DOKEZO Ubaguzi katika baadhi ya vyuo vikuu Tanzania

DOKEZO Ubaguzi katika baadhi ya vyuo vikuu Tanzania

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

nipopale

New Member
Joined
Feb 20, 2025
Posts
3
Reaction score
4
Kabla sijaleta mada yangu kuhusu ubaguzi niliouona katika baadhi ya vyuo vikuu vya Tanzani ninaomba niwaulize swali moja la msingi. Je! kuna tofauti kati ya bacholor Degree ya inayoitwa university na inayoitwa Institution? Je! TCU inazitambua hizi bachor Degree kwa weight tofauti?

Mada
Kuna baadhi ya viongozi wa vyuo vikuu hapa Tanzania(specifically nawajua ila sitowataja) wanafanya ubaguzi mkubwa sana kwenye secta ya elimu na haswa kwenye eneo la wana taaluma).

Tunashukuru sana serikali kwa kuleta kitu kinchoitwa ajira porta ambacho kwa kiasi kimepunguza huu ubaguzi ingawa unyanyasaji ni mkubwa. Kuna baadhi ya vyuo vikuu vya serikali ambavyo vinakataa watu waliosoma kwenye Institute(Mfano IFM,TIA,DIT,IAA) kuwa wakufunzi katika vyuo vyao kwa kisingizio kwamba mtu aliyesoma Institute hawezi kufundisha university).

Inafika mahali hata wale ambao wamepitia ajira portal wakafanya vizuri wakawapita hata wale wa vyuo vikuu wanavyovitaka wamekuwa wakinyanyaswa kwa maneno mabaya kwamba wamekosea njia kuja university na mlango upo wazi kuondoka.

Kama hao wa university zao wanazoziamini wameshindwa na watu wa Institute ambazo wanazozidharau(MWENYE AKILI HAPA NI NANI?).

Universal(University) ni nini kama hauna akili? Je wenye akili ni wanaotoka tu SUA, UDSM au Mzumbe(Politics). Hatuna lengo la kuchafua watu au vyuo lakini tunaiomba serikali iangalie upya aina ya viongozi ambao inawateua kwenye eneo la vyuo vikuu.

Wengi wamekuwa wakihama na vyuo walivyokuwa wanafanyia kazi kichwani na kuvipeleka kwenye vyuo vingine. Utumishi nao waingilie kati kwenye swala hili ili wale ambao wamesoma kwenye taasisi wapewe heshima yao.
 
Uongo bhana hujakizi vigezo ,kila chuo kina vigezo hawaajiri tu ovyo ovyo
 
Uongo bhana hujakizi vigezo ,kila chuo kina vigezo hawaajiri tu ovyo ovyo
Kukidhi vigezo gani tena kama Utumishi wamempeleka mtu halafu unamwambia amekosea njia. Yaani utumishi waniajiri halafu useme sijakidhi vigezo
 
Kama tumefika huku basi hali ni mbaya sana Kwa kweli.
 
Back
Top Bottom