Uamuzi wa Kesi ya Mkataba Wa Bandari na DP WORLD kutolewa 07/08/23, Mahakama yamsifu Mwabukusi kwa weledi

... mara baada ya Wakili Mwabukusi na timu yake kuhitimisha hoja zao Mahakama Kuu Mbeya; presidential jet imeonekana ikichana mawingu fasta na kutua Dubai thereafter the Kingdom of Saudi Arabia! Haijafahamika mara moja ni kwanini!
Alafu ngoma kimya kimya bila watanzania kujulishwa kuwa TANZ01 anavuka mipaka ya nchi yake.
 
Alafu Kuna wapumbavu wengine wa uvccm wanakuja majukwaani na kumtukana wakiri Msomi Mwabakusi kuwa anaingia Mahakamani na kwenye mahojiano akiwa amelewa. Hawajui hata rafudhi za watu wa Mbeya zenye kuonesha msisitizo katika hoja.
Kongole Mwabakusi kwa kutuwakilisha vyema vijana wa nyanda za juu kusini especially Mbeya.
Achana na hao chawa
 
Nawaombea hawa majaji wapate ujasiri kama wa majaji wa Kenya, wasiingize mambo ya kisiasa au kuogopa mhimili mwingine. Maamuzi yao ndio mstakabali wa maisha yetu na vizazi vijavyo.
Hujui majaji wa Kenya wameiingiza Kenya katika mgogoro mkubwa, na sasa Rais wao Ruto anatukanwa ovyo na mahakama inadharaulika au ufatilii yanayojiri Kenya? Hadi yule mama Jaji Mkuu kuna siku aliomba wananchi wawasamehe, akiwa kanisani?
 
Mkuu hakuna mahakama za kuumua tofauti na matakwa ya serikali. Na hata ikitokea muujiza mahakama ikaamua tofauti na serikali, hiyo hukumu haitatekelezwa.
Mala hii umeisha jua mwisho
 
Taarifa kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya inasema kwamba Uamuzi wa Kesi hiyo inayogusa maslahi ya Taifa , utatolewa 8/7/2023 , hii ni baada ya Mahakama hiyo kumaliza kusikiliza hoja za Mawakili wa Pande zote .

Hayo yameelezwa na Jaji Ndunguru , ambaye alizungumza Kwa niaba ya Majaji waliosikiliza shauri hilo .

Kwa kipekee Jaji Ndunguru amemwagia sifa nyingi wakili Boniface Kajunjumele Mwabukusi kwa kuonyesha Weledi wa hali ya juu kuanzia mwanzo wa kesi hadi mwisho .

View attachment 2702367
Kwa kipekee Jaji Ndunguru amemwagia sifa nyingi wakili Boniface Kajunjumele Mwabukusi kwa kuonyesha Weledi wa hali ya juu kuanzia mwanzo wa kesi hadi mwisho .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawaombea hawa majaji wapate ujasiri kama wa majaji wa Kenya, wasiingize mambo ya kisiasa au kuogopa mhimili mwingine. Maamuzi yao ndio mstakabali wa maisha yetu na vizazi vijavyo.
Tatizo lako na wenzio hili mahakama ionekane imetenda haka wapinga bandari wapewe ushindi mawazo mgando
 
Hapo ndipo nitakapoona kweli mhimili mmoja umejichimbia juu ya mihimili mingine nyakati zote. Huku case inayomhusu, yeye huhooo kimya kimya Dubai mpaka Saudia
Magufuli alisema serikali ni miimili 3 lakini kuna 1 imejichimbia chini zaidi
 
Mkuu hakuna mahakama za kuumua tofauti na matakwa ya serikali. Na hata ikitokea muujiza mahakama ikaamua tofauti na serikali, hiyo hukumu haitatekelezwa.
Usikariri!!!

Mchungaji Mtikila aliigaragaza sirikali mara nyingi mahakamani Kwa Katiba hii hii!!
 
“Kuna kipingele kwenye Mkataba Hakizungumzwi sana, “Early Project Activities” Yaani kuna shughuli zitaanza kabla ya Utekelezaji wa Mradi, Sina Ushahidi Lakini 80% Shughuli Hizo zimeanza, Ni hatari unamruhusu vipi Mtu kuingia kwako Kukuchunguza kabla ya Utekelezaji?” - @IssaShivji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom