Ubaguzi wazidi kuiangamiza CHADEMA

Chama Pekee cha upizani Tanzania ni chadema;
Cufu=ccmB(wamefunga ndoa na ccm)
TLP=Mrema shushu wa ccm
NCCR=Mbatia Mbunge wa kuteuliwa na CCM
 
ubaguzi wa chadema ni wa asili na ulianza wakati wa babu zetu kwa hiyo ubaguzi kwa chadema ni asili yao.
 
Good analysis. Ila najua kuna watu watakutukana na kukupa majina kibao ya ajabu

Hii analysis ni very selective....mlishasahau ubaguzi huu waliuanza CUF?Wakati CUF ilipokuwa na wabunge wengi baada ya uchaguzi wa 2005 ilimshirikisha nani?....by extension CUF si chama cha upinzani tena!Si kimeshafunga ndoa na CCM kule zenji?Kwa sasa CCM na CUF wanabonyezana kizenji tu....why should Chadema join forces with the "ruling" party(CUF)? na wanafiki kama NCCR?
 
MziziMkavu nakushauri uendelee na thread zako za kishirikina na tiba za kusadikika kule JF DOCTOR, Unalazimisha siasa lakini siasa haikutaki.

Sintoshangaa kesho ndio ukija na thread ya Chadema yashinda kata zote 4 Arusha, kama unaishi North Korea nakushauri hapa JF ubakie tu kuwa msomaji, wengi unatuchukiza kila siku kutupachikia habari za juzi wakati kila mtu anaitegemea JF kama be the fist to know, kama unatumika tafuta namna bora ya kutumika na si style ya condom.
 
Last edited by a moderator:
Umesahau maneno ya Nasari?
Mimi nayakumbuka ya UVCCM pwani wakiongozwa na Prince Ridhiwani Kikwete kwamba Mrithi wa JK hawezi kutoka kaskazini.

Na pia nakumbuka JK alituambia anayo orodha ya wauza unga, kwahiyo hawa wanaokamatwa sasa hivi na kuvusha kilo 150 ambazo ni sawa na mifuko mitatu ya cement basi haka Karidhiwani katakuwa ndio jemedari wao, ndio maana Baba yupo kimya.
 
Mimi binafsi sisikitiki hata kidogo kwa nccr kuamua kushirikiana na ccm ili kuongoza halmashauri ya Uvinza. Kila chama kinajua kinatafuta nini na kifanyeje ili kufikia malengo.
Chama cha upinzani kushirikiana na ccm na kukiacha chama cha upinzani ni salamu tosha kuwa wao si wapinzani isipokuwa ni ccm waliovaa ngozi ya upinzani.
Na suala la Arusha huyo mwandishi hata halijui amekurupuka na kuandika utumbo. TLP ina madiwani wawili lakini mmoja wa kiti maalum amezuiwa kuhudhuria vikao. Lakini pia asichojua mwandishi wa makala hii ni kwamba Meya anaondolewa kwa 2/3 ya kura za madiwani ambapo hata kama Chadema wakiunganisha nguvu na TLP hawafikishi kura 21 za kumng'oa meya. Hatahivyo itakuwa ngumu kwa meya wa ccm kudhibiti maamuzi kwakuwa Chadema ndiyo ina wingi wa kura za maamuzi kwahiyo hapo Chadema itakuwa inamuendesha meya kwa kudhibiti maamuzi!
 
Ubaguzi mmezanzisha nyinyi, umesahau maneno ya Nasari?

Sijui kwanini unasahau ukweli halafu unautetea kwa nguvu sana uongo .... kwenye thread hii hili la ukabila unalipenda sana....!

ulisoma "Historia"? km ndiyo ... haukuwahi kuona mapambano ya kikabila kt watemi wa makabila ya Kilimanjaro? Je haujui hakuna kabila la Wachaga? Ila Wachaga ni mkusanyiko wa Makabila km ma4 au zaidi (wakibosho, wamachame, wamarangu, warombo nk) ... Unaposema Wachaga tayari umeisha ondoa ndhana ya Ukabila kwasababu unataja muungano wa makabila zaidi ya moja....!
Sijui km nitaeleweka kabila la wachaga siyo moja kama waha, au wa haya au wasukuma ... Mwanza mpaka Shy lugha ni ile ile tofauti sana na Wachaga wenye kutosikilizana hata kwa sentensi ....!

Ila imekua vyema sana Ukabila utumike kukataa watu ili taifa litetereke hadi tuamue kuuacha mtizamo huo...
 
dhambi ya ubaguzi, kibri na kujiona bora haitoifikisha chdm mbali. sasa hivi yameongezeka mambo ya sumu, kujilipua nk..... CHAMA CHA KIGAIDI. eti tulianza na Mungu......... Mungu awe upande wa wabaguzi? mungu awe upande wa padre muasi na fisadi!? thubutu!!!!!!!!!!!!!
 

Uchambuzi ni mi lakini uko shallow sana. Ukiangalia juu-juu kama ulivyofanya utaona ni hivyo lakini ukiangalia kwa makini utona kinyume kabisa! Jiulize swli dogo tu; kwa nini CCM na CUF walimchagua Henry Matata kuwa Meya wa Jiji la Mwanza wakati yeye ni mwanachama wa Chadema?
 
Hii thread ni nzuri ana lakini kuna watu humu wameanza kuichafua na punde wengine tutaisusa. Inabidi sasa kila thread iwe na Moderator wake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…