Uandishi wa CV katika kuomba kazi

Uandishi wa CV katika kuomba kazi

yenyewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
621
Reaction score
94
Natumaini mko njema ndugu zangu.
Binafsi huwa nina maswali mengi kuhusu nafasi ya CV katika kuitwa kwenye usaili na pia kupata kazi.
Nadhan kwa wengi wasioitwa kwenye usaili suala la uandishi wa CV huwa linachangia sana. Hii hutokana na kukosekana kwa taarifa (information muhimu) katika CV.
Mfano kuna kipengele cha "Testimonial" huwa najiuliza kama ni cha muhim sana au la. Pia kuhusu "Referees" huwa najiuliza kama huwa hiki kipengele kinafatiliwa sana na kuwasiliana nao hao watu ili mtu aweze kuitwa kwenye usaili.
Nadhan hayo ni kati ya yale mengi yanayotuangusha sana sisi watafta ajira.
Kama kuna mengine tuongezee pia wanaoelewa vizuri kuhusu uandishi wa CV mnakaribishwa kutuelekeza wapi tunakosea.
Karibuni wadau.
 
asante kwa kukumbushana mzee.
hiko kipengere cha "testimonial" ndio kipi?

ujue CV ina uandishi wa aina nyingi sana. ila framework ndio zinafanana. kuna watu wana weka kwa table, kuna watu just wana mention tu etc, ila mambo ya muhimu ni:
1.personal info.
2.education background
3.work experience
4. publications
5. other skills
6. referees

sasa wapo watakao ongeza mbwembwe nyingine kibao.

mchango wa cv na cover letter kwenye kuitwa kwenye interview ni mkubwa sana. usifikirie vyeti vyako tu ndio vitaonesha how smart you're. wanajua nao kwamba elimu ya siku hizi ni madesa tu.

kama job seekers, tukubali kujifunza kutoka sehemu mbalimbali/watu mbalimbali juu ya uandishi wa cv, cover letter na usaili kwa ujumla. kuna threads humu kibao zinaongelea kuandika cv, cover letter, kujiandaa na interview, kujibu maswali etc. ukitumia search engine hapo juu utafaidi sana mkuu.

:focus: hapo kwenye referees, nasikia sometimes wana wasiliana nao, ila kwenye hatua za mwisho za kukuajiri. sio kwamba eti wanavyokuita tu kwenye interview waanze wasumbua hao referees, hapana. wakisha jihakikishia na u eshapita written na oral, so wanataka kuku hire ndio wanaweza kucontact na hao wadhamini wako.
 
Asante sana mkuu Secret Service . Testimonial ni kipengele kinachofata baada ya experience. Huu ni uthibitisho kutoka kule ulikofanya kazi ili kuonesha kuwa information ulizotoa kuhusu experience yako ni sahihi. Kwahiyo unaiandika kwenye CV kama ilivyoandikwa na mwajiri au mkuu wako ulikofanya kazi au kujitolea.
Sasa ndo sina uhakika kama ni lazima.
 
Last edited by a moderator:

mi ni fresh grad mzee, sijawahi kuweka, ila nimeitwa interview mara kadhaa.
 
Last edited by a moderator:
Katika kuandika CV inabidi uwe makini sana,tatizo siku hizi watu wanakopi na sometimes wanatumia maneno ambayo hata hawayajui yanamanisha nini.
Cv yako ikiwe inajieleza vizuri utaweza kuitwa kirahisi,kwa mfano hutakiwi kuna na CV moja,kwa kuwa kila kazi ina mahitaji tofauti,CV yako inabidi uwe unirekebisha kulingana na mahitaji ya kazi husika,ikiwezekana ondoa mambo unayoyafahamu ila hayahusiani kabisa na hiyo kazi,kumbuka CV ikiwe ndefu alafu imejaa madudu inaonyesha hukuelewa wanataka nini.
Jitahidi unachoandika kwenye CV uwe unakifahamu walau kwa 50%,mtu mwingine anaweka vitu alivyofanya zamani na kwa wakati huu haviwezi kabisa,hapo ndiyo matatizo yanaanza akiulizwa maswali.
Kama wengine walivyochangia referees huhusishwa mwishoni wakitaka kukupa job offer na si wakati wa kuitwa interview.Kwa walioko makazini sijui kama unajua umuhimu wa kutunza "performance appraisal" yako make sure you have a copy,hii ni testimony tosha kuhusu utendaji wako wa kazi.Sasa kama kazini kwenu hivi vitu havipo ,am sorry.
Kitu kingine job seeker wanachemka ni marefaree wao,mtu kamwandika referee hata mawasiliano naye hana,hata kumjulisha kwa sasa yuko wapi au anatafuta kazi hafanyi,wengine hata kuwatumia refarees wao CV zao hawawatumii.Sasa referee anaweza ulizwa maswali yakawa magumu sababu yako wewe hukumshirikisha mapema.So make sure referees wako wanajua kwamba ulienda kwenye interview sehemu fulani ili incase wakipigiwa wawe on the same page.
 
you hit the nail on the head...
 
Hivi nilazima kuweka kipengele cha Testimony kwenye CV kweli na Kwa mfano mtu hajawahi kuajiliwa ndio kwanza katoka chuo/shule hiyo Testimony atakuwa kaitoa wapi?

Alafu nimeona Secret Service ameweka kipengele cha Publications hii kitu unakua unaongelea nn?
 
Asanteni sana na hii thread inaelimisha,

Mimi ombi langu ni moja tu, naombeni mueke sample ya good cv hapa tuende sawa!
 
Si lazima uweke testimony kama huna hizi ni format tu ,si lazima alichoweka mwenzako na wewe uweke wakati unajua huna.
Publications kama say mtu ana say PHD labda kuna vitu aliandika(paper) au Research na kikawa published si kuandika na kukaa navyo ndani.I may not be correct but I am somewhere close to.
 
hicho hakina umuhim kwa fresh frm school ila kwa mtu unaeonesha umefanya kaz sehem nyingi ni muhim mana kitakueza kwa nn umeacha hzo kaz je kwa wema tu au kuna msara umefanya
 
Hivi nilazima kuweka kipengele cha Testimony kwenye CV kweli na Kwa mfano mtu hajawahi kuajiliwa ndio kwanza katoka chuo/shule hiyo Testimony atakuwa kaitoa wapi?

Alafu nimeona Secret Service ameweka kipengele cha Publications hii kitu unakua unaongelea nn?

sorry nime late reply boss.

hapo kwenye Publications mimi naongelea kama umewahi fanya projects, au umewahi andika reports/research flani na ukaipresent maybe chuoni wakati unapata degree ya kwanza, masters au doctorate.

Pia wengine wanaandika makala, projects na kuzipresent katika sehemu mbalimbali.

Sijui umenisoma? Vipi unaionaje mzee, au nayo sio necessary? (I am fresh graduate, job seeker so sio mkali sana mzee kwenye hizi mambo).
 
Hyo muhmu hata mi.nimeandika.. Hata hvyo inategemea na kaz unayoomba.. Cv hubadilika kulingana na requirements za post husika
 
Back
Top Bottom