Ubaguzi sio chaguo kwetu sisi wanadamu, bali ni jambo lipo(Automatically) ndani yetu. Hitimisho dunia bila ya ubaguzi haiwezekani na haitawezekana

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,050
10,487
Ukweli ni kuwa vita dhidi ya ubaguzi vilishindwa kabla ya kuwapo wazo la kupinga ubaguzi. Nani leo hii anaweza kusimama even hao wanaojinasibu kuwa ni wanaharakati wa kupinga ubaguzi na kusema kuwa yeye sio mbaguzi? Jibu ni hakuna sababu kila mwanadamu ana vina saba vya ubaguzi bali kinacho tutofautisha ni namna tunavyoact mbele ya vitu tusivyovipenda.

Ulimwengu unakadiliwa kuwa na watu takriban bilioni 7 wenye sifa tofauti tofauti kuanzia muonekano mpaka namna wanavyofikiria. Swali ni je nani awezaye kudeal angalau na watu laki moja kwa kuwapa heshima na uangalizi ulio sawa kwa watu wote na pasiwepo hata mtu mmoja ambaye atahisi kutotendewa haki au kupewa favor zaidi ya mwingine?

Kama ni ruksa mwanadamu kuchagua kitu kimoja dhidi ya kingine basi ni ruksa kwa mwanadamu huyo kumbagua mtu mmoja dhidi ya mwingine na ndicho haswa kinachotokea ulimwenguni.

Leo hii Tanzania kuna watu wanajiona wao ni Superior dhidi ya wengine sasa kwa nini tuwaite Mabeberu ni wabaguzi huku tukiona sawa wenzetu tunaoshare nao katiba ambao hawataki tuwe karibu hata na fences za mabangaloo yao.

That's life ubaguzi unaanzia mbali sana the funniest thing ni kuwa mtu anaanza kuchukia na kubagua viungo vyake mwenyewe mwilini. Je mtu wa namna hii anaweza kuwa na guts za kupinga ubaguzi unaotokea baina ya wanadamu?

Just ask yourself wazungu tuliwakosea nini mpaka wakaanza kutubagua licha ya kuja Afrika kuchukua rasilimali zetu na kuwatesa bibi/ babu zetu still mpaka leo hawatupi kipaumbele. Somo kubwa kuhusu ubaguzi ni kuwa mtu akiamua kukubagua no matter umemfanyia mazuri mangapi atakubagua tu.

Mimi BabaMorgan ni miongoni mwa vijana ambao naamini kila kitu kinachotokea ulimwenguni bila ya kujali ni kibaya au kizuri kimepangwa kuwa hivyo swali ni je kipo hivyo kwa maslahi ya nani?

From northern part of Tanzania.
 
Ila na sisi waafrika tunauendekeza..... hata kwa dada zetu weupe hawa tumewatukuza kiasi cha kuwafanya hata wengi weusi watumie make up kutoa weusi kidogo.

pia naonaga hata maofisini wazungu wakija wanapewa umuhimu mkubwa kwenye kushughulikiwa.
 
Unataka kusema Mungu alietuumba na akakemea ubaguzi, amefanya "mistake "kukemea jambo ambalo kw mujibu wako practically haliwezekani, yan Mungu muweza na mjuzi wa vyote amekemea kitu ambacho "hakiwezekani kukanyika?ndivyo unavyotaka kusema?

Yeye ameona inawezkana wanadamu kuishi bila ubaguzi ndo mana akaleta muongozo "vitabu" ambavyo ikiwa tutiashi kw mujibu wa muongozo huo tutaweza kuishi bila ubaguzi,matokeo yake wewe na wenzako mlio kataa muongozo huo mmeshindwa kuumaliza ubaguzi, then una hitimisha kuwa ubaguz ni lazima uwepo, sio kweli, Endapo tungeshikmana na mafundisho ya Mwenyezimungu ubagzi ungeisha.

Tumia kalamu yako na elimu yako kwa usahihi, trust me hii dunia ni ya Mungu na ukiishi bila kufuata utaratibu alio uweka "vitabu vyake"lazima tutapata tabu.Mkuu ni sawa na mm niombe hifadhi nyumbani kwako halafu nije na sheria zangu, je utaendelea kunifadhili?je nitaishi kwa Amani?
 
