Ubaguzi

bagwell

Senior Member
Sep 19, 2012
113
25
Kwanza wakuu habari zenu.....
Napenda kukupa habari hii ya nafasi za masomo katika shule moja ya jijini Upanga ambayo inaitwa Al-Muntazir Islamic Seminary(ALMIS), Shule hii inaongozwa na mashia wenye imani kali za dhehebu yao ya kishia.
Ukweli hii shule ni nzuri sana inasomesha uzuri na inafatilia maendeleo mazuri ya watoto wanaosomeshwa pale, na katika mazingira ya dini pale kuna watu wenye misimamo ya dini tafauti na hilo lipo katika shule nyingi sana hapa tanzania.Lakini kinachonikera mm ni pale mtu/mzazi akienda kuomba nafasi ya mtoto kwa ajili ya kusoma, sasa hapo ndipo kasheshe inaanza maana kama ikiwa sio SHia hupati nafasi labda uwe una hela ndio utapata nafasi ya kijana wako na kama hata ukiwa shia huna hela huwezi ukapatiwa nafasi ya kijana wako.

Na katika jambo la kutoa nafasi za masomo kuna mchezo ambao mm kama mzazi ambae watoto wangu wameathirika na mitindo yao ni kua wanatangaza nafasi nyingi sana za kujiunga ila ukweli ni kwamba hata watoto 500 wakiomba wanaopata nafasi ni 20 na ukiwauliza nafasi zilikua chache...sasa mm najiuliza kma walikua wanajua kua nafasi ni chache kwanini wanatoa fomu za watu kujiunga zaidi ya ile nafasi walizokua nazo? huu sio wizi wanaofanya?....Na hata kma ikiwa kijana wako amefaulu au hajafaulu ukiwauliza nioneshe matokeo niyaone hawataki sasa kwanini NECTA wanaonesha matokeo ila hawa mijamaa hawaoneshi?...hivi kwanini inakua hivi?...

Kama kuna kiongozi wa SERIKALI yeyote humu naomba suala hili alifatilie kwa nguvu zake zote..na hata ikibidi hizi shule za Almuntazir wapewe onyo kali....

Ahsanteni
naomba kutoa hoja
 
mpeleke shule nyingine nzuri zipo hizo ni kwa ajili ya mashia na matajiri wenzao/
 
Pole mkuu, hiyo ni bishara huria, mi nadhani wana haki ya kuchukua wamtakae na kumuacha wamatakae.
Usipate tabu mkuu, shule zipo kibao, mpeleke kweingine.
Zipo shule nyingi tu bongo za wahindi watupu au watu wengine wa kundi fulani.
Ni biashara na wanauamzi wa nani wamuuzie na nani wasimuuzie.
 
angali kila upande ndugu, usiumizee kichwa na sehemu 1, kuna shule nzur tuu hapa mjin ..maneno ya marafik na ndugu kuhusu shule 1 tuu, labd coz kuna watoto wao wanasoma hapa yackutishe,!
 
Umeashaliona tatizo unang ang ania kulalama wakati kuna shule nyingi tuu nzuri...
Tafuta wenyeji wa Tanga wanao´ifahamu shule moja ya kidini watakuelekeza,hiyo shule iko kwenye kiwango kizuri sana..
Nenda Peramiho Songea kwa wamisional uko ndio uatakiambia mwenyewe
Kama mvivu wa wakusafiri fika Bwagamoyo kule mission kwa mtafute father Bayo obgea nae alafu uje utuambie
Mwisho wa wote hata hapo Dar kuna shule nyingi lawama ya nini dugu yangu.....
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom