unakimbilia Figisu zisizo na Kichwa wala Miguu
Na Unajiita mwana Demokrasia
Upuuzi mtupu
 
Marekani haijampatia viza Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ya kuingia UN.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ametangaza kuwa Marekani bado haijampatia Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov viza ya kuingia nchini humo kushiriki katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York.

Sergei Ryabkov amesema leo kuwa, Marekani bado haijatoa viza kwa ujumbe wa Russia unaoongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov unaoelekea New York kushiriki katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Afisa huyo wa Russia ameendelea kueleza kwamba Moscow haina msimamo wowote juu ya kufichuliwa na kusambazwa nyaraka za Pentagon, lakini haiwezekani kukana usambazaji wa makusudi wa taarifa bandia uliofanywa na Marekani yenyewe.

Ryabkov amebainisha kwamba, "kwa kuwa upande wa pili katika mzozo uliopo ni Marekani na kwa kutilia maanani ukweli kwamba inaendesha vita vya mchanganyiko dhidi yetu, upo uwezekano wa kufanya hila kama hiyo kwa madhumuni ya kumpotosha adui yake, yaani Russia. Mimi sitoi madai yoyote, lakini ninakiri kuwa aina zote za dhana zinaweza kufikirika hapa".

Wakati huo huo, Bunge la Russia la Duma lilitangaza jana Jumanne kwamba ubalozi wa Marekani nchini Ukraine umekuwa ofisi ya ugani ya wizara ya ulinzi ya nchi hiyo (Pentagon) ili kuendeleza malengo ya kijeshi na kibiolojia ya Washington.

Vyombo vingi vya habari vimeandika kuwa Pentagon inaendelea kuchunguza kuvuja kwa taarifa kwenye mtandao wa kijamii zinazoelezea hali ya wanajeshi wa Ukraine na mipango ya Marekani na NATO ya kuwaimarisha askari hao.

Gazeti la New York Times limeripoti kuwa inavyoonekana, nyaraka zinazohusiana na mapema mwezi Machi zimesambazwa kwenye mtandao wa Telegram na waungaji mkono wa serikali ya Russia.
Kuondoa ukiritimba huu wa Merikani. ndio mara zote usisitiza kwamba Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa uhamishiwe Geneva, we mtu utamunyimaje VISA member wa UN wanao kuja ku-attend mkutano wa umoja wa Mataifa na wala si mkutano wa Govt ya Merikani na mataifa mengine.

Huu ni kuutumia vibaya Umoja wa Mataifa kwa manufaa ya kisiasa wa utawala wa Merikani, kukomesha ujinga huu makao Makuu ya UN ihamishiwe huko Geneva.
 
Back
Top Bottom