Nchi gani ni nzuri kwa kozi za afya na gharama ya chini kwa mwanafunzi

tss

Member
Aug 31, 2023
73
38
Habari ndugu zangu ,Mimi ni mhitimu wa kidato Cha sita,Katika maisha yangu ya elimu nilikuwa natamani niwe daktari wa moyo( cardiologist) sasa matokeo yangu so mazuri kivile kwa PCB nina phys-E,chem-D na bios-C,sasa Kwa elimu yetu ya Tanzania physics nmeanguka kw ajili ya kukidhi vigezo vya kusoma udaktari nchini,sasa nilikuwa naona nitafute nafasi Kwa nchi zingne nikasome .Je nawezaje kupata scholar ship itakayoniwezesha kusoma nje ya nchi,au nisaidieni nchi yenye vyuo vya gharama ya chini kusoma na maisha ya kuishi.Nawasilisha wakuu
 
China, Japan, India na Uturuki.

Jaribu na Australia... hii nchi wengi hawanaga habari nayo ila ina utamu wake alafu ipogo kimya sana
 
Pia mkuu angalia vyuo vya Cuba 🇨🇺, hapa gharama ni kidogo ila quality ya elimu yao sio quality sana,PA kuanzia sio mbaya, soma Cuba then nenda SA uka I polish vema,good luck
 
China, Japan, India na Uturuki.

Jaribu na Australia... hii nchi wengi hawanaga habari nayo ila ina utamu wake alafu ipogo kimya sana
Asante mkuu maana nilikuwa nataka kusoma kozi ya cardiology,japo sijajua kama ni kozi inayotambulika hapa kwetu tz
 
Pia mkuu angalia vyuo vya Cuba , hapa gharama ni kidogo ila quality ya elimu yao sio quality sana,PA kuanzia sio mbaya, soma Cuba then nenda SA uka I polish vema,good luck
Asante kaka
 
Asante mkuu maana nilikuwa nataka kusoma kozi ya cardiology,japo sijajua kama ni kozi inayotambulika hapa kwetu tz
cardiology isitambulike mkuu utachekwa.Dr Janabi si cardiologist mkuu.Ila huwezi soma cardiology kwa sasa direct tika formsix....unatakiwa usome shahada ya kwanza ya udaktari(medical dokta),miaka 5 na mwaka mmoja wa internship halafu ukasome miaka mingine 3 au minne ya ubingwa wa magonjwa ya ndani(physician)uwe daktari bingwa halafu usome miaka mingine 3 ya super specialist kwenye moyo ndo utakua umekua daktari bingwa wa moyo.
 
Afghanistan, Iran, Gaza, Morocco, Misri, Tunisia & Algeria.
Chagua nchi mojawapo wapo hapo☝
 
Connection ya kupata vyuo inakuwaje? Na ni nchi gan ambayo ni affordable na inayotoa elimu yenye ubora?
 
Kwa matokeo hayo ukirudi bongo utakutana na lungu la TCU plus Baraza la Madaktari. Labda usifanye kazi bongo.
Kifupi ni kwamba kama huna vigezo vya kusoma kozi fulani Tz ukakimbilia nje ukirudi husajililiwi kufanya kazi hapa.
 
Hakuna kurudi ukisoma unakaza huko maana ukirudi huku ni njaa Kali tu Bora ujitose tu huko huko Kwa walioendelea kiuchumi
 
Kwa matokeo hayo ukirudi bongo utakutana na lungu la TCU plus Baraza la Madaktari. Labda usifanye kazi bongo.
Kifupi ni kwamba kama huna vigezo vya kusoma kozi fulani Tz ukakimbilia nje ukirudi husajililiwi kufanya kazi hapa.
Bora umemwambia ukweli ajue. Kutafuta short cut ni mbaya sana. TCU imeweka mpaka utaratibu wa kuulizia kuhusu kusoma vyuo vya nje na vyuo ambavyo vinatambulika Tanzania. Zingatia vigezo vilivyo wekwa nchini hata kama unataka kusoma nje ya nchi. Pia zingatia chuo kinacho tambulika.
 
Sio kweli....kikubwa kabla ya kuondoka aende TCU kupata kibali cha kusoma hio kozi.....
Wakimruhusu anasoma bila shida yoyote tuu
 
Kwa matokeo yake hawezi kuruhusiwa kusoma Udaktari labda kozi nyingine.
Haelewi huyo ndio huwa wanadanyana mwisho wa siku wanalia lia kama wajinga. Umekosa vigezo hapa unaenda kutafuta short cut. Nenda ukiwa na minimum requirement ya kusoma programme husika hapa nchini, labda ushindani umefanya ukakosa nafasi au umependa mwenyewe kwenda nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom