Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,400
Jana Rais John Magufuli aliamuru kujengwa ukuta kuzunguka eneo la Mererani na kulinda madini ya adimu duniani ya Tanzanite ili kuwezesha upatikanaji wa kodi itokanayo na mauzo ya madini hayo kwa urahisi.
Ukuta huo utakaokuwa na eneo la kilomita za mraba 15, utazuia eneo zima la mgodi la kilomita za mraba 81.99 na litazuia maeneo yote ya uchimbaji ya A, B, C, na eneo D.
Sambamba na ukuta huo pia kutajengwa barabara nzuri ya lami ambayo itatokea kwenye machimbo hayo hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro yaani KIA.
Uamuzi wa kujengwa kwa ukuta huo inasemwa kwamba umechelewa yaani kwamba ukuta huo ulipaswa kujengwa mwaka 2002 baada ya timu ya washauri wa kitanzania na wawakilishi wa wanunuzi wakubwa wa madini hayo kuafiki kwamba kulikuwa na haja ya kujengwa kwa ukuta huo kwa wakti ule.
Timu hiyo iloitwa Tanzanite Tueson Protocol ilishauri kujengwa ukuta huo kudhibiti biashara haramu ya madini hayo na mitandao yake yote.
Hiyo ilitokana na mabadiliko mbalimbali ya sheria za kuhusiana na ugaidi katika nchi mbalimbali baada ya ripoti mbalimbali kuhusisha biashara ya hiyo ya madini na masuala ya ugaidi ambapo kiongozi wa magaidi duniani kwa wakati huo Osama Bin Laden alikuwa akihisiwa kujishirikisha na biashara hiyo.
Kujengwa kwa ukuta huu kutadhibiti si tu wafanya biashara halali bali pia wafanyabiashara wenye leseni na kuondoa biashara haramu ya magendo ya madini hayo.
Tanzanite ni madini ambayo yanapatikana nchini Tanzania pekee na yana soko kubwa nchini Marekani kiasi cha asilimia 99.
Lakini madini hayo yanasafirishwa moja kwa moja kwenda nchini Marekani kupitia katika nchi za Thailand, Kenya na India huku serikali ya Tanzania kwa miaka Zaidi ya 15 ikiwa inakosa mapato yake halali kutokana na upotevu huo.
Kujengwa kwa ukuta huo pia kutasaidia shughuli hizo za uchimbaji kudhibitiwa kirahisi, kupatikana fursa nzuri za wafanyabiashara wa katika maeneo hayo kama mama ntile na migahawa mingine, mahoteli, klabu za usiku na hata biashara za magari!
Biashara zote hizi zinawezesha kupatikana kwa kodi za mapato kwa kuwa wafanyabiashara hawa wote watakuwa wamesajiliwa rasmi katika mfumo wa TRA kwa wote kuwa na namba maalum za TIN.
Pia mgodi huo wa Marerani utawezesha wafanyabiashara waingizaji wa vifaa mbalimbali vya uchimbaji wa madini hayo kutoka nje ya nchi kuweza kufanya hivyo kuwa kutumia mfumo mmoja wa anuani ya eneo hilo hivyo hata kama mtu anaagiza mzigo kutoka marekani, au Uchina basi uaandikwa anuani ya Mererani.
Je, mwana JF unachukuliaje uamuzi huu wa kujengwa kwa ututa kudhibiti eneo lote za Mererani?
Je, faida zake zingine kubwa ni zipi?
Je , kuna hasara yoyote ile?
Tafadhali toa maoni yako bila kuingiza siasa.
Kama kawaida yangu napenda majadiliano yenye tija.
Karibu.