mwl. Nyerere alishawahi kusema, "dhambi ya ubaguzi haifi, inaendelea. Dhambi ya ubaguzi ukishakuitenda inaendelea, ni sawa na kula nyama ya mtu, ukila nyama ya mtu utaendelea tu.".
kila siku dhambi ya ubaguzi inazidi kumea na kuimarika ndani ya chadema kiasi kwamba kwa sasa wamefikia hata kuanza kutesa baadhi ya watu ili kuendeleza dhambi ya ubaguzi.
Viongozi wa chadema kila siku wanapanda kwenye majukwaa na kujigamba wakisema baadhi ya waajiriwa wa usalama wa taifa wanawapa siri za serikali na ccm lakini wanasahau kuwa, maneno yao yanachagiza karma law inayosema, what goes around comes around or as you sow, so shall you reap.
viongozi wa chadema walishawahi kunukuliwa kwenye mikutano katika thread hii;
chadema wanafurahi sana kudai wanapewa siri za serikali au ccm na baadhi ya waajiriwa wa usalama wa taifa lakini wanakuwa wa kwanza kutoa malalamiko na kudai wanahujumiwa pale siri zao zinapochukuliwa na watu hao hao wanaodai wanawapa siri za serikali au ccm. Waingereza wanasema, don't hate the player, hate the game!
unapopewa lazima pia ufahamu kuwa utatoa kwa njia hiyo hiyo iliyotumika katika kupewa. this is natural justice!
baadhi ya viongozi wakuu wa chadema ni ruksa kuwasiliana na baadhi ya wana usalama wa taifa (tiss) lakini mwanachadema mwingine akifanya hivyo hukumu yake ni kuteswa ndani ya ofisi za red brigade.
Baadhi ya viongozi wakuu wa chadema ni ruksa kuwa na rafiki au ndugu ambaye anafanya kazi katika idara ya usalama wa taifa, lakini mwanachama mwingine akionekana hata anapanda gari ya mfanyakazi wa usalama wa taifa adhabu yake ni kuteswa na kufukuzwa uanachama.
Baadhi ya viongozi wakuu wa chadema ni ruksa kuwa na namba za simu za viongozi wa ccm au serikali lakini mwanachama mwingine akiwa pia na namba hizo hizo anaitwa msaliti.
Baadhi ya viongozi wakuu wa chadema huwa wanafanya mawasiliano na mwenyekiti wa ccm taifa, lakini hao hao viongozi wakigundua mwanachama mwingine anafanya pia mawasiliano kama hayo, watamuita msaliti ambaye adhabu yake ni kufukuzwa ndani ya chama.
Hii haitokei kwa bahati mbaya bali kinachofanyika ni endelezo la dhambi ya ubaguzi ambayo inaendelea kuitafuna chadema.
chacha wangwe aliishabikia hali hii lakini mwisho wake ikamtafuna.
zitto kabwe na kundi lake waliishabikia hali hii mwisho wake ikawatafuna.
khalid kagenzi pia aliishabikia kwa kuanzisha red brigade, mwisho wake imemtafuna karibia apoteze maisha yake wakati anateswa ndani ya ofisi za red brigade kama siyo wasamalia wema kupiga kelele kuomba msaada.
Cuf na nccr-mageuzi walishabikia ubaguzi wa chadema kwa mwamvuli wa ukawa, kwa sasa umeanza kuwatafuna kwa kuanza kubaguliwa!. Neno ukawa kwa sasa ni bidhaa isiyouzwa au kuuzika ndani ya midomo ya wanachadema baada ya chaguzi za serikali za mitaa.
ifahamike tu, leo ni kwa mwingine ndani ya chadema lakini kesho ni kwako unayeendeleza ubaguzi huo ndani ya chadema.