Acha hizo watu sisi siyo wabaguzi kabisaaa nakataa wala wazungu siyo wabaguzi,.... ila ni mtu mwenyewe mmojammoja hasa dhaifu ndiyo anajibagua kwa kuwa anatamani kuwa km watu/mtu flani flani ktk jamii!!

Mfano mweusi anatamani saaana, kuwa karibu na wazungu afanye km wanavyofanya wao!! lakini sasa haweziii......Mzungu yeye anagusa tu mambo hayooo!! ni msafi, mzuri, mtamu kwa kila kitu!

Mwafrika shida, sura/roho ngumu na mbaya, visasi,..kula kwa shida, nyumba za hovyo sasa kwa nini usimtamani mweupe??...mwenye upendo/thamani/pesa/huruma/mtoa misaada nk!???

Mnatamani mambo yao na wanawapa lkn mna shindwa tatizo linakuja kuwa wao wamesha jua mnapenda kuwaowa! mpate vitoto virembo ndo maana wanawaringia ivo! lkn mngekomaaa kabisa! wange watafuta kwa tochi!

kubaguliwa ni mapungufu ya mbaguliwa na wala si mbaguajai mwenyewe...mie huaga niko ivi! ukinibagua na mie nakubagua mara dufu.....
 
Unataka kusema Mungu alietuumba na akakemea ubaguzi, amefanya "mistake "kukemea jambo ambalo kw mujibu wako practically haliwezekani...
Inawezekana kuishi bila ya ubaguzi kivipi? Je ulimwengu wa sasa unaweza kulinganisha heshima anayopewa mwenye pesa versus asiye na pesa?

Chanzo kikubwa cha ubaguzi ni utofauti pengine kiwango cha ubaguzi lingekuwa kidogo kama wote tungekuwa na sifa zinazofanana.

Siwezi kosoa uumbaji wa Mwenyezi Mungu ila akili yangu inanituma hivi ndivyo dunia ilikusudiwa kuwa.
 
Acha hizo watu sisi siyo wabaguzi kabisaaa nakataa wala wazungu siyo wabaguzi,.... ila ni mtu mwenyewe mmojammoja hasa dhaifu ndiyo anajibagua kwa kuwa anatamani kuwa km watu/mtu flani flani ktk jamii...
Kwani hakuna mtu mweusi anayembagua mzungu? WaAfrika pekee yao sio wahanga wa ubaguzi zipo jamii nyingi zinabaguliwa kutokana na sababu tofauti tofauti kama dini, tamaduni, mazingira, nk
 
Kwani hakuna mtu mweusi anayembagua mzungu? WaAfrika pekee yao sio wahanga wa ubaguzi zipo jamii nyingi zinabaguliwa kutokana na sababu tofauti tofauti kama dini, tamaduni, mazingira, nk
Yaani weye ukale mibichwa ya rijikiti Moto! lenu huko! ukisindikizia na chimpumu uchwara hapa...af eti usiku wende ukajambie kwa nyumba ya wasabato!! kisa??? eti wasikubague???...tutakutandika mpaka unye!!
 
Kila mtu akikaa eneo lake na akalitawala vizuri, na kufurahia hatahitaji............

Anyway ubaguzi kutokana na utofauti ni matumizi mabovu ya akili yako tu. Kwa nini kila mtu asijivunie kuwa yeye?
 
20220215_122159.jpg
images (16).jpeg
 
Dunia bila ubaguzi haiwezekani kwasababu tunatofautina ktk vipato, Imani ,mitazamo ya maisha,falsafa ,elimu,vipaumbele,itikadi za kisiasa yaani kila aspect tunazidiana hakuwezi kuwa na Usawa hata siku moja kwa kuwa Huyu anaamini na anatenda kwa njia anayoona inamfaa yeye mwingine haoni Kama itamfaa yeye

Tunajidanganya kuamini ktk Usawa usiowezekana kuwepo hata siku moja Ni Mwendo wa kubaguana tu Hadi siku tunakufa
 
ubaguzi upo utake usitake, na ni nature. mi sijisumbua kuupinga wala kujisikia vibaya mtu akinibagua.
ndo maana kuna SITI za mbele kwenye sherehe
 
Back
Top Bottom