Ubachela

Mtayarishaji

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
291
199
Unakuta Mwanaume anakuwa yuko tayari kuingia kwenye uhusiano lakini mwanamke anakuwa bado. Anataka kuula ujana na yupo katika kile kiwango cha ‘kunguru hafugiki’.

Mwanaume hata afanye nini, yeye si kutulizwa akatulia. Si wanaume pekee, hata wanawake nao wanakutana na kisanga hiki.

Unakuta mwanamke yupo tayari kwa lolote, amechoshwa na maisha ya kuhangaika na dunia, anataka kuingia kwenye uhusiano wenye tija lakini wapi. Anaambulia patupu maana kila anayekutana naye, hana huo mpango.

Huu ndiyo ulimwengu ulivyo.

Mwanaume aliye tayari, anahaha kumpata mwanamke aliye tayari bila mafanikio. Vivyo hivyo mwanamke aliye tayari, naye anahangaika kila uchwao kumsaka mtu ambaye atakuwa baba wa watoto wake lakini naye anapishana naye.


Natafuta jinsi ya kuuaga UbaCheLa
 
Back
Top Bottom