Ukuta sawa lakini unajengwa juu ya ardhi haujengwi nchini ya ardhi.Huko ardhini inaweza kujengwa tunnel ya kutokea nje ya ukuta huo na madini kutoroshwa.Natoa angalizo kwa serikali kama mtaalam wa Sekta ya madini.Hapo Mererani huko chini migodi inaingiliana wanaita "mitobozano",huo ukuta wa juu unaweza usisaidie sana madini yanaweza kupita chini kwa chini na kuvuka huo ukuta kwenda vitalu vingine ambavyo siyo A,B,C wala D.Kwangu mm ningekuwa Serikali ningejenga ukuta eneo lote la Mererani na kufanya patrol mita 100-200 kuzunguka huo ukuta kuhakikisha kwamba hakuna shimo lolote linatokeza nje ya Ukuta huo.Aidha,madini ya Tanzanite ningeyafanya nyara ya Serikali.Ukikutwa nayo isivyo halali,wafa.