Uandishi wa vitabu Tanzania

snochet

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
1,407
1,110
Habari wanaJf,naomba kuuliza,nikitaka kutoa kitabu hapa Tanzania kuhusu jambo Fulani(lolote),ili kupata ISBN number na kitabu change kupitishwa,ninatakiwa kupitia hatua gani?je kuna gharama yoyote?mwenye azoefu au idea ya uandishi wa vitabu hapo nchini kwetu tafadhali a-post chini ya thread hii.natanguliza shukrani
 
isbn hutolewa na maktaba na taifa kwa sasa, na huuzwa kwa bundle ya isbn 5 kwa 30000
 
ukihitaji huduma ya Printing, designing na text setting ya kitabu chako sema tu, mimi nafanya kazi hzo
 
Habari wanaJf,naomba kuuliza,nikitaka kutoa kitabu hapa Tanzania kuhusu jambo Fulani(lolote),ili kupata ISBN number na kitabu change kupitishwa,ninatakiwa kupitia hatua gani?je kuna gharama yoyote?mwenye azoefu au idea ya uandishi wa vitabu hapo nchini kwetu tafadhali a-post chini ya thread hii.natanguliza shukrani

Nitafute kwa hii number 0713584890, nitakufanikishia kwa gharama ya tsh. 30,000/= kiasi ambacho ni kwa ajili ya kulipia pale maktaba. Binafsi nipo kwenye kampuni ya Printing n Publications hapa Kariakoo Dsm. Gharama zetu ni very affordable, na huduma ni nzuri, trust me. Tuwasiliane kwa maelezo zaidi.
 
Hivi hii shughuli ya utunzi wa vitabu inalipa kweli maana nimeshangazwa na huyu jamaa yangu shigongo hatoi tena vile vitabu vyake na kuacha kuendelea kuandika kwenye magazeti Nina li stori langu nimeliweka ndan tu nataka siku moja nitafutie umaarufu na mimi nitambulike rasmi hapa Tanzania.
 
Mkuu sisi wasomaji ndio tunawakwamisha waandishi. Watanzania hatuna utamaduni wa kusoma vitabu na nadhani ndio maana hiyo biashara hapa kwetu inaonekana kwua ni biashara kichaa
 
Nimekuelewa kaka sasa nimeandika idea za maisha ya kibongo sijui kama kitafit kwenye international market baada ya kuwa kimetafsiriwa?
 
Waone pia na viongozi wa TAPA (Tanzania Publishers Association), akima Paschally Mayega au akina Shaffi Adam Shaffi.

Ila inawezekana isiwe inalipa sana kwa kuwa mtandao wa kuchapa, hatimiliki na usambazaji bado hauko transparent hapa kwetu. Nilimsikia juzijuzi Munir Zacharia wa Channel Ten akimhoji Shaffi Adam Shaffi juu ya mstakabali wa stahili za mwandishi wa zamani Mohamed Salim Ahmed ambaye vitabu vyake kama vitatu hivi vinachapwa na kusambazwa na makampuni ya Nairobi. Wakati warithii wake huko Unguja wanaishi maisha ya kifukara.
 
Nitafute kwa hii number 0713584890, nitakufanikishia kwa gharama ya tsh. 30,000/= kiasi ambacho ni kwa ajili ya kulipia pale maktaba. Binafsi nipo kwenye kampuni ya Printing n Publications hapa Kariakoo Dsm. Gharama zetu ni very affordable, na huduma ni nzuri, trust me. Tuwasiliane kwa maelezo zaidi.
nitakutafuta. naandika kitabu changu fulani.
 
kitu ambacho mimi pia sijakielewa, je? nikiandika kitabu changu kwa hapa tz, kinahitaji tena kupitiwa mikononi mwa watu wengine mfano wahariri fulani hivi ili wakiruhusu kuingia sokono, labda kwasababu hawataki watu walete vitabu pumba au huwa inakuwaje....naweza aandika kitabu changu tu, nikaki rewrite, edit every thing na kukipeleka kwa publisher? what about usambazaji? makampuni yepi ni wasambazaji wazuri kwa hapa tz jamani?
 
ukihitaji huduma ya Printing, designing na text setting ya kitabu chako sema tu, mimi nafanya kazi hzo

Mkuu nimeipenda hii nina vitabu vyangu viwili ndo naelekea mwisho katika utunzi nahitaji nikuone tuingie ka mkataba kwa hili kwani nilishindwa pa kuanzia na nilitaka kuacha kazi hii.e-mail yangu;ptlwongola@gmail.com
 
Nashukuru kwa kuwapata wadau wa uwandishi na uchapaji wa vitabu hata mm nina materials mengi sana kwa ajili ya wajasiriamali na naamini yatawafaa sana pindi tu nitakapopata muda nitaanza.
 
Wakuu mi pia naomba ushauri wenu.....hivi ukiandika kitabu cha somo kinachofundishwa darasani (kufuata sylubus),mfano kitabu cha History au Geography,je ili kitabu chako kipitishwe wizara ya elimu inahusika?
 
Nitafute kwa hii number 0713584890, nitakufanikishia kwa gharama ya tsh. 30,000/= kiasi ambacho ni kwa ajili ya kulipia pale maktaba. Binafsi nipo kwenye kampuni ya Printing n Publications hapa Kariakoo Dsm. Gharama zetu ni very affordable, na huduma ni nzuri, trust me. Tuwasiliane kwa maelezo zaidi.

Nitakutafuta mdau nijue gharama zikoje, maana tayari niko na mswada wa kitabu ukiwa umekwishahaririwa, kazi iliyobaki ni production tu.
 
Back
Top Bottom