Ubadhirifu mkubwa Benki ya Posta

HAYA TENA KINARA WA KUGHUSHI BENKI YA POSTA NDG BENEDICT KAPELEGA ANA SOO KWA MWAJIRI WAKE KANUNUA USED CAR KAGHUSHI DOCUMENT ZA BLAND NEW CAR....ETI SHIRIKA LA POSTA HOI KIFEDHA LINAWEZAJE KUWA NA AFYA KIFEDHA KAMA UONGOZI NI WA HAWA MAFISADI.....BLAVO JF ni kuwamulika tuu na kuwaweka peupeeee waonwe na wenye busara wawarekebishe
 
Mmeshaanza kuziba mianaya ya BOT na zile 10% za mikataba, mnafikiri CCM na Mafisadi watakula wapi?

TPB ndio mfuko mpya wa ustawishaji wa "jamii"!
 
BoT yachunguza ufisadi ndani ya Benki ya Posta

na Ratifa Baranyikwa
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

SIKU chache baada ya kuibuka kwa tuhuma za ubadhirifu ndani ya Benki ya Posta (TPB), Benki Kuu (BoT) imekiri kutuma maofisa wake kufanya uchunguzi ndani ya benki hiyo.

Gavana wa BoT, Profesa Beno Ndullu alilithibitishia gazeti hili jana kuwa, BoT imewatuma maofisa hao kufanya uchunguzi.

Hata hivyo, kwa kutaka kutohusisha suala hilo na tuhuma za ubadhirifu zinazoikabili TPB, Profesa Ndullu alisema kuwa wachunguzi hao walitumwa katika utaratibu wa kawaida wa BoT kuzikagua benki kila baada ya muda fulani.

Pamoja na kusema hivyo, alisema zinapotokea tuhuma za kuwapo kwa matatizo ya kiutendaji, basi maofisa hao wa BoT hulazimika kufanya uchunguzi wa kina zaidi, ili kubaini mapungufu.

Taarifa zilizoifikia Tanzania Daima siku kadhaa zilizopita, zilibainisha kuwa maofisa hao wawili wa BoT, ambao majina yao hayakutajwa, walitumwa kwa kazi maalum ya kuchunguza tuhuma hizo za ubadhirifu.

“Sisi tunafanya uchunguzi… ni kawaida yetu, tunaita ‘on site supervision’ inategemeana na taarifa ya benki… kila baada ya miezi mitatu tunafanya uchunguzi na tunafanya kama sehemu ya kazi yetu,” alisema Ndullu.

Tanzania Daima ambayo ilikuwa ikifika mara kwa mara katika ofisi za Makao Makuu ya benki hiyo mwezi uliopita kwa nia ya kuonana na Mtendaji Mkuu wake, Alphonse Kihwele, imekuwa ikipewa taarifa za kuwepo kwa vikao vya bodi ya wakurugenzi.

Kuibuka kwa tuhuma hizo katika mtandao wa intaneti, kuliwashtua viongozi wakuu wa benki hiyo, ikiwamo Bodi ya Wakurugenzi na kwa kushirikiana na menejimenti iliunda kamati maalumu ya kuwasaka watu wanaoaminika kusambaza taarifa hizo hali iliyosababisha bodi hiyo kuwapa likizo za lazima maofisa wake watatu.

Hata hivyo, Kihwele akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili ambalo lilikuwa likitaka kupata ufafanuzi wa juu ya kile kinachoendelea kwenye vikao hivyo sambamba na kutaka kupata maendeleo ya uchunguzi, alimtaka mwandishi wa habari hizi kuandika maswali aliyotaka kumhoji na kisha kuyawasilisha ofisini kwake.

Tanzania Daima ilifanya hivyo na kuwasilisha maswali kwa Mtendaji Mkuu huyo, lakini hata hivyo alipopigiwa simu alisema kuwa hana majibu ya maswali aliyoulizwa.

Katika maswali ambayo gazeti hili lilitaka kupata uthibitisho, ni pamoja na kuwepo kwa taarifa za benki hiyo kuwafukuza kazi watumishi wake kwa madai kuwa ndio waliovujisha siri za benki hiyo.

Aidha, ufafanuzi mwingine ambao ulikuwa ukihitajika ni pamoja na kutaka kujua zoezi la kuwachunguza watu wanaoaminika kutoa taarifa za siri za benki hiyo kwenye mtandao wa Jamboforums.

Habazi zilizopatikana zinadai kuwa, moja kati ya ufisadi unaotajwa unahusisha tuhuma za kughushi barua ya Bodi ya Benki ya Posta, ili kumuwezesha Kihwele kuongezewa mkataba, wakati bodi inadai haikuwahi kukaa kikao kupendekeza aongezewe muda.

Mbali na tuhuma hizo, pia imeelezwa kuwa ufisadi mwingine uliofanyika unamhusisha kigogo mwingine anayedaiwa kuwalazimisha watengeneza mahesabu katika Idara ya Fedha kuhakikisha wanatoa hesabu zinazoonyesha benki inapata faida kinyume cha ukweli.

Aidha, tuhuma nyingine zilizomo kwenye waraka huo ni zile zinazodai kuwa, menejimenti imeandaa mtandao unaowahusisha baadhi ya wafanyakazi ndani ya benki hiyo, ili kuweza kufanikisha ufisadi huo.

Pamoja na mambo mengine, inadaiwa kuwa, timu hiyo ndiyo iliyoiingiza benki hiyo katika mikataba mibovu ikiwemo ule wa uwekezaji na uendeshaji wa mashine za kutolea fedha (ATMs) ambazo zinadaiwa kuigharimu benki hiyo mamilioni ya fedha.

Mkataba huo ambao TPB imeingia na taasisi moja ya fedha unaelezwa kuwa, ni kielelezo tosha cha mikataba ya kifisadi yenye nia ya kuliangamiza shirika ambapo benki hiyo imekuwa ikiilipa taasisi hiyo mamilioni ya pesa bila kupata faida yoyote.

Katika waraka huo wenye kurasa tisa, pia ufisadi mwingine uliolalamikiwa ni ule wa kuwepo utaratibu wa kulipa watu binafsi au kampuni za wanaodaiwa kuwa ni za marafiki pasipo kufuata taratibu zozote za fedha.

Utata mwingine umeibuka katika kesi inayodaiwa kuwa ni ya kupanga ikimhusisha ofisa mstaafu wa jeshi aliyeishitaki TPB, ambako katika kesi hiyo walitumiwa mawakili wa nje kuitetea benki hiyo huku mlalamikaji akitetewa na kampuni ya uwakili inayomilikiwa na mmoja wa watendaji wakuu wa benki hiyo.
 
Benki ya Posta kuna mambo mengi sana, nadhani BoT chini ya Ndulu, itayaweza maana Ballali alikua mshikaji wa Kihwele. Lakini humo ndani kuna mazito zaidi ambayo huenda yakaanikwa katika kipindi cha ndani ya siku saba zijazo hata kama BoT hawatazibaini kwa kuwa zinawagusa vigogo wengine wazito nje ya Benki ya Posta.

TUSUBIRI TUSIKIE KAMA BAADA YA KUWAFUKUZA HAO WATASEMA ZIMETOLEWA NA NANI TENA, WATAWAMALIZA WAFANYAKAZI WAO WOTE KUMBE MCHAWI NI UFISADI WAO NA MFUMO WA MAWASILIANO WA SASA UNATOA NAFASI KWA KILA KITU KUWA WAZI. WAKO UCHI JF INAWAONA
 
JF inakuwa ya kwanza kwa kila kitu, Taasisi zote lazima zijifunze kufanyia kazi taharifa za JF badala ya kukanusha.
 
utasikia kitu kinachunguzwa lakini taarifa yake haitoki maisha.
 
Kama ni uchunguzi wa kawaida kwa nini iwe big deal. Vitu vingine ni kujishaua tu. CRDB imehusika kwenye EPA na RICHMOND lakini hatujasikia hao BOT wakifanya uchunguzi. Hii ndiyo Tanzania-the land ya ku-TANIA kila kitu
 
... Lakini humo ndani kuna mazito zaidi ambayo huenda yakaanikwa katika kipindi cha ndani ya siku saba zijazo hata kama BoT hawatazibaini kwa kuwa zinawagusa vigogo wengine wazito nje ya Benki ya Posta.


I hope the famous guy mwenye "akili sana" kwenye hili hayupo!!
 
labda Prof.Ndullu asichokijua ni kwamba mara baada ya wakaguzi wake kuondoka Kihwele na Jamaa yake Kapelega wamefanya mambo tena
 
Benedict Kapelega ambaye ni mwajiriwa wa shirika la posta,akiwa ni makamu mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi (Si mtendaji )amepelekwa kuchunguzwa afya India kwa Gharama inayofikia DOLLAR 35,000.00 za kimarekani zote zikiwa zimelipwa na Benki ya POSTA.
malipo yanahusisha per diem ya Kapelega,Mke wake na Nurse anayewasindikiza huu pia ni ufisadi
Bado hatujapata mgawanyo wa hizo Dollar Kati ya hao watatu,mara tutapopata tutawaelezeni ili umma uone jinsi Mafisadi hawa walivyojenga himaya zao na Kiburi cha hali ya juu kabisa
 
Kwanza inasemekana rufaa ya kwenda india imetoka kwenye hospitali binafsi iliyoko kariakoo,
Hili linazua maswali mengi sana kwa wenye busara,ina maana kariakoo kuna Hospital ya rufaa ? kuweza kumpeleka mgonjwa anayetumia mali ya umma moja kwa moja nje ya nchi ?
Pili iweje mwajiriwa wa shirika la posta apelekwe matibabu nje kwa gharama za Benki ya posta na si mwajiri wake ?
Nafuatilia kubaini uhusiano uliopo kati ya kihwele na kapelega ukiacha kwamba ndiye aliyemsaidia kupata u CEO kwa mlango wa uani
 
This time kila mahali patafunuliwa tuone uchafu na uozo uliojazana humo. Ka-benki kenyewe hata hakajawa na afya ya kutosha wameanza kukamega?? kweli kuna majitu yamepinda kinoma...Tatizo litakuwa lile lile wakaguzi wanapelekwa wakimaliza kazi ripoti inakaliwa then inaundwa timu kuwachunguza hao wakaguzi mpaka jua linazama ngoma inalala watu wamevuta mapene yao wasonga mbele... Mchezo wa kitoto kabisa hatufiki popote....
 
mmh kazi ipo, kwanza nasikia hii benki ya posta haija-qualify ku-operate kama Bank, kwa taarifa za BoT hii inatambuliwa kama "taasisi" ya fedha.
 
labda Prof.Ndullu asichokijua ni kwamba mara baada ya wakaguzi wake kuondoka Kihwele na Jamaa yake Kapelega wamefanya mambo tena


Hivi Tanzania kuna sheria kwelli ? Unajua hata huwa najiuliza inakuwaje mambo ya namna hii yanatokea ama ni kila kitu siasa tu ?
 
Kama kuna mtu anadai...si anatakiwa alipwe..utaratibu wa kulipana ndio tatizoo hapo ........suala la lu forge baruua hilo zitoo sana tusubiri"uchunguzi'maana mm tz kwa kupenda tume,uchunguzi....mechanism ili tusahau/........
 
Jamani kwa taarifa nilizonazo huyu jamaa anapeta na kuongezewa mikataba kwa sababu zifuatazo
1. Yeye na Apson ni marafiki wa karibu sana
2. Mke wa Kihwele ni binamu wa JK

WanaJF wenzangu nani anaweza kusema kitu hapo. Ndiyo maana anafanya mambo kwa kujiamini sana
 
Hii issue siyo ya kukurupuka inahitaji kuipanga vizuri kisha kuianika kwenye magazeti na kuifikisha bungeni, I hope hawataunda kamati ya kuchunguza anaziunda JK kila siku. Sasa ni wakati wa kuwachukulia hatua mafisadi ili wakome. Kama ni kazi wapo wengi wanaweza fanya kazi waliyongangania tena vizuri kabisa.
 
Back
Top Bottom