Ubadhirifu mkubwa Benki ya Posta

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Kama ilivyofikishwa...

Nawakilisha
 

Attachments

  • Benki ya Posta sasa.zip
    26.3 KB · Views: 654
Mkuu Invis.. shukrani tele..... Unajua ukiangalia haya yote yanayojitokeza inapelekea mtu kupata pich kwamba kwa kweli "deals/makampuni/iadara/wizara nk ambazo zinajulikana kama mali za uma zimekuwa zinatapanywa na wale wachache wenye meno...ooops wenye nguvu!!!

Mimi ni mmoja kati wale tunaosema labda ni "majungu" lakini jamani kama hata OCAG walisema kwamba kuna udhaifu mkubwa kwenye mambo ya "AUDIT" inepelekea kuamini kwamba lisemwalo lipo.......

Hya JF tuongoje tuone na tuendelee kuyajadili maswala mazito haya.....
 
Hizi ni tuhuma nzito kwa Bw Kihwelle. Ingefaa Media ikapata nakala. Kudos Invisible kwa kutufungua macho.
 
Kama ilivyofikishwa...

Nawakilisha

Asante mkuu, Nimeisoma yote, imeandikwa vizuri sana, nadhani lazima kitu kifanyike hapa kunusuru benki hii, ambayo nadhani inamtandao mkubwa nchini. Jamani nini Tanzania, kila sehemu watu wanapiga mapanga kwenda mbele...ufisadi... ufisadi .... Ikulu, mahakama, BOT, makampuni ya kiserikali, Wawekezaji, mikataba ... kote ni ufisadi ..kwenda mbele bado utahamia na magerezani kama bado .... Mkullo anatajwa na huko...kazi ipo
 
NImeisoma yote

Tunawashukur waliotuletea taarifa hiyo kwani kuna maswala kadhaa inabidi kuangaliw akwa undani mfano

1.Contract ya Kihwele
2.Mradi wa Ubungo Plaza
3.mambo ya supplies of stationaries

however, kuna swali kwa waandishi.

1. kesi ya Millioni 9 inayomusisha Mej.Gen Msataafu Sande Ligate!!!!!...hiikwa kweli imenishangaza......9m??!!...au figure ilikosewa!!

Tuhuma zengine, ni kuangalia utaratibu mzima wa kibenki juu ya ukopeshaji na tender awarding......ni vitu vinavyotakiwa kuangaliwa especially ktk maeneo yaliyoonyeshwa na waraka huu


Shukran sana Mkuu Robot
 
Tatizo sio kuumbua hizi kweli ila ni kupima ni mangapi yamelipuliwa hapa na nini kimetokea na kufanyika wahusika wamechukuliwa hatua gani.
Mwisho wa maradhi yote haya ni serikali ya CCM kupata usugu na ndio ukawakuwa watu wanaishi Tanzania na virusi vya maleria lakini hawaumwi wala hawapati madhara makubwa zaidi ya homa ya siku moja tu ,na wengine hata hawana habari kama wamekumbwa na virusi hivi mwilini ila wanajua kuwa wanaishi na virusi ,so long JF itakuwa mstari wa mbele katika kufichua uchafu huu ,ikiwa serikali haiambiliki wala wahusika hawana habari labda homa ya siku moja au mbili na halafu wanarudi kama sio na kutanua kwa jeuri zaidi,hamwoni kama mwisho wake watakuwa croniko.
Ni wazo tu.
Mwiba.
 
Tatizo sio kuumbua hizi kweli ila ni kupima ni mangapi yamelipuliwa hapa na nini kimetokea na kufanyika wahusika wamechukuliwa hatua gani.
Mwisho wa maradhi yote haya ni serikali ya CCM kupata usugu na ndio ukawakuwa watu wanaishi Tanzania na virusi vya maleria lakini hawaumwi wala hawapati madhara makubwa zaidi ya homa ya siku moja tu ,na wengine hata hawana habari kama wamekumbwa na virusi hivi mwilini ila wanajua kuwa wanaishi na virusi ,so long JF itakuwa mstari wa mbele katika kufichua uchafu huu ,ikiwa serikali haiambiliki wala wahusika hawana habari labda homa ya siku moja au mbili na halafu wanarudi kama sio na kutanua kwa jeuri zaidi,hamwoni kama mwisho wake watakuwa croniko.
Ni wazo tu.
Mwiba.

Nashukuru..mfano upo straight.Labda jamaa wamekunywa dawa za kinga so wao wanaogopa vipele tu kwa kung'atwa na mbu ila sio hayo malaria.
 
Naamini Mkurugenzi wa masoko anayetajwa hapa ni Imani Kajura na si huyu wa sasa- Mwinda Kiula ambaye amejoin hiyo bank in less than a year time wakati haya madeal yote yameshafanyika.Hiyo combination ya Kihwele,Imani Kajula na Nkuba ilikua inatisha kwa madeal machafu ya nguvu, they were altogether known as Boys II Men among TPB employees.
 
Baada ya kumaliza kusoma barua hiyo nikakumbuka maneno ya Mch. Mtikila....

"SAA YA UKOMBOZI NI SASA"
 
Kwa hiyo huyu Imani Kajula niwa kuangaliwa sana hata huko alikoenda NMB.

Jamani hivi tufanyeje ili Nidhamu + Uzalendo urudi serikalini na kwenye mashirika ya umma??

kila siku ukigeuka kila sehemu ni upuuzi tu
 
Tatizo ni mfumo mzima uliopo. Ufisadi kwenye mashirika ya umma unalelewa na viongozi walio serikalini. Benki ya Posta wajumbe wa Bodi huteuliwa na Waziri wa Fedha, na hata mwenyekiti wa Bodi anaweza kuteuliwa na Rais baada ya kupata pendekezo la Waziri wa Fedha. Once CEO/MD wa shirika akishamshika waziri anayehusika basi mambo yote huwa tambarare. Bodi itawekwa mfukoni na ufisadi utaendelea. Hizo barua ambazo zilikuwa zinakwenda Wizara ya Fedha ilikuwa ni sawa na kupeleka kesi ya nyani kwa tumbili, dont expect kupata haki yako. Wanajuana na wako kwenye mtandao wa kifisadi, ambao unaanzia kwenye shirika mpaka kwenye ngazi ya wizara na wakati mwingine mpaka Ikulu.

JK na serikali yake kuendelea kuwa na kigugumizi katika kushughulikia ufisadi kutawafanya hata hao mafisadi wadogo wadogo wawe na guts za kuendelea kutafuna, sana sana watajitahidi kujisogeza karibu na ma-godfather ili wahakikishe kwamba wanalindwa just in case of anything.

Bado tuna safari ndefu sana na mwisho wake haujulikani. Ukishakuwa na viongozi serikalini ambao waroho wa pesa kiasi kwamba hawaachii hata ka-deal ka shilingi milioni 10, basi ujue kwamba nchi imekwisha. Maana hakuna hata mmoja ambaye atatolewa mfano. Na hata wakipatikana wachache wa kutolewa kafara, hao wengine watatafuta njia mbadala ya kujipenyeza kwenye CCM na serikalini ili walindwe. Asilimia kubwa ya mafisadi wakubwa wana-connection serikalini ama kwenye chama na wengine wameamua kuingia Bungeni kabisa ili kutetea ufisadi wao.

Majambazi wa EPA akina Lukaza tumewaona mara nyingi kwenye blogs na magazetini wakipeana mikono na akina Lowassa na akina JK eti wafanya biashara wanaoshiriki kwenye kuchangia shughuli za maendeleo kwa kutoa michango ya shilingi milioni 3, na kumbe wamechota mabilioni ya shilingi kutoka BoT. Usanii mtupu ...

Kuitenganisha serikali na ufisadi ni kazi ngumu sana na kuitenganisha CCM na ufisadi pia ni ngumu sana. Siku hizi mafisadi wote wanakula na wale walio serikalini na pia wanakula na CCM. Utaenda kuwashitaki wapi ili sheria ichukue mkondo wake?

Swali la kizushi:
Mtendaji mkuu wa wizara ya fedha ni Katibu Mkuu (Hazina) ambaye ni Bwana Mgonja. Inakuwaje aendelee kuwa pale wakati kila kukicha taasisi zilizo chini ya wizara ya fedha zinakumbwa na uchafu mkubwa lakini yeye amebaki kuwa kisiki cha mpingo. Kuna nguvu gani inayomlinda? Juzi nimesoma kwenye ThisDay akiwa amenukuliwa wazi kwamba alimwagiza mwanasheria wa wizara ya fedha kusaini mkataba ambao ulikuwa na utata. Hivi hii nchi inakwenda wapi? Halafu unategemea walio chini yake wakiona ka-deal ka shilingi milioni 1 watakaachia?
 
umefanya kazi nzuri maana ni project hii utangulizi ,uchunguzi akinifu,hitimisho na mapendekezo.Na ipapendeza hata hoja zingine mtu akileta iwe au tuiweke katika mtindo huu.Inakuwa umelaani na kutoa njia ya kushughulikia tatizo.Sio kulaumu tu.
Sasa hawa wenye serikali yao si wanawebsite yao tukawamwagie hizi data kama wana moyo wakufanyia kazi hatafanyia.Ama ndio kama inavyosemekani nao huingia humu !?
 
Ama Kweli yanahitajika mapinduzi makubwa ya uongozi humu serikalini!Sijui mawazo ya UJIMA yatatuondoka lini Wadanganyika ili tusiendelee kukumbatia uchafu wa namna hii?
Hongera TANESCO kwa maandamano maana mlionyenyesha ukakamavu kudai maslahi yenu.Voksi populi voksi dei.

Hivi Kwenye fuko la fedha hapo hazina kwa nini kila kukicha huyu KATIBU MTENDAJI ANATUHUMIWA,ALAFU HAONDOKI,AU NDO KABEBA MIKOBA YOTE YA UCHAWI HUU UNAOTUSUMBUA?

Kwa desturi yaTZ ukisikia hivi huwa kuna asilimia fulani ya ukweli ingawa unaweza usiwe ukweli kamili,Lakini kuna namna ipo.
Kama watu hawana uchungu na mashirika yanayosaidia umma mbona vituko kabisa!

Who will come to propagate good the governance for sisiem? A leadership with discontent and dishonest that undermining the public opinion and dogmatic to be enlighten..Absolutely,the people are demanding changes that would have dramatic impact on the fate of this nation.
....2010.............................
 
Ukiangalia Vizuri Utakuta Hata Nyie Wanachama Wa Jf Mumeadhirika Na Ufisadi Huu Mnaamua Kuufuata Kwa Njia Moja Au Nyingine Huko Makazini , Mashuleni Na Sehemu Zingine Za Maisha
 
Haya mambo yamekuwa yakizungumzwa tu, nadhani unahitajika mkakati wa nini kifanyike kwa ajili ya ukombozi
 
Nasikia harufu ya Mustafa Mkulo imo Benki ya Posta, kabla hajawa Waziri. Wahusika hebu tupeni data zake, hasa mikopo aliyochukua na kufutiwa deni kiaina.
 
Back
Top Bottom