Uanaume Si Ndevu.

Uanaume Si Ndevu.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
UWANAUME SIYO NDEVU.

1)Moja ni uvumilivu,na kutokata tamaa.
Ili mbele kula mbivu,na kuacha kuzubaa.
Kujilinda na uvivu,na kuiacha zinaa.
Uanaume si ndevu,ni matendo na tabia.

2)mbili wala si mchoyo,kwa kile alichopata.
Hata kama kiboyo,hushinda akitafuta.
Siyo mpiga mboyoyo,na mkia akifyata.
Uanaume si ndevu,ni matendo na tabia.

3)tatu mwingi wa upole,tena alie jasiri.
Asopiga makelele,alojawa na usiri.
Daima msonga mbele,kikamanda jemedari.
Uanaume si ndevu,ni matendo na tabia.

4)siyo mkurupukaji,japokuwa hutokea.
Hajifanyi mjuaji,kwa lile asolijua.
Tena yeye mkanyaji,baya akishuhudia.
Uanaume si ndevu,ni matendo na tabia.

5)basi kuwa mchamungu,uzipate sifa hizi.
Tafuta chini uvungu,mwaume siyo mwizi.
Wa kale tangu na tangu,katika hiki kizazi.
Uanaume si ndevu,ni matendo na tabia.

Shairi=UWANAUME SI NDEVU.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashairi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom